Ulimbukeni wa Wabongo kwenye lugha ya Kiingereza

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
583
1,478
Habari.

Raha ya kumfikishia mtu Ujumbe ni mpokea Ujumbe aelewe ulichokiandika na ulichokikusudia.

Wabongo wakijua Kiingereza basi ni mkomoeni. Tena bora wale waliosoma shule za magari ya njano kuliko hawa waliosoma shule za kata.

Unakuta mtu anajua kabisa kingereza ni lugha yetu ya pili sio lugha mama, na ni mazungumzo ya kawaida sio professional lakini mtu anajipinda kutumia misamiati migumu na lengo lao kubwa ni mpokea ujumbe atafute dictionary ili kuelewa alichoandika.

Unakuta mtu anajisifu "huyu hawezi kuelewa nilichoandika labda atumie dictionary". Mtu anaandika halafu anatafuta maneno magumu anayachomeka huko ili aonekane msomi.

Huo ni ushamba kwa nini usiandike lugha nyepesi ya kawaida ili ueleweke? Kwanza kingereza chenye maneno magumu hakivutii hata kusoma. Ila simple English ukiisoma hadi raha, unaelewa vizuri , kichwa hakiumi na hauna haja ya kila baada ya neno moja uchungulie dictionary. Na kinavutia haswa.

Tupunguze ushamba, tumia lugha nyepesi kama nia yako ni kueleweka. Haina haja ya kuhangaika kutumia maneno magumu ili uonekane msomi sana au unajua sana. Haina haja ya kutumia maneno magumu ili kukomoa watu.

Ni rahisi sana kuelewa kingereza cha wazungu kuliko cha wabongo.

Tubadilike.
 
Maadam hawavunji sheria yoyote ya nchi hii, sidhani kama kuna tatizo katika hilo.
Let's meet at the top, cheers 🥂
 
"Wi a in ze rait trak"-mungujiwe

"Put him insaidi"-Ndalichako


Yani simpo inglish, simpo endi klia, mtu unaeleweka kabisa!
 
Nenda shule , ukisoma hutaona hiyo lugha ni ngumu ila ukiwa hujui kila anaejua ngeri utaona anajimwambafai,
 
Oooh the things of talking england. Few humans is can talk england. The very much of you is cant talk england you is come here and speak that we the expertsr are mwambafying myself.

You cant us you know, can't she?
 
Back
Top Bottom