Pole sana Mkuu kwa Uchumi kuporomoka. Siyo kwako tu, ni janga la wengi.
Pamoja na hilo, kuwa na la kushukuru. Una afya njema, unapumua vizuri na viungo vyako vinafanya kazi vema.
Kuna wengine pamoja na kuwa Uchumi na kudorora lakini wana hali mbaya kiafya, wana msongo wa mawazo na pengine wapo katika hatihati ya kukata roho.
Kuna Mhenga aliwahi kusema, kama unakula na kuvaa, mengine hayo ni ziada tu. Shukuru Mungu kwa hayo mawili.
Pili, kama afya yako i njema amini hata kesho utapambana na Uchumi wako utatengamaa.