Ulikuwa wapi wimbo huu ulipotoka?

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
342
706

Nibebe - Nyota Ndogo​

“Nibebe” from the album “Mpenzi
Nyota Ndogo featuring Nonini

Nonini
Ngoma kali hufanya niwakumbushe wakenya
Vile Swahili ni kitamu
Au sio
Nyota aa, Nyota aa
Ndogo oo, Ndogo oo

Nakupenda sana sitoficha
Kama kukupenda ni makosa
Sitaki kuwa sawa duniani
Kwani nakupenda sio siri
Wengi wakiyaona kwa macho
Machozi yatoka kila siku
Sitochoka mimi kukupenda
Watakaosema na waseme
Wengi wakiyaona kwa macho
Machozi yatoka kila siku
Sitochoka mimi kukupenda
Watakaosema na wasemee
Wameze wembe

Nibebe nami nikuonyeshe penzi
Nakukupa
Ili
Usiende

Penzi langu kwako limefika
Tabasamu langu sitokunyima
Daima nitakuwa wa furaha
Nipe tafadhali nikuonjeshe
Wee hautataka kubanduka
Penzi langu nikikuonjesha
Kama sio wewe nani tena
Hakuna kama wewe maishani
Wee hautataka kubanduka
Penzi langu nikikuonjesha
Kama sio wewe nani tena
Hakuna kama wewe maishanii
Ni wewe wangu

Nibebe nami nikuonyeshe penzi
Nakukupa
Ili
Usiende

Niliskia manzi fulani akisema jua cali ananyesha
Baada ya teso teso mi najua jo sitatesa tesa
Pia nimejaribu kuchunguza mvua gani hiyo inawaka
Nyota ndogo nikiiangalia juu hewani nairushia kamba
Niivutie hapa kwa mchanga iwe yako msichana
Ah-ah sitaki usiku ati mapenzi unionjeshe
Nipe yote tuandamane kwa balcony ndethe
Na usishtuke hata ka hapo nje tunaonekana na wasenge
Sabu vile ntafanya nikikupa penzi langu bebe
Itafanya wasee wengi wasichana, washike wasichana waanze kukatika genge
Mwili zetu wawili zipate joto vile tumeshikana
Na mi nakuambia tulia hapo ndani namwaga picana
Sa ka uliteremka huko chini unaeza jijazia kijana
Hakuna mali naenda niko na wee milele
Nimekubeba mkononi jo balcony inaongezeka kelele
Unanigwara mgongo ukisema
Kuwa waipenda (na nikimwaga maziwa)
Mvua yanyesha

Nibebe nami nikuonyeshe penzi
Nakukupa
Ili
Usiende
 
Nilikua hata sijui anaimba kwa ajili ya nini 😂😂.
Utoto wangu hamna kitu nilikua sielewi kama mapenzi, nilikalili nyimbo nyingi za mapenzi ila sikua naelewa dhima.
 
weka audio yake hapa sasa nilivyoona tu nyota ndogo ikaanza kuimba kichwani hiyo nyimbo!
 
Nilikua Mwaka wa pili TECHNICAL COLLEGE Arusha (TCA)...ulikua ukipigwa Clouds katika kipindi cha Africa Bambataa na kina DJ Too Short n.k
Daaah maisha yalikua Burudani sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom