Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

Tumeishika hio kitambo mbna ,soon baada ya chuo nilijivua usomi wote na kuwa mtu normal tu ila sio rahisi kihivo ni msoto ila tumeihesabu
 
Sijawahi kushika 10M cash mkononi niliishia 7M tena ni mwaka 2016 ila mpaka sasa aseets na Liabilities zangu na Uwekezaji wangu katika kilimo nadhan inaweza kuwa 20M sasa sijui nipo upande gani juu ya hii mada kama niko wrong mnikosoe
 
Uzi mzuri sana, Kiukweli nimekuwa napoteza fedha zangu nyingi kwenye investment mbuzi zisizo na kichwa wala miguu.

Ila kipindi mwaka unaanza Rafiki yangu mmoja alinipa siri ya “Saving” ambapo na mimi nimeanza.

Malengo 2024 ni kumaliza na saving ya 20M.

Saving nimeanza February mpaka sasa nimefikisha 7.1 M. Kiukweli nimejiwekea nidhamu ya hali ya juu sana. Malengo ni kuhit angalau 10 M mwezi wa 6 kabla ya kuingia ngwe ya pili inayoanza July hadi december.

Katika saving soma kitabu cha the Pyschology of money na the school of money.. hutojutia kabisa kupata elimu adhimu ya saving.
 
Sijawahi kushika 10M cash mkononi niliishia 7M tena ni mwaka 2016 ila mpaka sasa aseets na Liabilities zangu na Uwekezaji wangu katika kilimo nadhan inaweza kuwa 20M sasa sijui nipo upande gani juu ya hii mada kama niko wrong mnikosoe

Mkuu hoja hapa ni cash na sio assets,
 
Aim ilikua 1 kufikisha target,mimi ni mtu dhaifu sana wakuangalia hela tu ipo mbele yangu....

hivyo naibadilisha hela navitu vyenye thamani ya pesa yangu,nilianza kwa kununua pikipiki....

nainunua leo kesho natangaza naiuza kwa bei ya juu,nikiiuza nanunua kitu kingine,kesho kutwa....

natangaza nakiuza kwa bei ya juu,mwendo ni huo huo,na kodisha frem 300k namimi naikodsha kwa 400k...

maisha yalikua namna hiyo kimasihara kama asemavyo rikiboy ten Em hii hapa na zaidi,life goes on...
Hongera mkuu! Wazo lako nimelipenda
 
Mwaka 2016 baada ya kumaliza chuo,Maisha yalikuwa magumu Sana,nilikuwa siwezi hata kupata vocha na Kula kulikuwa ni kwa manati.nikaanza kufanya kazi za saidia fundi kujenga nyumba,,KWA KWELI NILIDHARAULIKA SANA PALE MTAANI!!,niki-apply kazi siitwi hata kwenye interview,nikipeleka CV door to door,wanaishia tu kusema CV ni nzuri lakini kazi sipewi!!home hali ni Mbaya,nikimuangalia mama nasikitika sana, mana Kipindi niko shule ilikuwa inafika kipindi anauza ardhi na vitu muhimu ili nisome, lakini ajira hakuna!!Mwaka 2017 nikaweka vyeti pembeni nikaanza kuokota vyuma chakavu(screper)kwenye Madampo na Mahali popote pale nitakapo pata ilimradi tu isiwe ya kuiba,ilikuwa ni fedheha lakini nilikuwa sina namna nyingine,mwezi wa Saba nikawa nimefikisha tani1½ nikauza nikapata laki5,baada ya hapo nikanunua piglets8 wa kienyeji@30000,nikatumia kama Laki2½ hiv,2wakafa maana nilikuwa nawafuga kibabe, wakabaki6 nikawakuza hadi mwezi3,2018,nikaja kuuza kila mmoja lak1.75 nikapata million 1na elf50..nilikaa mwezi mzima nikitafakari ni biashara gani naweza kufanya..baada ya hapo niliamua kufanya biashara za kujumua mpunga mwezi 5,,nikawa naenda Mbalari na Kamsamba-ya ziwa Rukwa.nilikuwa nachukua shambani kwa Bei rahisi nakuja mjini Mbeya nakoboresha nauza. Mwezi wa 9 pesa ikawa imeshakua million 2.8.msimu wa mpunga ukawa umeisha.nikarudi home kutafakari tena nifanye nini..siku moja napitia baadhi ya timu barani ulaya na africa nikaona Kama Kuna fursa flani,.(maana wakati niko kwenye msoto,ilibidi nijifunze kubeti) ,nikasema potelea mbali wacha nirisk elf 30 leo,nikaingia parimatch wakati ule walikuwa hawakati Kodi nikaweka Odd 35.6,KWELI NIKAAMINI MWENYE NACHO HUONGEZEWA,,tiketi ika-WIN nikapata mili1.10 hiv.,wakati nafanya kazi za saidia fundi hakuna tiketi niliyo bet na ika-WIN..na hakuna pesa niliyopata kiurahisi Kama hii..baada ya hapo nikawa nafanya scalping natafuta odd ndogo nastake pesa kubwa nikakuta pesa inakuwa kiutani utani hadi najishangaa..sikumoja nikajiRISK tena nikaweka STAKE ya mill.2 kwa ODDS.3 nikapata milioni 6,sikuamini Kama ni pesa yangu,,NIKAJIULIZA MBONA KIPINDI KILE KWENYE MSOTO MAMBO HAYAKUWA HIVI,?!maana niliitumia takriban karibu miezi7 kupata Tani moja ya vyuma chakavu!!BAADAE ukafika msimu wa kilimo Nikaenda Mbeya vijijini kulima viazi mviringo nikatumia Kama milio1.8,nikavuna nikapata millioni3.4.mpaka Sasa naendelea kujishughulisha na kilimo ufugaji na NA PESA YANGU TAYARI ILISHAVUKA MILION10,naelekea 20mill.
Hongera mkuu kwa kupambana bila kukata tamaa
 
Binafsi saving kwangu haijawahi kuwa tatizo maana pia naogopa mikopo .

Nina salary ndogo tuu take home haizidi 600k but hapo nasevu half of it .

Sasa nikipata na viposho posho huwa sipingui 2.5-4 ndani ya miezi 6 na nikipata hiyo nanunua investment au nafanya mtaji somewhere.

Ndani ya mwaka naweza fikisha saving ya Kati ya 5ml hadi 6 kwa hiyo hizi naweka kweye assets mwisho wa siku nikijumlisha assets zangu zinavuka hiyo 10 mln.

Kitu cha kukwamisha ni labda nipate mgonjwa wa mda mrefu tofauti na hapo nafikisha,nimejenga kwa staili hii hii na kama nakopa ujue ni kwa friend na si vinginevyo.
big up mkuu, nayo ni njia nzuri.
 
Jiunge kikoba au Sacco's pia michezo ya Kila siku.

Nipo kwenye mchezo naweka 20,500 Kila siku sometimes nacheza majina hata 3.

Siku nikipokea hela napeleka kikoba.

Tumevunja juzi piga hesabu.

Mwaka huu mwendo ni ule ule namuomba Mungu sana ila najua inawezekana tu kwake in five years to come niwe na m 50 hivi
Hii michezo sijawahi kuiamini hata siku moja
 
Back
Top Bottom