Ulinganishi CCM huku na CHADEMA kule

Ulinganishi CCM huku na CHADEMA kule

bendaki

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
952
Reaction score
346
Ndugu wana JF
Nimeguswa tena na hili la wanachama wa vyama hivyo viwili hapo juu kuhamia kutoka upande mmoja na kuhamia mwingine. Ni kweli mmoja anahama kutoka pa bovu na kwenda pazuri hasa hawa wanaotoka CHADEMA na kwenda CCM?

Niliamini na nina amini kuwa wanao kuwa Chadema na au upande wa upinzani kwa ujumla wao ni katika dhana ya kuupotezea uwepo wa chama kimoja kutawala nchi na kufikia hata hatua kikawa na kujiamini kikajiamulia kushika hatamu.

Hivi vitu viwili vya "CHAMA KIMOJA TU NA CHAMA KUSHIKA HATAMU" ndivyo vilivyo tudumaza miaka mingi na tukaendelea kuwa nchi maskini ndani ya utajiri mwingi tulio jaliwa na Mungu.

Nisijue kuwa kuna watu makini wasio ona kuwa Pamoja na kukubali kuwa Tanzania iachane na mfumo wa chama kimoja na tuwe na mfumo wa vyama vingi ili nchi ipate maendeleo kumekuwepo na upinzani wa kiwango cha juu ili hali ibakie ile ile ya chama kimoja?

Angalia jinsi demokrasia ya mfumo wa vyama vingi ilivyo chukuliwa na CCM tangu 1992, Wapiga kura walitishiwa bila sababu kuwa kuchagua vinginevyo ni kuleta kuuana kama Rwanda, tutakuwa kama Misri, Libya , NK NK ili wananchi wajawe na woga waishi na chama kimoja katika mfumo wa vyama vingi yaani wanaonyeshwa maisha ya kistaarabu kwa maendeleo yao lakini wao wanang'ang'ania kutokuwa tayari kuwa wastaarabu na kuendelea kudumazwa akili japo walienda shule. Wachochezi wa hali hii walikuwa na bado ni CCM.

CCM iling'ang'ania kutokuwa na Katiba ya uhuru na demokrasia ya vyama vingi wakati wa kuandaa Katiba Mpya, wao CCM waliandaa ya kwao na kuikataa ya Warioba ambayo wanaanchi waliitaka ilikuwa ni kwa nini?

Ilikuwa wawe na Katiba itakayolinda masilahi yao. Maslahi ya wanani? Wao wachache wanaojiita WENYEWE> Yaani maamuzi ya nani awe diwani yawe mikononi mwa mtendaji wa kata. Mbunge aamuliwe na Mkurugenzi wa Wilaya ambaye anakuwa kwa ngazi hiyo ni kada wa CCM> Raisi aamuliwe na mteule wake yaani Kamishena wa NEC> Ili mfumo mzima ubakie chini yao ili kila kitu kiendeshwe kikada na Ndiyoooo, Yapiteeeeee nk nk

Yaani pamoja na ubovu wake CCM iendelee kuwepo.
Ubovu gani? Kutokuwa na umakini wa kujiendesha kama watu wenye weredi.

Mfano uwe unataka kujenga nyumba yako kwenye kiwanja fulani unacho kimiliki. Utangaze zabuni za kujenga watu wajinadi na Mmoja ashinde zabuni. Unaingia naye mkataba kukujengea na wewe unajiendea Ulaya kuendelea na shughuli zako za siku zote. Unarudi baada ya miaka mitano, pamoja na kuwa ulilipa pesa zote za ujenzi ukute ulijengewa GOFU, utajisikiaje.

Uje kuchunguza ukute waliojenga hawakuwa na ujuzi, walikuwepo ongezeko la watu hewa kujenga lakini muda wote wa miaka mitano mjengaji hakuona kuwa ni tatizo yeye kula pesa zako tu. Hata aseme atajirekebisha namna gani kama una akili timamu, hukulishwa limbwata, hauko kama nyumbu, kondoo nk utamuacha aendelee kukujengea?

Sasa huko ndiko kunaweza kuwa kimbilio la wenye kuipenda TANZANIA?
Kuna nini wanakimbilia?

Watanzania kiwanja chetu ni Tanzania. Siku zote anayeshinda zabuni kutujengea ni CCM kwa vipindi vingi vya miaka mitano mitano. Mpaka leo nyumba iliyojengwa ni gofu. Uchumguzi umetuhakikishia kuwa hawana WEREDI. Ilikuwaje wana wajenzi HEWA na kwa muda wote wasio kuwepo yaani HEWA?

Ilikuwaje walipewa nafasi ya ku-recruit waka-recuit wasio na sifa yaani wengi wao ni vyeti vya kugushi na wamekuwa wakiishi nao tu. Na kwa muda wote tumekuwa tukiwaona ni wajanja wajanja wa maneno na huku wao ni debe tupu? Mtu na akili yako unaweza kuhamia kwa watu wa namna hiyo badala ya kuwakimbia?

Imenipa taabu nikaona Wana JF niwaulize.
Kuna mtu anayefikiri kuwa kuna haja ya kuendelea kuwaamini CCM kama taasisi katika mazingira hayo?
 
CCM hawatakiwi kuaminiwa hata chembe,

Ni miaka 50 sasa ya uhuru bado tuna tafuta dawati za kukalia watoto shule ya msingi na wengi tu wanakaa chini,

Ni miaka zaidi ya 50 ya uhuru wameshindwa kumtua bibi jembe kijijini,pembejeo hakuna na akivuna hao hao CCM wanataka wampige,

Ni miaka zaidi ya 50 ya uhuru hatuna majengo yanayoridhisha ya madarasa ya wanafunzi,

Zaidi ya miaka 50 huduma za Afya ni duni sana ndo maana watu mpaka wanalala nje kusubiri Matibabu ya meli za wachina,

Miaka yote hiyo ya uhuru hatuna sera ya taifa yaani tunasimamia nini tumekuwa watu wa kurukaruka tu kama kuku aliyekatwa kichwa

Miaka yote hiyo CCM wapo madarakani wizi,rushwa na ufisadi umeshamiri kwa kiasi kikubwa tena miongoni mwa hao hao viongozi wa CCM

Hao wanaojiita wazalendo wakati ndo waliotuingizia hasara kama taifa kwa maamuzi ya kukurupuka leo hii ndo wazalendo

Hao hao wazalendo mnaowaita leo ndo ma-organizer wa kupigwa risasi watu wasio na hatia
 
Ndugu wana JF
Nimeguswa tena na hili la wanachama wa vyama hivyo viwili hapo juu kuhamia kutoka upande mmoja na kuhamia mwingine.
Ni kweli mmoja anahama kutoka pa bovu na kwenda pazuri hasa hawa wanaotoka CHADEMA na kwenda CCM?
Niliamini na nina amini kuwa wanao kuwa Chadema na au upande wa upinzani kwa ujumla wao ni katika dhana ya kuupotezea uwepo wa chama kimoja kutawala nchi na kufikia hata hatua kikawa na kujiamini kikajiamulia kushika hatamu.
Hivi vitu viwili vya "CHAMA KIMOJA TU NA CHAMA KUSHIKA HATAMU" ndivyo vilivyo tudumaza miaka mingi na tukaendelea kuwa nchi maskini ndani ya utajiri mwingi tulio jaliwa na Mungu.

Nisijue kuwa kuna watu makini wasio ona kuwa Pamoja na kukubali kuwa Tanzania iachane na mfumo wa chama kimoja na tuwe na mfumo wa vyama vingi ili nchi ipate maendeleo kumekuwepo na upinzani wa kiwango cha juu ili hali ibakie ile ile ya chama kimoja?

Angalia jinsi demokrasia ya mfumo wa vyama vingi ilivyo chukuliwa na CCM tangu 1992, Wapiga kura walitishiwa bila sababu kuwa kuchagua vinginevyo ni kuleta kuuana kama Rwanda, tutakuwa kama Misri, Libya , NK NK ili wananchi wajawe na woga waishi na chama kimoja katika mfumo wa vyama vingi yaani wanaonyeshwa maisha ya kistaarabu kwa maendeleo yao lakini wao wanang'ang'ania kutokuwa tayari kuwa wastaarabu na kuendelea kudumazwa akili japo walienda shule. Wachochezi wa hali hii walikuwa na bado ni CCM.
CCM iling'ang'ania kutokuwa na Katiba ya uhuru na demokrasia ya vyama vingi wakati wa kuandaa Katiba Mpya, wao CCM waliandaa ya kwao na kuikataa ya Warioba ambayo wanaanchi waliitaka ilikuwa ni kwa nini?
Ilikuwa wawe na Katiba itakayo linda masilahi yao. Maslahi ya wanani? Wao wachache wanaojiita WENYEWE> Yaani maamuzi ya nani awe diwani yawe mikononi mwa mtendaji wa kata. Mbunge aamuliwe na Mkurugenzi wa Wilaya ambaye anakuwa kwa ngazi hiyo ni kada wa CCM> Raisi aamuliwe na mteule wake yaani Kamishena wa NEC> Ili mfumo mzima ubakie chini yao ili kila kitu kiendeshwe kikada na Ndiyoooo, Yapiteeeeee nk nk

Yaani pamoja na ubovu wake CCM iendelee kuwepo.
Ubovu gani?
Kutokuwa na umakini wa kujiendesha kama watu wenye weredi.
Mfano uwe unataka kujenga nyumba yako kwenye kiwanja fulani unacho kimiliki. Utangaze zabuni za kujenga watu wajinadi na Mmoja ashinde zabuni. Unaingia naye mkataba kukujengea na wewe unajiendea Ulaya kuendelea na shughuli zako za siku zote. Unarudi baada ya miaka mitano, pamoja na kuwa ulilipa pesa zote za ujenzi ukute ulijengewa GOFU, utajisikiaje. Uje kuchunguza ukute waliojenga hawakuwa na ujuzi, walikuwepo ongezeko la watu hewa kujenga lakini muda wote wa miaka mitano mjengaji hakuona kuwa ni tatizo yeye kula pesa zako tu. Hata aseme atajirekebisha namna gani kama una akili timamu, hukulishwa limbwata, hauko kama nyumbu, kondoo nk utamuacha aendelee kukujengea?

Sasa huko ndiko kunaweza kuwa kimbilio la wenye kuipenda TANZANIA?
Kuna nini wanakimbilia?

Watanzania kiwanja chetu ni Tanzania. Siku zote anayeshinda zabuni kutujengea ni CCM kwa vipindi vingi vya miaka mitano mitano. Mpaka leo nyumba iliyojengwa ni gofu. Uchumguzi umetuhakikishia kuwa hawana WEREDI. Ilikuwaje wana wajenzi HEWA na kwa muda wote wasio kuwepo yaani HEWA? Ilikuwaje walipewa nafasi ya ku-recruit waka-recuit wasio na sifa yaani wengi wao ni vyeti vya kugushi na wamekuwa wakiishi nao tu. Na kwa muda wote tumekuwa tukiwaona ni wajanja wajanja wa maneno na huku wao ni debe tupu? Mtu na akili yako unaweza kuhamia kwa watu wa namna hiyo badala ya kuwakimbia?
Imenipa taabu nikaona Wana JF niwaulize.
Kuna mtu anayefikiri kuwa kuna haja ya kuendelea kuwaamini CCM kama taasisi katika mazingira hayo?
Wasomi wengi ni kama hawafikirii vile, yaani kajitokeza mtu binafsi mwenye mawazo yake yasiyo kuwa ys taasisi basi wote huko, kwa hiyo wote twende huko ili kusiwepo mkosoaji? Eti kila mtu anasema naunga mkono juhudi, ni kweli? Nadhani tunatafuta gape la unafuu ngoja wasipopata hiyo fape utaona tu watafanana na ngiri waliotimuliwa shamba la mihogo, sasa wote turudi huko tukakutane huko uone linalokuja. Tuelewane
 
Ccm ni lidude flani hivi!

Limekusanya waovu wa kila namna ya uovu.

Lina taint image ya taifa letu TANZANIA.

Chama kikongwe ambacho hakitokagi madarakani kimegeza madaraka kuwa ni mali yake.

Chama cha mapinduzi kina chembe hai za kupindua pindua lolote jema.
 
Back
Top Bottom