Ulinzi shirikishi kura shirikishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulinzi shirikishi kura shirikishi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Nov 14, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Ndugu wana JF, ulinzi shirikishi una manufaa mengi kwa jamii – hasa kuwalinda wananchi na mali zao na kuwafanya waishi kwa amani. Hata hivyo, ulinzi shirikishi ukitumiwa vibaya utazaa kura shirikishi – kwa maana ya kukipendelea chama kinachoongoza serikali.

  Katika kunusanusa kwangu nimekutana na mtu ambaye anasema: “Ikitokea ulinzi shirikishi ukatumika vibaya utaleta kura shirikishi.” Nimependa kutumia phrase hii kwa vile nimeona a;iyesema ametumia ubunifu. Na mtu huyo alisema kwa vile structures za ulinzi kutoka juu hadi chini zina mfumo kama ilivyo hapa chini, basi ni wazi kwamba ukitumiwa vibaya utanufaisha chama kinachoongoza serikali wakati wa uchaguzi.

  Sababu alizozitoa huyo jamaa ni kama ifuatavyo hapa chini. Nimejaribu kuchukua maneno yake verbatim na kwa hiyo sikuweza kuelewa kirefu cha kila acronym. Hivyo nimeamua kuzitumia acronyms zake kama nilivyosikia. Kama wachangiaji wengine wanaweza kumchallenge au kueleza kwa namna nzuri zaidi ni kitu chema. Nanaelewa kirefu cha acronyms chache! Anyway, mtu huyo alidokeza kama ifuatavyo:

  1. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kitaifa: President.
   • IGP
   • CDF
   • CNS
   • PM
   • Rais wa Zanzibar
  1. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa: RC
   • RPC
   • RPO
   • RSO
  1. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Wilaya: DC
   • OCD
   • DPO
   • DSO
  1. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kata: Mlinzi wa Amani wa Kata
  Wajumbe:...

  Kama kuna mtu mwenye maelezo tofauti na haya, please, atueleweshe maana kufanya hivyo ndiko kujifunza! Swali, je maelezo yake ni sahihi au hapana?
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hujaeleweka. Ulinzi shirikishi upi unaozungumzia? Structure uliyotoa inahusika vipi na kura shirikishi? Nini maoni/mawazo yako wewe kwa hicho ulichoandika?
   
 3. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kombo, maoni yangu ni haya:

  1. Ulinzi shirikishi ambao ni effective ni ule unaowashirikisha wananchi wote - kila mmoja anakuwa mlinzi wa jirani yake. Nchi nyingine kama Uingereza unaitwa ‘good neighbourhood'. Ulinzi huu unafanyika kwa namna hii: mwananchi anapomwona mtu anayemtilia mashaka sehemu alipo, anawajulisha watu wa nyumbani hapo ili wajiridhishe kama ni mgeni wao au la na waweze kuchukua hatua kama na wao wana mashaka.

  Ulinzi wa aina hii una mafanikio kama kila mtaa utakuwa na utaratibu mzuri wa kupeana habari. Ulinzi unaohusu kikundi fulani cha vijana kama walinzi wa usiku (kama inavyoonekana ikifanyika hapa Tz) hauna tofauti na sungusungu, ambayo haikuleta mafanikio sana (walau sehemu ninakotoka mimi).

  2. Kuhusu ulinzi shirikishi na kura shirikishi kama alivyo‘coin' mtu niliyem‘quote' alichokuwa anazungumzia ni kwamba ulinzi ukianza kuwa wa kikundi fulani cha vijana ni rahisi sana kuwa‘influence' na hasa wakati wa uchaguzi na hivyo kuanza kuvunja miiko ya utaratibu mzima wa ulinzi shirikishi.

  Hii ndiyo changamoto ya ulinzi shirikishi kama inavyoonekana ikifanyika maana vijana watajiunga na vikundi vya ulinzi shirikishi wakiwa na matarajio fulani kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawana ajira (ni jobless) na huenda baadhi yao hawana rekodi nzuri mtaani kwao.
   
 4. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Magobe umejieleza vizuri nashangaa kwanini ulishindwa kuanza na hoja hizo badala ya kuegemea ideas za mtu mwingine ambazo hata hivyo imekushinda kuzi-own.

  Aina ya ulinzi shirikishi inayofanyika hapa nchini ni police-centred jambo ambalo linasababisha wengi wa vijana (wananchi) kukacha kujiunga nao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuogopa kulipiziwa visasi na watakaowafichua kujihusisha na uhalifu kwa kuwa bado kuna askari wanaotoa siri.

  Tunahitaji people-centred type of community policing if this whole thing is to be sustained.

  ...bado nakushauri urekebishe post ya kwanza. Unaweza ukahamisha maoni yako na kuhoji sustainability ya ulinzi shirikishi chini ya usimamizi (100%) wa polisi ambao kila kukicha wako barabarani wanawapiga mabomu wananchi wanaowategemea wawape taarifa za wahalifu na washiriki doria.

  Uingereza na America aina hiyo ya ulinzi huitwa "neighbourhood policing" ama "community-oriented policing". Sina hakika sana na urahisi wa kuwatumia vijana hao kisiasa kwani ninavyowafahamu baadhi yao ni "wahalifu waliookoka" na wengi ni "radicals" kwenye maeneo wanakoishi.

  Ni maoni tu, huna ulazima wa kuyachukua.
   
 5. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kombo, nashukuru kwa maoni yako. Hata kama sikuyaweka vizuri mwanzoni nadhani ndiyo maana ya mjadala kwamba wachangiaji wengine kama wewe wanaweka maoni yao na hatimaye tunaboresha wazo la mwanzoni. Nimefurahi kuona kama hata wewe unaliona hilo la ulinzi shirkishi ambao ni POLICE-CENTRED wakati tunaoutaka ni PEOPLE-CENTRED (community policing). Police-centred policing will never work! Hata viongozi wetu waje na lugha nzuri kiasi gani - ulinzi wa aina hii hautafanikiwa kamwe maana umeundwa kutokana na polisi wanavyotaka uwe na siyo kutokana na matatizo ya wananchi (their needs). Ulinzi shirikishi utadumu kwa muda tu kisha utakuwa kama wa sungusungu.
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, ni kama tuko kwenye transition hivi kutoka sungusungu kuelekea polisi jamii, bado masuala mengi muhimu hayajakaa sawa. Leo ukimpata polisi na kumwuliza nini maana ya polisi jamii/ulinzi shirikishi unaweza kucheka pekeyako kama chizi. Hata wao hawajui tunaelekea wapi kwenye falsafa hiyo.
   
Loading...