Ulipaji wa NSSF kwa wafanyakazi wa sekta binafsi

Walichonifanya aisee Mungu anawaona yaani unahitaji kusubiri miezi 18 baada ya kumaliza kuchukua fao la kukosa ajira, mbaya zaidi staff wao ni watu wa kuogopa changamoto kwa maana ya kumwambia mtu ukweli yaani mambo yapo hivi na hivi lakini wanakuwa wanakwepa kwepa kama wanasiasa
Kiongozi ilikuchukua muda gani kupata FAO LA kutokuwa na ajira baada ya kujaza na kuwakabidhi fomu zao?
 
Na hiyo miezi 18 sio kama wanakupa kile kilichobaki isipokuwa utakuwa na hiyari ya kuiamisha michango yako kwenda kwenye kundi LA wachangiaji wa hiyari mpaka utakapofikisha umri wa kulipwa pesa yako ambao ni 55 years.
Ila wanasema angalau ukiingia kwa hiari hiyo miezi 18 ikipita ni rahisi kuichukua hela yako tofauti kama haijaisha hiyo miezi 18 maana wanadai mpaka uwe na sababu ya msingi ndo uandike kuiomba hiyo hela japokuwa hata hizo sababu za msingi ukiwa nazo bado wanaziona sio za msingi
 
Kwa ujumla nahisi hawa jamaa huwa wanachukua hela ili wale maana nazidi kuuliza watu tofauti tofaut but napewa majibu ya kusikitisha sana. Kuna jamaa alikuwa anaendesha gari la shule X alikuwa analipiwa ikafika laki 9. Hizo hela alizungushwa mpka akahisi kukata tamaa ila aliishia kupata lak 5. Wanazingua sana hao jamaa. Maana kuweka ni rahisi kutoa ndo kasheshe ingekuwa kutoa ni kama kuweka mbona mambo raha sana
 
Mkuu, na miezi yote sita walikulipa vizuri kwa mtiririko maalum?
Yes iliingia kwa mtiririko mzuri yaani kila mwisho wa mwezi salio lilikuwa linasoma, kulikuwa na delay ya siku 2 mpaka 5 na si zaidi ya hapo. Na ilivyoisha miezi 6 tu na salio wakakata. Kwani vipi kwa upande wako mkuu maana hawa jamaa sio watu wazuri sana inapokuja suala la kulipa wanachama wao
 
Nami nimeingia kwenye dhoruba hilo hilo Mkuu.
Walianza kunilipa Feb 9, lakini ya mwezi March mpaka sasa bado sijaona salio. Naendelea kusubiria!
Ila hawa jamaa wanachotufanyia sio haki kabisa. Basi ni bora hata wangebadilisha sera zao ili ziruhusu hata mwanachama kukopa kwa dhamana ya michango yake, ingekuwa nafuu zaidi kuliko kukalia pesa zetu huko.
 
cc yuga

hilo ndilo Jibu hata mm nilihisi hivyo , ingawa si mwajiriwa wa Sekta yoyote wala serikali, ukishaajiriwa maeneo hayo ni lazima mwajiri atoe taarifa zako na kukupelekea michango yako
Uko sawa, akajaze form ya NSSF mapema Ili apate kitambulisho cha NSSF na namba ya account yake ya NSSF Ili iwe rahisi kuangalia kila mwezi Kama pesa zako zimefika NSSF na ukiacha mwajili anakukata anabaki nazo na huwezi kumudai maana Sheria inataka ukazichukulie NSSF na si vingine.
 
Basi wewe ulikuwa Terminated maana uki resign hakuna kitu kama hicho mpaka uzee.

Contract iliisha mkuu, uki-resign wanasemaje kuhusu fao la kukosa ajira? Maana mtu anapo-resign si anakuwa katoa sababu either ugonjwa au anaenda kumuuguza mzazi wake au shule
 
Hawa nssf hawapo humuj!wake watupe majibu mtu Aki terminate mkataba ama aka resign inakuaje kuaje?
 
Hawa nssf hawapo humuj!wake watupe majibu mtu Aki terminate mkataba ama aka resign inakuaje kuaje?

Kwenye controversial huwa hawajibu na kila staff anajifanya sio msemaji. Ukiwapongeza faster wanakuja na kila mtu anakuwa msemaji wa kile ulichopongeza
 
Mku walikupa fao lako lote sio kwani na mm ndo natafuta kazi nikikisa nianze harakati za madai
Mafao hawatoi yote, kinachofanyika ni kukupa 33% ya salary yako kwa miezi 6 baada ya kuacha kazi, mfano kama unalipwa 1,000,000 watakupa kila mwezi around 330,000 kila mwezi kwa muda wa miezi 6.

Hivyo nakushauri kama upo kijiwe ichukue kabisa hiyo hela maana ukiiacha siku ambayo unaanza kuichukua na utakapomaliza hiyo miezi 6 utasubiri mpaka ipite miezi 18 ndo uanze process ya kuchukua mkwanja uliobaki tena

Ila kuna baadhi ya post mfano Drivers, Office Assistant yaani zile hazihitaji elimu ya juu sana wanatoa japokuwa mtu akienda wana discourage kiaina
 
Vipi kwa sisi wa sekta binafsi?
Kuna usumbufu wowote wakati wa kutoa.

Mimi sijaajiriwa lakini nataka kuweka akiba.
 
Vipi kwa sisi wa sekta binafsi?
Kuna usumbufu wowote wakati wa kutoa.

Mimi sijaajiriwa lakini nataka kuweka akiba.

Hiyo haina shida kwenye kutoa kwani hata sie ikifika miezi 18 baada ya kulipwa fao la kujitoa unaingizwa kwenye upande wa michango ya hiari (hapo ndo inakuwa ruksa kutoa mkwanja wako). Kama ni kuchangia kwa hiari haina shida
 
Back
Top Bottom