ni kweli kabisa
Jukwaa siku hizi limeharibika, hakuna cha kujifunza ila ni ubishi tu
mtu kapata smartphone kajiunga JF basi atataka anachookota huko barabarani akilete humu na asipingwe atabishaa mpaka saver ijae.
hata kuchangia au kuelimishana elimu tulizozipata tunashindwa maan hujui unayewboshana naye ni kichaa au gwiji aliyebobea
sasa 4D na YOGA au NDOTO na Medidation ni wapi na wapi
Sometimes huwa nikisoma post nyingine nacheka hata nikiwa peke yangu .... ebu ijaribu hiyo Meyiiiiiii uone kama ina madhara yoyote.Kila kitu kimegota na kusimama kwenye hiyo meyiiiiii meyiiiii.kw hiyo hata km utafuata hayo maelekezo mengine lkn ukakosea kwenye hiyo meyiiiii meyiiiii.hutafanya lolote.hivyo meyiii meyiiii ndio kila kitu.
Sisemi kuwa ina madhara yoyote.ila nataka nijue huyoo meyiii meyiii ni nani ktk umimwengu huuu?,!! Na ana mamlaka yapi ktk ulimwengu huu mpk jina lake litumike kufungua mlango wa jicho la tatu?!!Sometimes huwa nikisoma post nyingine nacheka hata nikiwa peke yangu .... ebu ijaribu hiyo Meyiiiiiii uone kama ina madhara yoyote.
Kwanza bro ungeyataja hayo mambo unayosema una anza kuyaona ili tuyajadili moja baada ya jingine tujue ukweli wake.Kwanza nianze kwa kumshukuru Mshana Jr amekuwa msaada mkubwa kwangu kwenye kujifunza mambo mengi. Nami sasa naona nianze sasa kuwafundisha wengine ..
ULIMWENGU WA 3D NA 4D
Unajua kila mtu anaishi katika sehemu mbili; katika ulimwengu wa 3D na katika ulimwengu wa 4D. D= Dimension. / mwonekano
Katika ulimwengu wa 3D ndio huu unaoniwezesha sasa naandika haya kwenye kompyuta na nikiangalia ninaona jua magari na tunaenda shule kusoma nk. Ni ulimwengu huu ambao umeuzoea siku zote tuna kula na kunywa. Katika ulimwengu huu tunatumia macho mawili na huku tunashangaa kwanini watu wengine wanafanya miujiza wakati sisi wengine hatuwezi? Au kwanini watu wengine wanatabiri wakati sisi hatuwezi?.
Hawa watu wanaweza wakafanya hivyo kwa sababu wanaweza wakatumia jicho la tatu ambalo mtu akiwa mtoto mdogo au mchanga huwa lipo very active. Na kadri anavyozidi kuwa mkubwa jicho hilo hufumbwa na kufanya asiweze kuona tena vitu vilivyo kwenye 4D.
Watu wanafanya mambo hayo ni kwa sababu wanauwezo wa kufumbua jicho la tatu na kuona vitu vilivyo kwenye 4D. Huo uwezo wa kufumbua hilo jicho ndio unaosababisha watu wanafanya miujiza wanatabiri na wanafanya vitu vingi ambavyo havionekani.
Kwa sababu mtu amefumba jicho hilo kwa mda mrefu huwa inamchukua mda kuwa na uwezo wa kulifumbua jicho hilo. Lakini kwa maelekezo maalumu jicho hilo linaweza likafumbuka. Jicho la tatu linakufanya uone ulimwengu mwingine tunaoishi sisi ambao ni mzuri sana. Tofauti na huu ambao umeharibiwa na watu wachache. Mantiki ya sisi kuwepo ni kuufanya ulimwengu huu ufanane na ulimwengu ulio kwenye 4D. Uoga na kuogopeshwa kumewafanya watu wasiweze kabisa kuingia katika ulimwengu huo.
Nitajaribu kueleze jinsi ya kuingia katika ulimwengu huo hatua kwa hatua na ndipo sasa utaanza kujielewa wewe mtu ni wa namna gani? Je! ni nguvu gani uliyo nayo ambayo umefungwa na watu wachache walioweka kanuni zao ili wewe upumbazike.
*Jicho la tatu ndilo linalotufanya tuone vitu kwenye ulimwengu wa 4D*
Kwa sababu ni mda mrefu sana haujawahi kulitumia jicho hilo ni vyema kuanza kufanya mazoezi jinsi ya kulitumia. Tafuta sehemu iliyotulia. ambayo hakuna kelele kelele. Au ikiwezekana jifungie chumbani na uzime taa. Hatua utakazo fanya ni unakaa vizuri mikono yako weka kwenye magoti.
Fumba macho yako haya mawili. Kaa kimya kwa mda wa dakika kama 6 - 10 hivi. Vuta hewa kwa kutumia pua na itoe kwa kutumia mdomo. Fanya hivyo taratibu taratibu. wakati mwingine ukiwa unaanza utasikia kichwa kinauma. Usihofu hiyo ni kawaida.
Anza kutoa sauti kwa taratibu ukisema MEYIIIIIIIIIIIIII, MEYIIIIIIIIIII. Bada ya mda jicho la tatu litaanza kufunguka taratibu. Kwa sababu mda mrefu hujawahi kulifumbua utaona giza giza vitu vitu usivyo vielewa. Fanya hivyo kwa mda wa wiki mbili tayari utakuwa umezoea utaanza kuwa na uwezo sana.
Utaanza kujua vitu vingi sana na kuanza kujielewa sasa wewe ni nani na una nguvu gani. Nitakueleza siri hiyo wanatumia akina nani na inaleta matokeo gani. Hakuna uchawi hapa mtu asikudanganye. Ni wewe tu jinsi ya kujielewa.
Karibu tuujifunze kwa pamoja (theory na practical)
Unapenda ku jibu nusu nusu ili uulizwe au...si ueleze kitu umalizeHata nikikueleza nimejuaje hutakubali kwa sababu hujafunguliwa ...
Binadamu ana milango 8 ya fahamu ... lakini mitatu ya mwisho (isiyofundishwa) ndo inategemewa sana katika elimu ya vitu visivyoonekana.
Macho yatakuonesha kitu fulani lakini kuna sehemu yanapeleka hizo data.
Masikio yakisikia kitu fulani yanapeleka data sehemu fulani; hivyo hivyo pua, ngozi, ulimi ... pale ambapo data hizo zinafanyiwa processing ndo panapofungua hilo jicho la tatu ambalo linafungua ile milango mitatu isiyofundishwa madarasani.
Asante Zurri kwa kuja nadhani tutajua mengi kuhusu huu UziKwanza bro ungeyataja hayo mambo unayosema una anza kuyaona ili tuyajadili moja baada ya jingine tujue ukweli wake.
Pili,nini maana ya MEYIIIII na kwanini MEYIIIII ?
Ukishajibu nitakuja kukupa faida kubwa sana juu ya mambo hayo.
Kwa ufupi huo ni USHIRIKINA na unakupelekea katika upotevu.........
Narudi bro...... Elimu sahihi ni nuru na Ujinga ni giza.
Hujajibu swali langu mkuu, ni bora utuambie maana ya maneno hayo kwanza kabla ya kuyatumia. Mimi naamini hayo maneno yana maana, siyo bure tu, na kama hayana maana basi inawezekana kabisa hilo likawa "jina" la kitu fulani au kiumbe fulani. Kama hujui maana yake basi usiwaambie watu wayatumie, inaweza kuwa hatari zaidi kuliko unavyofikiri wewe.Jaribu kwanza ..
Unajua nashangaa kwa nini usijiulize kwa nini A inaitwa hivyo na wala sio Z
Mkuu hata mimi nimemuuliza swali hilo hilo, akikujibu maana ya MEYIII naomba uni-tag.Pili,nini maana ya MEYIIIII na kwanini MEYIIIII ?
hakuna kitu kama hii Bro. hizi ni ndoto ambazo Holywood wamezipandikiza ktk vichwa vya watu.
asilimia 99 ya maneno ya watabiri wote na waganga wote NI UONGO.
Nimefanya Research miaka chungu mbovu.
Usipoteze muda wako kuzigeuza hizi fictions kuwa Reality. Hizi habari za 4 Dimension ziwache kwenye movie's tu. kinyume cha hapo utapoteza muda wako huenda ukadhurika kwa kulishwa UCHAFU na sumu na waganga wa kienyeji.
kiongozi hakuna kitu kama hii.Hujajibu swali langu mkuu, ni bora utuambie maana ya maneno hayo kwanza kabla ya kuyatumia. Mimi naamini hayo maneno yana maana, siyo bure tu, na kama hayana maana basi inawezekana kabisa hilo likawa "jina" la kitu fulani au kiumbe fulani. Kama hujui maana yake basi usiwaambie watu wayatumie, inaweza kuwa hatari zaidi kuliko unavyofikiri wewe.
Fahamu kwamba ulimwengu wa "roho" umegawanyika mara mbili, kuna "Roho njema", na roho "wachafu", hizi roho chafu ni kama sumu, na sumu haijaribiwi kwa kuionja, utakufa. Itakuwa vipi kama hayo maneno(MEYIII) ni jina la roho mchafu na huyo roho akawaingia hao watakaomuita???
mkuu naona kama aujamuelewa mtoa mada vizuri kutokana na yeye kajichanganya kidogo alivyoanza na mambo ya 3D na 4D za kisayansi zaidi lakini mwisho wa uzii ameenda kwenye point yake mambo ya kumeditate na mjicho wa tatu sijui
Dunia ina mambo mkuu kwa habari ya jicho la tatu alilo lizungumzia mtoa mada ni kweli kabisa inawezekana na ukiwa na nia ya kulifungua ilo jicho litafunguka tu na utaona madudu ya ajabu ajabu
Kama mtu anapata kuwa na jicho la jini au la mzimu haumdanganyi kwa lolote labda wale matapeli tu.Sijapungukiwa akili kiasi cha kwenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta solution ya issue zangu.
labda hufahamu maana ya Research.
nani aliwahi kukaa peke yake dakika kadhaa akaita hio research?
nakupa Homework
manake nadhani na wewe ni ktk wale wavaa hirizi kwa kujilinda na TRA.
Nenda kwa mganga yyt hali ya kuwa una mke na watoto kisha kamwambie unatafuta watoto miaka mingi sana unataka akutazamie tatizo ni nini kama atagundua wewe una watoto.!
au mpeleke asie na mke wala mtoto kisha mwambie mganga mke wa jamaa anatembea na MTU na unataka kujua ni mtu gani kama hakukutajia jirani yako au mjomba wako .
halafu fuata hizo Fictions za huyu jamaa uone km utaiona hio 4 Dimension.
Elimu ni kitu muhimu sana.
someni bandugu au mtaendelea kuibiwa mpk Siku ya kufa.
Hehehe alafu sasa hivi una third eye?Yote sawa! hata mimi nilikuwa mbishi kama wewe!
hakuna kitu kama hii.Kama mtu anapata kuwa na jicho la jini au la mzimu haumdanganyi kwa lolote labda wale matapeli tu.