Uliwahi kumuimbia mpenzi wako?

Uliwahi kumuimbia mpenzi wako?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,856
Hebu tutazame kidogo fani hii ya zamani kidogo,je kumuimbia mpenzi nyimbo zozote kuna weza kuwa dawa ya kuongeza mapenzi? Tujadiliane pamoja.

SHAIRI=wewe ni wangu.

1>wewe ndie nyota yangu,usiku wamulikia.
Uniachi peke yangu,ukanacha ninalia.
Nikabaki peke yangu,mbali ukanikimbia.
Nakupenda ewe wangu,kwengine siwezi kwenda.

2>wewe ndie mwezi wangu,usiku waangazia.
Ewe ndie taa yangu,mwanga wanimulikia.
Wewe ndie nuru yangu,wewe ndo langu pazia.
Nakupenda ewe wangu,kwengine siwezi kwenda.

3>wewe ni asali wangu,nyuki sitowafukuza.
Kuvunja mzinga wangu,ni jambo nisiloweza.
Nikabaki peke yangu,ulimwengu kuniweza.
Nakupenda ewe wangu,kwengine siwezi kwenda.

4>ewe ndio shuka langu,lanilinda kwa baridi.
Wewe ndie koti langu,daima sitokaidi.
Takulinda vazi langu,ili nije kufaidi.
Nakupenda ewe wangu,kwengine siwezi kwenda.
. . . . . . . . . . . . . . . .

Nini maoni yako?
 
tatizo nilikua nikimuimbia lazima asinzie.
sikuwa nafurahishwa na hiyo hali.
 
Mimi nikimuimbia kichwa kinamuuma........je ni ugonjwa gani huu dr......?....
 
Ukimuimbia wangu ujue siku hiyo hupati papuchi analala usingizi wa pono na hataki usumbufu tenaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom