Uliwahi kusikia hizi tamaduni?

TIASSA

JF-Expert Member
Jun 17, 2014
2,893
3,423
(1) Kuzika walio kufa na walio hai,

Hii ilitokea hayo maeneo ambayo yalikuwa na machifu., chifu akifa wanachaguliwa vijana kama wanne wa kumsindikiza chief.

(2) Kuwatupa mapacha,

Naskia hii ilikuwa sana huko kilimanjaro ambapo waliamini mapacha ni nikosi na nuksi kwenye ukoo hivyo waliwatupa mbali kongorongoni au kwenye bonde refu.

(3) kuwafunga watoto viuzi vyeusi kiunoni hii niliiyona sana huko kanda ya ziwa.. Nasijui inamaanisha nini

(4) nahii nyingine ya mtoto aliyezaliwa alafu mama yake akafa basi yule mtoto alichukiwa sana maisha yake yote na watu walikuwa wakimwambia kuwa amemuu mama yake..

Zipo na nyingine nyingi unaweza ukatujuza unazo zifahamu na wewe pia.. Za hapa Tanzania na nche ya hapa
 
Kufagia Usiku Ni Mkosi.
Kuita Chumvi Usiku Ni Mkosi
.
Mwanaume Kulia Kwenye Kwenye Sufuria Hutaoa.
Mwanamke Kukalia Kinu Hutazaa
.
Ukizaa Mtoto Kabla Ya Siku Zake. Marufuku Kulia.
Ukiwa Unapika Alafu Moto Ukawa Unatoa Sauti Fulani Hivi Ujue Kuna Wageni.
Ukiwa Unaenda Sehemu Gafla Ukakutana Na Wingi Wa Sisimizi Basi Huyo Mtu Humkuti.
Marufuku Kuchukua Nyama Kabla Ya Wakubwa.
Kuku Akichinjwa Watoto Marufuku Kula Firigisi Na Maini.
 
Unapoenda safari ukiondoka nyumbani alfajiri mtu wa kwanza kukutana naye akiwa m'me safari yako ni ya neema akiwa m'ke safari inamkosi.
 
Kule Tabora kama jina lako Kashindwe basi kama kuna radi kali ulitakiwa kutoka ndani na kwenda nyuma ya nyumba kutukana!tusi lolote halafu unarudi ndani!
 
Shangazi yangu alipika makande ya njegele yakagoma kuiva akaniita nikavuanguo zote mbele yamafiga ndo yakaiva eti jogoo akiwika mlangoni kunawageni ukifagiliwa miguu hutaoa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Shangazi yangu alipika makande ya njegele yakagoma kuiva akaniita nikavuanguo zote mbele yamafiga ndo yakaiva eti jogoo akiwika mlangoni kunawageni ukifagiliwa miguu hutaoa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

na mimi nitakuita siku moja
 
Msimu wa mvua ukifika halafu isiwepo kwa kipindi kirefu wazee wa mambo ya jadi wanakwenda makaburini na vibinti vyenye miaka kati ya 6 na 10 vikaimbe na kucheza vikiwa vitupu huku chakula kikiandaliwa na kuliwa huko, kama sijakosea sana hiyo shughuli inaitwa kulangalanga kwa wale wanaokumbuka vizuri zaidi yangu waweza kutoa maelezo ya kina
 
Mtoto akitanguliza meno ya juu(wanayaita ya plastics)ni laana kwahyo anatupwa hiyo ni kilimanjaro
 
watoto kucheza kombolela mchana, utaota manyoya kwenye ulimi,
kumwangalia baba yako sehemu za siri mshombombo hautasimama kamwe, nk
 
Kule Tabora kama jina lako Kashindwe basi kama kuna radi kali ulitakiwa kutoka ndani na kwenda nyuma ya nyumba kutukana!tusi lolote halafu unarudi ndani!

Dah nmecheka sana hii tamaduni kama kweli ipo! Kwa mfano ww ndo unaambiwa ebu nenda kaitukane radi...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom