Kwa urahisi ni hivi: Mpeg4= wake na mpeg2=wanawake. Ukiwa na mlinganyo huo ni sahihi kusema wake (wanawake walioolewa) wote wa watu ni wanawake ila si kweli kwamba wanawake wote ni wake za watu. Kwa mtazamo huu ndugu
josephjul40 bado kuna shughuli kubwa ya kuendelea kueleza mambo ya msingi kabla watu hawajaweza kutega nyungo. Kutegeza ungo inaweza kuwa rahisi sana (kwani watu wengi hufanya kwa mazoea) Layman anaweza kujua kuwa ALU (Artemether Lumefantrie) inatibu malaria lakini hawezi kujua ni kwa namna gani inatibu. Ndivyo ilivyo na kwa watu wanaoweza kutega nyungo kwa mwelekeo fulani. Kama kuna yeyote ambaye haamini ninachosema awe wa kwanza kujibu swali hili : NI KWA NINI UNGO WA PACKAGE YA AZAM UNAELEKEZWA MAGHARIBI WAKATI SATELAITI YAKE IPO MASHARIKI? (NI MUHIMU UNITAJIE SATELAITI HII).Fatilia kuona majibu yatakayoletwa hapa.