Umesema kweli shemeji. Nakumbuka marehemu babu yangu alikuwa mkali, ikitokea akaona tumetupa hata tonge moja fimbo zake sio za kawaida!!!!Nyumbani chakula hakimwagwi kamwe, nakumbuka enzi hizo watoto, ukipigwa ugali ukabaki, mtaula baadae au wakati wa kusonga ugali mwingine ule utatangulizwa kwenye maji mnaongezea unga kigogo.
Kama ni mihogo, italowekwa kwenye maji ili isiharibike na mtaimaliza tu, ole wako ukamatwe umemwaga chakula.
Na wakati niko Boarding tulikuwa na sera ya The Share Provided Must be Finished, hii mpaka leo naendelea kuitumia.
Ni dhambi kumwaga chakula na hali kuna watu wanateseka duniani anatamani ale hata wadudu wanaotambaa kukidhi haja yake.