Ulimwengu wetu ulitokeaje?

THE SPIRIT THINKER

JF-Expert Member
Sep 9, 2019
392
555
WATAALAMU wa anga hufurahia sana kupiga dunia picha wanapoiona ikiwa kubwa kupitia dirisha la chombo cha angani. “Huo ndio mwono bora zaidi unapokuwa angani,” akasema mmoja wao. Lakini dunia yetu huonekana kuwa ndogo sana ilinganishwapo na mfumo wa jua na sayari zake. Dunia zipatazo milioni moja zinaweza kutoshea ndani ya jua, na bado nafasi ibaki! Lakini, je, mambo hayo juu ya ulimwengu yanahusu maisha yako na maana yake?

Ebu tuelekeze uangalifu wetu kifupi katika anga na kuona uhusiano uliopo kati ya dunia na jua. Jua letu ni mojawapo tu ya nyota nyingi sana zenye kutazamisha zilizo sehemu ya kundi la nyota linaloitwa Kilimia (Milky Way), ambalo nalo ni sehemu ndogo sana ya ulimwengu. Kwa macho, inawezekana kuona madoa machache ya nuru ambayo kumbe ni makundi mengineyo ya nyota, kama vile kundi kubwa la nyota lililo maridadi linaloitwa Andromeda. Kilimia, Andromeda, na makundi mengine yapatayo 20 ya
nyota, yameshikamanishwa pamoja kwa nguvu za uvutano na kufanyiza fungu la makundi ya nyota, yote hayo yakiwa sehemu ndogo tu ya mkusanyo mkubwa wa mafungu ya makundi ya nyota. Ulimwengu una mikusanyo mingi sana kama hiyo, na mambo bado.Mafungu ya makundi ya nyota hayana mpangilio wenye utaratibu angani. Yakipanuliwa, yanafanana na tando nyembamba na mapovu makubwa yaliyo matupu yenye nyuzinyuzi zinazotokezea pande zote.
Huenda hilo likashangaza wengi wanaofikiri kwamba ulimwengu ulijitokeza wenyewe tu katika mlipuko mkubwa. “Kadiri tuwezavyo kuona kwa uwazi zaidi ulimwengu ukiwa na mambo mengi matukufu,” akata kauli mwandishi mmoja mkuu wa Scientific American, “ndivyo inavyozidi kuwa vigumu kueleza kirahisi tu jinsi ulimwengu ulivyopata kuwa hivyo.”



NITAENDELEA KUELEZEA HADI MWISHO LAKINI MNARUHUSIWA KUJADILI.




UFAFANUZI WA KUNDI LA NYOTA

(Milky Way)


Inachukua kilometa kwintilioni moja kuvuka Kilimia, yaani kilometa 1,000,000,000,000,000,000! Inachukua nuru miaka 100,000 kulivuka, na kundi hili moja la nyota lina nyota zaidi ya bilioni 100
 
Ulimwngu ulitokea kama coincidence au ulitokea kwa makusudi ya something/someone intelligent.
ila kama tukisema ulimwengu ulitokea kwa makusudi ya something/someone intelligent, then maswali hayatoisha.
sababu utauliza huyo someone/something ambacho ni intelligent kimetokeaje?

na tukisema ulimwengu ulitokea kama coincidence kutokana na spontaneous nature activities.
still skeptical lakini lakini hili jibu la chini linamake sense in some percent.
 
ULIMWENGU WETU ULITOKEAJE ? UBISHI ULIOPO

SEHEMU YA PILI.


UTHIBITISHO UNAONYESHA KULIKUWAPO NA MWANZO.

Uthibitisho Unaoonyesha Kulikuwa na MwanzoNyota zote unazoweza kuona ziko katika Kilimia. Kufikia miaka ya 1920, watu walidhani kwamba hakukuwa na kundi jingine la nyota ila hilo tu.


Ingawa hivyo, labda unajua kwamba uchunguzi uliofanywa na darubini kubwa umethibitisha kwamba hiyo si kweli. Ulimwengu wetu una angalau makundi 50,000,000,000 ya nyota.


