Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Wakuu salama!
Ishu hii imekuwa ikinikera sana kwani si ya kiungwana hata kidogo.
Sisi watanzania tulio wengi tunatoka kwenye familia masikini , na ndio maana tunapofika vyuo vikuu tunaomba mikopo HESLB kwa mantiki kwamba bila huo mkopo hatuwezi kujisomesha.
Jambo ambalo limekuwa likinikera kwa muda mrefu, ni ile tabia ya vijana wanapofika chuo kikuu kupenda kuishi maisha ya kuigiza sana na kujifanya kuwa ni watu ambao umasikini hawaujui bali kila mtu yuko safiiiiii. Any way hilo halikeri sana linalokera zaidi, ni pale mtu anapotafuta umaarufu na sifa za kibwege.
Nimeshuhudia kwa macho yangu mara nyingi tu hapo UDSM, mtu eti anaenda kunywa chai , kwa mfano; anajua kabisa uwezo wake ni kula chapati moja, lakini anaona akinunua chapati moja, sijui wenzake watamuona masikini au bahili, basi ananunua 2 au 3 anakula moja zingine anashika shika anaacha kwenye sahani baadae zinatupwa kwenye dust been na kisha dampo.
Kinachosikitisha na kuudhi zaidi, ni kwamba kuna watu wenye hali ngumu kimaisha ambao hutegea mabaki hayo ya vyakula yakishamwagwa dampo, wanaenda kuokota, wanafuta uchafu wanakula na chakula kingine wanapelekea familia zao nyumbani.Siku moja nilikuta mzee mmoja akimuhamasisha mwenzake kuwa waongozane wakaokote vyakula vilivyotupwa kwenye dampo la hapo UDSM; ILINIUMA SANA ILA SI KUWA NA LA KUFANYA.
Hiyo hali ya hapo UDSM, ni sample tu inayowakilisha baadhi ya wa - Tanzania, ila nimeamua kuizungumzia UDSM kwa kuwa hapo kuna "Wasomi". Najiuliza hivi mtu anashindwa nini kuchukua chakula anachoweza kumaliza, na kinachobaki/fedha inayobaki akawasaidia wenye shida kiroho safi, au hata akaitumia kwa matumizi mengine?
Msomi ni yule mwenye hekima, busara, na uelewa mpana wa mambo na akawa mfano kwa wengine. Msomi ni yule ambaye uwepo wake duniani unaleta nuru na afueni ya maisha kwa wengine. Kwa mantiki hiyo, tunawaasa wasomi wetu na watanzania kwa ujumla kuacha ulimbukeni huu unaochukiza.
Wakati unakula na kusaza, na chakula kingine kutupa jalalani; tambua kuwa kuna mwenzako anashidha na njaa, na anaenda kuokota hicho ulichokitupa jalalani na kula kwa raha mustarehe. Tuacheni ulimbukeni wa kutupa vyakula kwani ni Dhambi na jambo la kuchukiza.
Naomba kuwasilisha.