Ulipokuwa mgodi wa Buzwagi kujengwa Kongani maalumu ya viwanda

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,895
Reaction score
11,788
Serikali imelitangaza eneo ulipokuwa mgodi maarufu wa dhahabu wa Buzwagi kuwa sehemu ya kujengwa eneo maalumu la kongani ya viwanda “Buzwagi Special Economic Zone” baada ya kuhitimishwa kwa shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.

Hatua hiyo imewekwa wazi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na maeneo maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri na kuongeza kuwa tayari serikali kwa kushirikiana na wawekezaji imeanzisha Buzwagi Special Economic Zone ambayo ina mpango wa kuwa kitovu cha uzalishaji, usindikaji na usambazaji wa bidhaa za mgodi kwa soko la Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.

Kwa upande wake Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameongeza kuwa zaidi ya viwanda 30 vitajengwa katika sekta mbalimbali ikiwamo nishati, elimu, uzalishaji bidhaa za migodini, bidhaa za kuchakata madini na bidhaa zingine zinazotumika kwenye sekta ya madini ikiwemo vipuli vya viwandani.

"Zaidi ya wawekezaji 30 wameonesha nia ya kuanzisha viwanda katika eneo la Buzwagi na tayari mwekezaji mmoja aitwaye East Africa Conveyors Supplies ameanza kuzalisha bidhaa zinazotumika migodini.” Amesema Mavunde

Mbali ya mwekezaji huyo, Mavunde ameongeza kuwa kampuni ya Tembo Nickel inatarajiwa kuwekeza katika ujenzi wa tajenga kiwanda cha kuongeza thamani madini ya metali (Multi-Metal Refinery Facility) kitakachotumia teknolojia ya kisasa ya Hydromet kuyeyusha kwa joto kali.

Mgodi wa Buzwagi ulikuwa ukimilikiwa na kampuni ya Acacia Mining sambamba na migodi ya Bulyanhulu na Mara ambayo kwa pamoja mwaka 2014 ilizalisha aunsi 719,000 za dhahabu.
FB_IMG_1766348173620.jpg
 
Hii inchi ni tumekula hasara za mfululizo hadi fedheha na aibu kuhadithia. Sasa viwanda kwenye mashimo ya machimbo yaliyokwisha mali ya madini vinakwenda kuwekwa wapi hapo pumbavu zao hawa?
 
Yani mgodi unachimbwa hadi madini yanaisha na wananchi bado ni masikini. Faida yote imeishia kwa mzungu. Dah, sisi ni wapumbavu sana
 
Nani akaweke uwekezaji katika mashimo ya madini, msituone mafala.
 
mambo ya chifu mangungo wa msovelo

waafrika akili hatuna ukweli ndio huo
 
Nani akaweke uwekezaji katika mashimo ya madini, msituone mafala.
Hii nchi hata sijui kama itakuja ku escape umasikini. Kuna uwezekano hadi tunakufa Tanzania itabaki kuwa third world country kwa mambo ya kipumbavu kama haya
 
Wameshachukua utajiri wote tumeachiwa ardhi tupu waje wachina wajenge viwanda vitakavyochafua hewa
 
Serikali imelitangaza eneo ulipokuwa mgodi maarufu wa dhahabu wa Buzwagi kuwa sehemu ya kujengwa eneo maalumu la kongani ya viwanda “Buzwagi Special Economic Zone” baada ya kuhitimishwa kwa shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.

Hatua hiyo imewekwa wazi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na maeneo maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri na kuongeza kuwa tayari serikali kwa kushirikiana na wawekezaji imeanzisha Buzwagi Special Economic Zone ambayo ina mpango wa kuwa kitovu cha uzalishaji, usindikaji na usambazaji wa bidhaa za mgodi kwa soko la Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika ya Kati.

Kwa upande wake Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameongeza kuwa zaidi ya viwanda 30 vitajengwa katika sekta mbalimbali ikiwamo nishati, elimu, uzalishaji bidhaa za migodini, bidhaa za kuchakata madini na bidhaa zingine zinazotumika kwenye sekta ya madini ikiwemo vipuli vya viwandani.

"Zaidi ya wawekezaji 30 wameonesha nia ya kuanzisha viwanda katika eneo la Buzwagi na tayari mwekezaji mmoja aitwaye East Africa Conveyors Supplies ameanza kuzalisha bidhaa zinazotumika migodini.” Amesema Mavunde

Mbali ya mwekezaji huyo, Mavunde ameongeza kuwa kampuni ya Tembo Nickel inatarajiwa kuwekeza katika ujenzi wa tajenga kiwanda cha kuongeza thamani madini ya metali (Multi-Metal Refinery Facility) kitakachotumia teknolojia ya kisasa ya Hydromet kuyeyusha kwa joto kali.

Mgodi wa Buzwagi ulikuwa ukimilikiwa na kampuni ya Acacia Mining sambamba na migodi ya Bulyanhulu na Mara ambayo kwa pamoja mwaka 2014 ilizalisha aunsi 719,000 za dhahabu.
View attachment 3518835
kwann kila mrad wa ccm lzm utangazwe na haumalizik
 
Kabla ya buzwagi kulikuwa na wachimbaji wadogowadogo walifaidika sana lakini walipokuja wawekezaji wakawafukuza wazawa kama wakimbizi.wazungu wameimaliza dhahabu na wenyeji kubaki MASIKINI wa kutupwa.Ni Bora wangewaacha tu wenyeji wangenufaika zaidi kuliko huu uhuni aliotufanyia kikwete na genge lake la wahuni
 
mavunde anatafuta investors kwenye ardhi isyo na mali bali sumu ya kutosha kuku ua baada ya 10 yrs
 
Back
Top Bottom