Mavella, kama ungo wako upo tayari kwenye eutelsat 16a basi jaribu kuzungusha lnb yako clockwise/anticlockwise na blindscan receiver yako.Aidha check decoder yako kama ni mpeg4 na inasapoti dvb-s2 8psk kwani freq 10804 h 30000 ni dvb-s2 8psk. Hiyo freq 11024 h 3333 uliyoipata ni dvb-s1 mpeg2.Hata hivyo ninapata mshangao kwa vile frequence hii iko mbali sana na Tanzania,nihakikishie kama huishi Tanzania.Kwenye sat eutelsat 16a ni beams mbili tu ambayo Tanzania tunaweza kupata, Eutelsat 16A South East Africa na Eutelsat 16A Saharan Africa,ukitembelea hapa flysat.com/e16a-beam.php utaelewa nn namaanisha.
haya kwa wale waliofunga KU na wanshindwa kuzipata radio zilizopo bonyeza batani hii kwenye rimoti yako TV/R utapata radio zote hakikisha chneli uliyoweka ipo upande wa ku mfano kbc.
ATN iko wazi kwa sasa kwa kupitia king'amuzi chao AAL-003,faidi kabla hawajaifunga
unaweza kupata fta chaneli nyingi kutokana na uwezo wa kuwa na satdish 2 au 3,
(1)uwe na c band satdish futi 6 au 8 pamoja na lnb 3 moja iwe c band lnb na 2 ku band,
lnb ya kwanza ambayo ni c band utapata chanel 9 ambazo ni
1.itv
2.eatv
3.capital
4.tbc
5.star tv
6.channel 10 (kwa shida)
7.mtv1
8.mtv2
9.tim
lnb ya pili ni ku ambayo utaifunga juu ya ile c band ya katikati na utapata chanelli kama,
btv, sabc 1,2 na 3, f24, nollywood plus, nollywood moves, ctl, press tv, channel 44, afrika unite tv, citezen tv, emanuel tv ziko nyingi zaidi ya 70.
Lnb ya tatu ni ku utaifunga upande wa chini na hii umapata chaneli kama kbc, k24, familly tv, sayare tv (sauti ya rehema), na wbs.
Kama utakuwa na dish dogo la ku lifunge liangalie kaskazini muelekeo wa dstv utapata chaneli kama,
lcf, golfe tv, rdv, ortb, drtv internatinal, love world, ebru tv, tpa (feed) kama una hd reciever unapata na channel ten. To be cont...
Mkuu leo nafikiri nianze na receivers/decoders.Hicho ni kifaa kinachopokea mawimbi ya matangazo kutoka kwenye satellite husika kupitia ungo.Kwa sasa receivers zote ziuzwazo duniani kote ni DIGITAL.Ndio maana zimeandikwa mbele DVB[ Digital Video Broadcasting] Zinaitwa decoders kwa sababu zikisha pokea mawimbi zina uwezo wa kukuambia zimepokea nini[picha na sauti unayopata ndio decoding ability ya receiver yako]Kwa hiyo sio kila receiver ina uwezo wa kudecode [kukuambia nini kimepokea]mawimbi yaliopokea.Kwa sababu hiyo ndio maana kuna reiceiver inanasa mawimbi ya tv channels ambazo zinapatikana bure hewani [FTA TVs] na zingine tvs za kulipia tu.
Tunaendelea.Nimesema receivers/decoders zote ni digital ok? Ndiyo, ingawa ni digital bado zina uwezo wa kupokea(to receive)mawimbi ya anologia na kutupa picha/sauti (to decode).Receivers/decoders hizo ziko za aina anuai, nazo ni; DVB-S, DVB-T na DVB-T
DVB-S : Hizi ni vile zenye uwezo wa kupokea mawimbi kwa njia ya satellite, nazo ziko za aina kuu mbili Dvb-s1(digital video broadcasting-satelite 1st generation) na Dvb-s2(..................2nd generation).Receivers/decoders nyingi tulizo nazo majumbani mwe2 ni Dvb-s1 mfano mediacom zote,gulf star,baadhi ya strong n.k. zote hizo mpeg2.Ricva hizo hazina uwezo wa kupokea mawimbi ya satellite 2nd generation(dvb-s2)
Dvb-s2 ni technology ya kisasa. Mfano wa ricva zake ni strong srt 4669,4930, humax ir1020,2000,2020, Ting aal-003, zuku decoder,dstv hd decoder n.k. Ricva/Decoders hizo zote ni mpeg4 compatible na nyingine ni HD compatible.
Tunasema receivers tulizonazo hazifai sana kwa sababu si tu kwamba tvs zinahamia digital bali nyingi zinahamia dvb-s2.Hebu tembelea FlySat Yahsat-1A @ 52.5° East utaona ninachomaanisha.Utaona kuna baadhi ya tvs unahitaji revceiver ya dvb-s2 ili uikamate.Kwa ufupi kwenye dvb-s unahitaji dish kupata mawimbi ya tvs
DVB-T: hizi ni zile zinazokamata mawimbi kwa njia ya antenna( digital video broadcasting-terrestrial) nazo ziko za aina mbili, dvb-t1 na dvb-t2.Ving'amuzi vya startimes na ting aal-001 na al-002 viko hapo.
DVB-C: hivi hukamata na kutoa matangazo kwa njia ya cable.Aina hii ya ving'amuzi c mashuhuri sana Africa hususani Tanzania. Kulingana na Jina la Thread hii mijadala yote itahusiana sana na DVB-S receivers/decoders na fta tv stations.
Mavella, uko sahihi ,nilikuwa naangalia flysat ambako tvm haionekana. kupata channels unahitaji ungo wenye ukubwa 40dBW=120CM hii ni kwa mujibu wa [flysat.com], lakini we jaribu tu na ungo wa 3ft unaweza ukashika kwani 120cm ni estimation tu. Good luck
Hongera Mavella kwa kazi nzuri unazoendelea kuzifanya humu ndani. Ni dhahili kuwa ungo wako upo kwenye sats Amos/ Eutelsat 16a na pengine hupati frequences zingine ni kwa 7bu ya size ya dish.
Leo niendelee na kifaa kingine kiitwacho satallite dish(ungo). Kabla sijaendelea na somo la leo naomba niwarudishe nyumba kidogo kwenye somo lilopita lililohusu receicers/decoders kwamba kuna baadhi ya ricva/decoders zina uwezo wa kutumika kama dvb-s, dvb-c na dvb-t. Mfano wa decoders hizo ni strong srt 4902 na sun ray 4 HD 800 se ambayo Viper anayo.
kuna aina kuu mbili za nyungo nazo ni; prime focus dishes(maarufu kama c-band dishes) na offset/parabolic dishes(maarufu kama ku-band dishes).Kwa aina ya kwanza kuna ambazo ni za bati na za wavu zenye ukubwa unaoanzia 6ft na kuendelea.Ni madishi ambayo ni ya duara.Madishi hayo ndiyo mengi sana majumbani mwetu. Kati ya bati na ya wavu, ningependa watu waelewe kuwa yabati ni bora zaidi kwani yana uwezo wa kukamata frikwensi dhaifu kuliko za wavu.Aidha zinaweza kutumika kukamata frikwensi za ku. View attachment 68884View attachment 68884View attachment 68884
Aina ya pili ni madishi, ni yale yenye umbo la yai Ambayo dstv, zuku na Ting wanayatumia.Madishi hayo yana ukubwa kati ya 2ft -6ft.Kama ilivyo kwa madishi ya aina ya kwanza watu wengi tunafikiri kwamba aina hayo ya madishi yanatumika tu kwa kupokea mawimbi ya ku pekee,si kweli bali yanaweza pia kupokea mawimbi ya c-band pia kutegemea na ukubwa wake.