Hatumaanishi nyota bilioni 50—lakini angalau makundi bilioni 50 ya nyota, na kila kundi lina mabilioni ya nyota zinazofanana na jua letu. Lakini, si wingi huo wa makundi makubwa-makubwa ya nyota uliowashtua wanasayansi katika miaka ya 1920.

Jambo lililowashtua ni kwamba makundi hayo yote yako mwendoni.Wataalamu wa nyota waligundua jambo moja lenye kutokeza sana: Nuru inayotoka kwenye kundi la nyota ilipopitishwa kwenyekipande cha glasi kinachotawanya nuru, mawimbi ya nuru yalionekana yakiwa yamerefuka, ikionyesha kwamba makundi ya nyota yaliyo mbali na dunia yalikuwa katika mwendo wa kasi sana.


Kadiri kundi la nyota lilivyokuwa mbali zaidi, ndivyo lilivyoonekana kwenda kasi sana mbali na dunia. Hilo ladokeza kwamba ulimwengu unapanuka!Hata kama sisi si wataalamu wa nyota wala wapenzi wa mambo ya nyota, twawezakuona kwamba upanuzi wa ulimwengu unaweza kuashiria mambo mengi sana kuhusu wakati wetu uliopita—na labda wakati wetu ujao vilevile. Ni lazima kitu fulani kilianzisha upanuzi wa ulimwengu—kitu chenye uwezo sana kuliko nguvu nyingi za uvutano za ulimwengu. Mtu anakuwa na sababu nzuri ya kuuliza, ‘Ni nini kingeweza kusababisha nguvu nyingi sana hivyo?

Ingawa wanasayansi wengi husema ulimwengu ulianza ukiwa kitu kidogo sana ambacho kilifinyana sana, hatuwezi kuepuka suala hili kuu: “Ikiwa wakati fulani uliopita, Ulimwengu ulikuwa kitu kidogo sana kisichoweza kuwazika na chenye uzito usioweza kuwazika, ni lazima tuulize ni nini kilichokuwapo hapo awali na nini kilichokuwapo nje ya Ulimwengu. . . . Ni lazima tukabili suala la kuwapo kwa Chanzo fulani.”—Sir Bernard Lovell.Hili ladokeza zaidi ya kuwapo
chanzo cha nishati nyingi. Busara na akili pia zinahitajiwa kwa sababu kiwango cha upanuzi wa ulimwengu chaonekana kuwa kimepimwa barabara kabisa. “Ikiwa kiwango cha upanuzi wa Ulimwengu kingeongezeka hata kwa kiasi cha sehemu moja tu ya milioni moja mara milioni moja,” asema Lovell, “basi kufikia sasa kila kitu kilichomo Ulimwenguni kingekuwa kimetawanyika. . . . Na ikiwa kiwango hicho kingalipungua hata kwa kiasi cha sehemu moja tu ya milioni moja mara milioni moja, basi nguvu zabasi nguvu za uvutano zingalisababisha Ulimwengu uporomoke miaka ipatayo milioni elfu moja ya kwanza. Hapa tena twaona ya kwamba hakungekuwa na nyota zenye kudumu na basi hakungekuwa na uhai.”



SEHEMU YA TATU NITAONGELEA JUU YA MAJARIBIO YA MAHABARA YALIYO FANYWA ILI KUUTENGENEZA ULIMWENGU NA KUCHUNGUZA JINSI ULIVYO ANZA.


TUENDELEE KUWA PAMOJA.


(NAWAHITAJI WATAALAMU WENYE UJUZI WA ELIMU YA ANGA PIA MAANA NIPO KWENYE MRADI WA KUANDIKA KITABU CHA MASWALA YA ANGA NA TEKNOLOJIA ZAKE .HII NI KWA FAIDA YA WATU WOTE WANAO ZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI ILI WAJIFUNZE ELIMU HII KWA MIFANO YA KAWAIDA NA WAUJUE ULIMWENGU WAO )
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom