Ulishawahi kusingiziwa kitu?

Ulishawahi kusingiziwa kitu?

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
22,165
Reaction score
43,854
Katika maisha kuna mambo mengi sana watu wengine hukumbwa na visa na mikasa mizito mpaka kufika hatua ya kuona dunia ni chungu.

Je wewe ushawahi kusingiziwa kitu au Jambo fulani kuwa umefanya wakati sio wewe ?Je nini kilitokea? Karibuni
 
Mara nyingi sana. Ila moja ambayo sitakuja kusahau ni pale niliposingiziwa kuwa nina mahusiano na dada mmoja aliyekuwa mfanyakazi mwenzangu wakati huo. Na aliyezusha hilo ni boyfriend wake.

Ilibidi nifanye kibingwa baada ya kupita siku na mgogoro huo kukuzwa na kuniuma sana. Nilimwomba yule dada akanielewa ikabidi tuanze maisha ya uhusiano.

Ananipenda hadi leo japo nimeoa naye anaye mchumba ambaye yuko Ughaibuni kwa sasa.

Mungu tu anisamehe kwa hilo
 
Duuh ukaamu ufanye kweli sasa...!! Haa ha... we noumah
 
Mara nyingi sana. Ila moja ambayo sitakuja kusahau ni pale niliposingiziwa kuwa nina mahusiano na dada mmoja aliyekuwa mfanyakazi mwenzangu wakati huo. Na aliyezusha hilo ni boyfriend wake.

Ilibidi nifanye kibingwa baada ya kupita siku na mgogoro huo kukuzwa na kuniuma sana. Nilimwomba yule dada akanielewa ikabidi tuanze maisha ya uhusiano.

Ananipenda hadi leo japo nimeoa naye anaye mchumba ambaye yuko Ughaibuni kwa sasa.

Mungu tu anisamehe kwa hilo
Pole
Hakuna kitu kinaumiza kama kusemewa uongo, ingawa wengi husema ukweli unauma, kwangu uongo huniumiza zaidi.
 
Si kwako tu,uongo unauma zaidi hasa kama hauna uhusiano wowote wenye uhalisia na uzushi huo
 
Nilisingiziwa kuiba na mtoto wa kaka angu ,japo alinizidi umri...
kaka angu (Mtoto wa mama mkubwa) ana uwezo hasa.
Tulikua na mama na wifi yangu

sasa tukawa tumeenda kwa sherehe kwao, baada shuguli kwisha ndio ikatokea hio sintmfahamu hela imepotea tena ef10 tu...

aisee walinishupalia mno kuwa nmeiba ,niliumia sana sana....
nilijiskia dhihaka mno...
yani nilijipa maswali, bila majibu,kwasababu mama angu masikini labda ndio maana wanaona mm ndo nastahili kuiba.aisee nilisononeka sana.

baada ya mda wakaja kugundua alieiba ni mdogo wake,wakaja tukaombana msamaha nikasamehe ila sitasahau kwakweli,na uyo dada alimaliza chuo akaishia kuwa malaya tu ,huyo dogo mwizi hadi leo...
pamoja na pesa alizonazo baba yao watt washenzi mno
 
Watu wanaangaliaga na watu wa kuwasingizia jamani!

Labda wananisingizia kwa chinichini sijawahi kusikia!
 
Nilisingiziwa kuiba na mtoto wa kaka angu ,japo alinizidi umri...
kaka angu (Mtoto wa mama mkubwa) ana uwezo hasa.
Tulikua na mama na wifi yangu

sasa tukawa tumeenda kwa sherehe kwao, baada shuguli kwisha ndio ikatokea hio sintmfahamu hela imepotea tena ef10 tu...

aisee walinishupalia mno kuwa nmeiba ,niliumia sana sana....
nilijiskia dhihaka mno...
yani nilijipa maswali, bila majibu,kwasababu mama angu masikini labda ndio maana wanaona mm ndo nastahili kuiba.aisee nilisononeka sana.

baada ya mda wakaja kugundua alieiba ni mdogo wake,wakaja tukaombana msamaha nikasamehe ila sitasahau kwakweli,na uyo dada alimaliza chuo akaishia kuwa malaya tu ,huyo dogo mwizi hadi leo...
pamoja na pesa alizonazo baba yao watt washenzi mno
Aisee kuna ndugu ni ishu...!! Me nkiwahi kwenda kwa ndugu yangu nkaibiwa pesa lakini sikutaka kusema kitu ili nisije leta sintofahamu pale kwao afu nlikuwa mgeni...
 
Mimi nilisingiziwa na maza flani jirani na home kwetu.

Nilikua nasoma boarding tangu o'level mpaka a'leve na nilikua kuonekana home ni mara chache sana, sasa huyu mama akahamiaga kitaani kwetu akawa ananionaga wakati wa likizo tu.

Nimemaliza cha sita, narudi home mara jirani kuna kabinti karuzi nikakatupia voko, nikawa najilia taratibu. Mama yake akajua, na yule mama jirani mwingine ni shosti ake.

Basi wakamwambia binti, unadanganywa na huyo jamaa hapo sio kwao kwanza anakujaga kusalimia tu kwao ni Mbeya huko hapo kwa mjomba wake tu.

Doh, yani nilikua nikirudi home likizo basi kumbe yule mama alikua anadhani nimetokea mbeya kuja kusalimia ndugu..

Nilicheka sana
 
Back
Top Bottom