Ulikuwa wapi siku zote...? Eh...?!

Ulikuwa wapi siku zote...? Eh...?!

Asprin

Platinum Member
Joined
Mar 8, 2008
Posts
68,271
Reaction score
96,398
Wandugu salamu,

Jana saa mbili kamili usiku, Etiennes Club kaunta ya Juu:Bia ya baridi, glasi ya moto, mhudumu mweupe.

Kijana mmoja akatokea akawakuta rafiki zake kaunta, babu nawaangalia tu na mawani yangu.
Wakagongeana mikono na kutaniana kidogo, babu nawaangalia tu bila mawani
Kisha wakapeana habari ya yaliyojiri jana yake, babu nawasikiliza tu.

Maongezi yakaendelea kupeana yaliyojiri kama walivyokubaliana jana yake. Mpaka ilipofikia sentensi ifuatayo ndipo babu akshtuka, nainukuu.... "Si nikamfanyia kama mlivyoniambia?....Nikaona tofauti bana....alipagawa flani hivi.....mwanaume nikajua bibiye nimemfikisha pafikishwapo...." Mara jamaa kabadili sura........" Baada ya gemu si ndo nikajua kumbe yule demu kauzu........ Eti akanambia mpenzi wangu ulikuwa wapi siku zote jamani? Sikujua......"

Mjadala ukaanzia hapo:
Nilikuwa wapi siku zote, ana maana gani?
Jamaa 1: (Huku Anacheka)....anasikitika kama ungemfanyia hivyo siku zote asingemegwa na wengine, angekupa wewe tu, unamegewa wewe!
Jamaa 2: Hapana bana, bibiye alikuwa anaelezea hisia zake, ulichelewesha kumpa maufundi bana
Mhusika: Mi mjanja bana....huyu anamaanisha ...yani nlikuwa mshamba flani nlikuwa wapi siku zote sikumfanyia hayo majambo, mpaka ndo namfanyia safari hii.....demu mwingi sana yule....haya mambo aliyajulia wapi mpaka anambie nlikuwa wapi siku zote?......(Sina sababu ya kuwaambia alichomfanyia bibiye, babu si mbea)

Babu kwakuwa sipendi dhambi nikajiondokea zangu....nikarudi zangu kitandani.

Sasa kaswali kwenu vijana wangu na wajukuu wangu wapendwa:

Mpenzi wako wa siku nyingi akikuonyesha ubunifu mpya katika mapenzi (kwenye sita kwa sita) ambao miaka yote hiyo hakuwahi kukufanyia....... kuna uwezekano kaupata sehemu flani ndo anakuletea? Unapaswa kumuuliza kajifunzia wapi au kumwambia ahsante?.......Je kuna sababu yoyote ya kuleta ubunifu mpya wa mapenzi kwa mpenzi/mwenza wako wa siku nyingi? Si hatari kwa mahusiano?

Jamani nawaulizeni? : MLIKUWA WAPI SIKU ZOTE............?

Babu anarudi kitandani kutafakari.
 
ha ha ha haaaaaaaaaa,babu umetulia.....inategemea na mtu na mtu,kuna watu wanapokea mabadiliko kwa shukrani na furaha,kuna wengine wanapokea na maswali mengi na kuna wengine kwa mashangao wa ajabu!!

Ubunifu ni muhimu kila wakati,la muhimu uwe na uwezo wa ku-justify ulipoutoa in case utaulizwa maswali mengi....mimi nilikuwepo na nitaendelea kuwepo na Babu...lol
 
ha ha ha haaaaaaaaaa,babu umetulia.....inategemea na mtu na mtu,kuna watu wanapokea mabadiliko kwa shukrani na furaha,kuna wengine wanapokea na maswali mengi na kuna wengine kwa mashangao wa ajabu!!

Ubunifu ni muhimu kila wakati,la muhimu uwe na uwezo wa ku-justify ulipoutoa in case utaulizwa maswali mengi....mimi nilikuwepo na nitaendelea kuwepo na Babu...lol

Hahahaha...Michelle bana.... hebu twambie...we ukifanyiwa mapya utasema ahsante au utauliza alikuwa wapi siku zote?

BTW Ulikuwa wapi siku zote Michelle wa babu?
 
Hahahaha...Michelle bana.... hebu twambie...we ukifanyiwa mapya utasema ahsante au utauliza alikuwa wapi siku zote?

BTW Ulikuwa wapi siku zote Michelle wa babu?

Nitasema asante kama nimefurahia.....nipo Babu,majukumu kidogo tu but am here,so close to you..lol
 
Tunajifunza kila kukicha. Swali na namna hilo jibu lake umelipata ndg yangu.
 
muhimu kufurahia ubunifu mengine utajiletea presha bure............... unatoa asante ya nguvu....... unamwambia kesho uje na style nyingine :bange: mambo mapya kila siku na staili mpya

 
Hahahaha...unafanya nini bafuni? Au ndo unapata maubunifu mapya?Ulichelewa wapi Afroie?
Mhhh babu unajua ukimpata anae Kukuna panapo washa utasema au uliza kituChochote.."Ulikuuwa wapi"?Sijui " nimemuona farasi" Wengine yoe tu ..Balaa umpate yule unawashwa mguu Yeye akukuna shingo utamuuliza"Umetoka wapi"? Mnnhhhhh
 
we ni babu kijana, mi nilikuwa napata majamboz na mavituz mapya kutoka kwa mjukuu wako
 
Watu wengine huuliza lakini kwa sasa huwezi kuuliza maufundi yamejaa kwenye mitandao kibao kama hapa
 
babu nimeipenda hadithi yako......unajua inatufundisha nini?? Inatufundisha kufurahia maisha kwa kuwa na mioyo mikunjufu na yenye shukrani. mapenzi babu ni matamu na katu mtu asijaribu kuyafikiria yangekuweje kama yangeongezewa chumvi au shubiri! ukianzauliza maswali ya umejifunzia wapi, nani kakujuza ni kuyatia shubiri mapenzi kwa kujitia jakamoyo! Umepewa leo mlo mtamu umepikwa kiufundi bwana lake neno AKSANTE MPENZI. Unauliza ya nini wakati uwezekano ni mkubwa kuwa wakati anafikiria kukupikia hicho chakula alikuwa ana furaha sana na akaamua akuonyeshe furaya yake na mapenzi yake kwako kwa yeye kuwa mbunifu na kujitungia tu 'Recipe' yake ambayo anaona itatoa chakula kizuri utakachokipenda?? Recipe si lazima ugawiwe na mwingine bana
 
Nyie watu wote hapo juu nawauliza hivii.......

Mlikuwa wapi siku zote?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom