Ulimwengu unaelekea wapi?

PHILE1879

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Posts
645
Reaction score
483
Katika pitapita zangu mtandaoni nikaona tangazo la muuzaji wa iPad. Nikasevu namba yake ili nimtafute nikiweka salio. Nilipocheki kwenye WhatSapp nikamkuta yupo tayari.

Tukaanza kuchati baada ya muda akaniuliza :"Are you married?" nikashtushwa na swali hilo, nikajihoji kwanini ananiuliza hivyo.Nikagundua kwenye profile picture nimeweka picha ya mke wangu.

Nikamjibu :"Yeah, Am married".Akasema:"Good to know, so is it fine if we know each other despite you being married?" jambo hili lilinishtua nikaenda sebuleni nikamwonyesha mke wangu alicheka ile mbaya.

Amenishauri niweke picha yangu ili kupunguza kero hizo nami leo asubuhi nimeondoa picha yake na kuweka yangu.Jamaa huyo sikumjibu tena, nikakaa kimya mpaka sasa, bado anahoji "Hello!"

Dah Dunia hii sasa imekuwa balaa. Ndoa zitaponyoka kweli?
 
Wake za watu wemekua wepesi kuachia upeujer kuliko walioko single ndio maana!
 
Inakuwaje unaweka picha ya mkeo au mtoto kama picha kuu kwenye mitandao yako ya kijamii??
Weka picha yako kwasababu inakuhusu wewe na sio wao.
 
Wala hauendi popote bali unarudi kinyume nyume si unakumbuka ya Sodoma na gomora?
 


Usiogope ... life is good. Na kwenye hiyo avatar yako tuwekee picha ya mkeo
 
ulimwengu unaelekea kidigital nowadays kila kitu online kuanzia kazi, mapenzi, usaliti, fursa n.k... Kavipi weka hiyo profile picture ya mkeo kwenye avatar yako ya JF uone ulimwengu wa JF utakavyo ku pm
 

Hivi kulikuwa na umuhimu gani wa kuanzisha topiki kama hii? Hivi hii topiki ina umuhimu kweli wa kuwekwa hapa JF? Kama huna topiki ya maana ni bora unyamaze kimya tu. soma michango ya wenzako.
 
Hivi kulikuwa na umuhimu gani wa kuanzisha topiki kama hii? Hivi hii topiki ina umuhimu kweli wa kuwekwa hapa JF? Kama huna topiki ya maana ni bora unyamaze kimya tu. soma michango ya wenzako.

Mmmmmmmh!
 
Mi nilikuwa nasubili Tu pale unaikuta iPad ndani na namba unagundua wife anayo bila taarifa yoyote

Wakati mwingine uache kukatisha story mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…