Ulishawahi kukataliwa baadae ukagundua ilikuwa sio sehemu sahihi?

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,363
6,903
Kuna wakati mambo yanatokea unajiuliza mbona kwangu tu. Kumbe ulikua unaepushwa na majanga makubwa zaidi au utakuja kupata kitu kizuri chenye mafanikio zaidi. Yapo mambo mengi yanaweza kukupata ukafikiri huna thamani lakini baadaye ukashukuru akasema ee Mungu asante.

1. Ulishawahi enda interview ukakataliwa kwamba huwezi ukaja kupata kwingine pazuri zaidi?

2. Ulishawahi kwenda kazini ukakataliwa? ulijisikiaje.

3. Ulishawahi kataliwa na watu au wanakuchukia tu bila sababu.

4. Ulishawahi kataliwa na mchumba, rafiki, au mke baadae ukapa mtu bora zaidi hadi ya yule wa mwanzo akajilaumu kukupoteza?

5. Ulishawahi fanya kazi, biashara, ikagoma baadae ukakuta haikuwa sahihi kufanya hicho kitu?

Kuna wakati unavyotaka wewe katika maisha haviji kama unavyotaka wewe unajiuliza kwa nn.

Kuna wakati unaweza kukata tamaa mwisho wa siku ukashangaa unafanikiwa tu bila wewe kujua imekuaje tena. Kwa hiyo usihofu kila kitu na zama zake.

Jambo likwama Muombe Mungu akutie nguvu, arudishe furaha yako.

Hata kama kuna janga lilikupata usilipize kisasi. Kaa kimya kuna wakati yataisha tu na utasahau.
 
Kuna wakati unaweza kukata tamaa mwisho wa siku ukashangaa unafanikiwa tu bila wewe kujua imekuaje tena. Kwahiyo usihofu kila kitu na zama zake.

UPO SAHIHI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom