sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,406
- 19,361
Binafsi nakumbuka nlikuwa na girl friend ambae tulidumu, Nlizani nimepata kumbe nimepatikana (kwa sauti ya msanii 20% 😁).
Enzi hizo nlikuwa nasoma chuo cha uhasibu pale Arusha (I.A.A) mitaa ya Njiro huko kwa matajiri wa Arusha.
Nlikuwa mtu wa watu sana, washkaji kama wote na hiki ndicho kilinisaidia, marafiki zangu wa kike wakaanza kuniambia huyu dem wako tunamuonaga mida ya jioni anachukuliwa na gari, mi nikawapuuza na kuwaona wananizushia tu wana wivu japo trust yangu kwa huyu manze ilishuka.
Basi baada ya siku 3 nilitumiwa picha kibao za huyu ex wangu akiwa kiwanja flani akimpa burudani mwenye pesa zake, hizo picha moja kwa moja ziliashiria nshaibiwa inabidi nitulie ni move on.
Sikumwambia hii ishu ila tulipokutana nlimwangalia machoni na kumwambia kwanini anani cheat, alikataa kata kata na hapa ndipo nilipojua kwamba moyo wa mtu ni msitu.
Nilipomuonyesha zile picha hizo dharau za kunijibu kwa kujiamini ziliyeyuka, hakuwa na cha kusema zaidi ya michozi kumtoka, mda huo nlikuwa na hasira sana yani nmesalitiwa na bado nikadanganywa 😠😠, kila nkimwambia kwanini umenicheat kimya, nikamfukuza atoke.
Baada ya wiki ndio akaanza kuja chuo japo alikuwa ananikwepa sana, nilimcheki usiku na kuuliza swali lile lile, kwanini ulinicheat basi ndo akanipa makavu kwamba yote aliingia tamaa ya pesa kwasababu alikuwa anadaiwa ada na nyumbani kwao pesa hawana, hata boom nililozani analo aliniambia ukweli kwamba hakuwa na boom ila aliniambia hivi ili nisimuone mzigo.
Anyway tangu hapo huyu dem ndio ikawa tabia yake na akawa mdangaji sana kadri siku zinavoenda na bado hadi sasa anaendelea kudanga, kiukweli namuombea abadilike maana ashakuwa mraibu wa haya mambo yeye ni pesa tu.
Hii kitu iliniumiza sana, anyway nilipata cha kujifunza na ku move on maisha yakaendelea nikampata mpenzi mwengine ambae watu wake wa karibu wengi nilijuana nao.
Fundisho: Jaribu uwe na urafiki na watu wa karibu au wanaoishi na mpenzi wako, hii inasaidia sana, ningekuwa sina connection za marafiki zangu hao waliokuwa wanaishi na huyo ex wangu nisingegundua kabisa haya mambo ama ningechelewa.