Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Jambo la pili ambalo ni “Mujarab” ni kwamba; miongoni mwa watanzania ambao ni “Smartest” ni Rais wetu Mh. Magufuli. Katika muktadha wa mada hii, hoja hii inajengwa kwa sababu moja kubwa. Mheshimiwa ni moja ya watanzania wachache sana ambao wana uthubutu wa kusimamia kile wanachoamini kwa gharama yoyote ile. Yaani yeye anachoamini kuwa ni sahihi; atakisimamia kwa uwezo wake wote. Hii ni sifa kuu ya kwanza kabisa ya mtu “Smart”
Miongoni mwetu, kuna watu wanaoamini au wanaodai kuwa ni “Smart” na wengine wanadai ni wasomi lakini ni vigumu kufahamu wanaamini nini au hawaamini nini na wanasimamia nini hasa. Wao hawa, hata kutoa mawazo yao (wanayoamini ndio sahihi) hadharani wanaogopa; achilia mbali kuyasimamia au kuyatekeleza, na wale wanaotoa wengi wao mawazo watakayotoa leo na watakayotoa kesho kwenye jambo lile lile yanakinzana.
Sasa unajiuliza, hivi ni mtu gani ambaye ni “smart” au anayedai kuwa msomi lakini anashindwa tu kuelewa concept rahisi kwamba mawazo ambayo yako ndani ya kichwa cha mtu lakini hayajatolewa na kuwa “Shared” kwa jamii na wala hayafanyiwi kazi na mtu yoyote akiwemo aliyenayo; mawazo hayo hayana maana yoyote?
Kuna hoja kuwa, hata watu wakitoa mawazo waliyo nayo hayafanyiwi kazi. Sasa swali la kujiuliza, kama kweli wewe ni “Smart” kwa nini wewe usitoe hayo mawazo yako halafu ukaanza kuyafanyia kazi katika level yako kulingana na kile kilichopo ndani ya uwezo wako ili angalau kuonesha mfano?
Halafu pia tunafikiri tuko “Smart” lakini tunashindwa kuelewa jambo moja muhimu na rahisi sana kueleweka kuwa,ili kufanikiwa; haihitajiki mawazo yako yote ya kubalike. Inahitajika wazo lako moja tu likubalike hata kama umetoa mawazo 10,000.
Ikumbukwe kuwa hata kama unaomba kazi kwa mfano, huhitaji kupata kila kazi unayoomba, unahitaji kupata kazi moja tu kati ya mamia ya kazi unazoomba. Utakuwa mtu wa ajabu kama utaomba kazi 400 halafu unataka upate zote muda huo huo unadai wewe ni “Smart” halafu usipopata unaacha.
Unatoa ushauri mara tatu, halafu ushauri wako wenyewe umechanganya na matusi humo humo, ushauri unaoutoa wewe mwenyewe ungeweza kuanza kuufanyia kazi katika level yako lakini hujafanya kitu, halafu unaancha unadai sasa husikilizwi utafanyaje? Hivi kama tunakata tama kirahisi hivyo, ikitokea siku ukipewa majukumu yeye controversies kibao unafanya nini?
Tunasahau kuwa hata wanasayanisi waliofanya uvumbuzi wa aina mbali mbali, walifanya majaribio yaliyofeli mara maelfu lakini walihitaji jaribio moja tu lilikubali na kuibadili dunia na wamefanikiwa mara nyingi?. Kwa hiyo kama wewe kwa mfano una wazo ambalo unadhani ni zuri, halafu kwa kuwa ulishalifanyia kazi mara moja ukashindwa kasha ukaacha, au ulishatoa ushauri mara moja ukakataliwa ukakata tamaa nab ado unajiaminisha kuwa wewe ni mtu “smart” Ujue unajidanganya. Sifa ya kwanza ya mtu yoyote smart ni kusimamia anachoamini katika shida na raha.
Ni kweli tuna changamoto nyingi ila ili tutoke tulipo na kupiga hatua, ni lazima tutambue hasa mzizi wa tatizo ni nini na kushughulika na mzizi, kuja na majibu marahisi rahisi hakuwezi kuwa na faida ya maana.
Ikumbukwe, wewe ukidhani uko “Smart” au ni “msomi” lakini hutekelezi wala kusimamia mawazo yako; wale ambao unawaona sio smart watasimamia na kutekeleza mawazo yao, na kwa msingi huo, wao ndio smart hata kama wewe unawaona kinyume chake.
Kama una mawazo ambayo unaamini ni mazuri lakini huna ujasiri wa kuyatoa hadharani, wenye mawazo ambayo wewe unadhani ni mabaya watayatoa na yatafanyiwa kazi, na kwa kuwa hamna mbadala; hayo yatakuwa ndio mawazo bora zaidi katika eneo na muktadha huo.
Jambo hili la kusimamia kile mtu anachoamini kwa uwezo wake wote ni jambo muhimu. Kwa hiyo ni vyema tukajifunza jambo hili jema kutoka kwa Mheshimiwa.Hata hivyo, ni muhimu Zaidi kuendelea kujifunza ili kujiridhisha kama yale tunayoamini ni sahihi maana wakati mwingine pia unaweza kuamini jambo na baadae ukagundua ulichoamini hakikuwa sahihi.