Ulifanya nini shuleni kilichofanya kengele ya dharura ipigwe kwa ajili yako?

Jicho kote mpumbavu sana ,alizamisha meli mwehu yule,top layer nimetumia sana skull kipindi kile,nimegawa sana msosi shuleni na nimekula sana nyama ndoo nzima na washikaji zangu ,life la bording school la kipindi cha miaka ya 2005 kushuka chini lilikuwa la kibabe sana .

Kwanza wanafunzi walikuwa watu wazima kabisa ,miaka ya 2000 hata waalimu kuchapa mwanafunzi wa form 3 au 4 ni mtihani ,mana jamaa ni jeba hasa ,na anaweza kukufanyia timbwili mda wowote.

Shuleni kwetu head boy tu alikuwa na sifa zote za mwalimu
😂😂😂😂😂dah umenikumbusha mbali sana asee,miaka hiyo,niko school fulani hivi,nadhani nlikuwa form two kama sio three,basi bhana wale form four asee walikuwa wakubwa,walikuwa wanabeba nondo mabwenini,kupiga push-up ndo zilikuwa battle zao,ukiona huo ugali mtu anaokula dah unasema nsipokosa chakula leo basi😂😂😂😂. Kipindi hicho mambo ya mieleka haya yalikuwa yanatamba sana basi wakawa wamepeana hayo majiana yaan dah. Sasa kati yao palikuwa na mwamba mmoja ni mjerumani,waza ile miili ya kijerumani halafu kapanda hewani balaa halafu awe anapiga chuma,yule mwana alikuwa balaa na nusu plus alikuwa kiongozi. Siku hiyo bhana kengere ya chai imegongwa,ticha wa zamu akawahi jikoni,madogo tukawa tunapigania mikate pale ikawa vurugu ticha kapambana sana watu tukaatulia kidogo ndo viongozi wanafika pamoja na huyo mjerumani,basi akaja kule kwenye mikate akawa anawaongoza watu kuchukua mikate,ticha akachukia akamfata akawa anamgombeza,nyie mlikuwa wapi mimi nahangaika mwenyewe hapa? Akawa anampiga na fimbo kidogokidogo mkononi,jamaa akawa anampotezea basi ticha akakasirika akaruka juu ili amfikie ampige kofi😂😂😂😂,bhana weee,ile alivyotua chini mwamba akatupa konde,ticha kainama ile kuinuka kakutana na nyingine inakuja😂😂😂😂,ticha akaona hapa ntakufa hapa akakimbilia mashambani😂😂😂😂
 
Nilimwambia montress nitamroga yeye na mwalimu wa darasa vichwa vyao viwe vikubwa kama milima baada ya kuandikwa jina na kuadhibiwa kwa kupiga kelele darasani, montress akakimbia staffroom kupeleka taarifa. Uchawi kwetu haupo wala nini niliropoka tu ila tatizo ni kwamba nilikuwa nasoma nchi ya jirani tena eneo ambalo wanaamini watanzania wana uchawi mkali sana. Sikuchapwa hapo parade walitangaza tu nilichofanya nikaambiwa nilete mzazi kesho.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
🤣
 
Ambao hamjasoma Boarding hamuwezi kujua.

Mimi na crew yangu tulikuwa VIP shuleni. Ugali na maharage ya mchuzi hatukuwahi kuwa waumini wake. Sisi tulikuwa tunakula ugali na maharage yaliyokolea mafuta. Wezi wa mafuta hayo.

Sasa wakishapika maharage na kukaribia kuiva, wanaweka mafuta na yenyewe yaivie humo. Yale mafuta yanaelea kwa juu, matamu balaa ukila na ugali. Sasa sisi tusioridhika na chuzi la maji, tukishajua yameiva tunatimba jikoni kufanya yetu, mpishi akishatoka kwenda kujiandaa kwa ajili ya kuja kugawa chakula cha jioni.

Ikawa michezo ya muda mrefu kwa mafanikio. Za mwizi arobaini, zamu yangu kutimia.

Watu tunagawana majukumu. Kulikuwa na 'jicho kote', huyu alikuwa na kazi moja ya kuangaza na kutoa signal kama kuna hatari yeyote. Huyu kazi kuwaangalia walimu, wapishi na wanoko (viranja).

Yupo 'kinga', ambaye yeye anakuwa na Bakuli kubwa ndani ya ndoo. Kazi yake kupokea bakuli lenye wese na kupakia kwenye hilo bakuli ndani ya ndoo.

Kuna mtu wa mwisho, 'Master'. Huyu ni mchotaji. Anapaswa kuhakikisha kuwa anaondoka na layer ya juu ya mafuta pasipo chembe za mchuzi. Hii ni hatari maana mafuta yanakuwa ya moto balaa na unapaswa kuwa sharp.

Majukumu ni ya kupokezana. Na mimi siku hiyo nilikuwa na majukumu yangu kama Master.

Jicho kote ni sijui alizembea wapi yule mpumbavu. Alishangaa na hakumuona Mpishi anapokuja.

Nashangaa tu nimefikisha mkono usawa wa dirisha, nasikia vishindo nimepewa fimbo nzito ya mgongo. Ule ughafla, nikajimwagia mafuta na bahati mbaya yakamrukia na mpishi kichwani.

Sikusikia maumivu, nikatimka mbio. Maumivu naenda kusikia baada ya kufika kwenye chocho ya kupasulia kuni. Mpishi akapiga kelele. Wanafunzi wakajaa na walimu wakafika. Kengele ikagongwa, wote parade.

Sikwenda na wakaagizwa maskauti wanifate. Nilikuwa mbabe, hawakuthubutu kunigusa.

Wakanishauri tu, nikajiendea mwenyewe. Nililambwa viboko balaa na wenzangu. Hawakujali hata nalia maumivu.

Kesho yake tukarudishwa nyumbani miezi mitatu. Aibu. Unarudi nyumbani kwa wizi wa wese na umeungua. Tumbo baya sana.

Niliacha utukutu. Kurudi shule adhabu ikawa mpaka tunamaliza tulikuwa wa mwisho kula. Muda mwingine tunapata kingi, siku tunakosa kabisa. Haturuhusiwi kuonekana maeneo ya jikoni.
Adhabu hauruhusiwi kuonekana maeneo ya jikoni😂
 
Kipindi nipo form 5 shule x, nilitoka nje ya shule na kwenda kulala na binti mmoja.

Dah! Si akadaka ujauzito bwana!!! Siku ya siku nikaona kaja shule na wazazi wake.

kengere ikagongwa nikaona kaja na wazazi wake pale assembly ground.

Ukawekwa ulinzi wa kutosha pale kuhakikisha hachomoki mtu.

Ikapigwa roll call kuhakikisha wanafunzi wote tupo.

Baada ya hapo yule binti akaambiwa apite kila mstari kuanza kumtafuta mtu wake face to face.

Nilijaribu ku "deform" sura nisigundulike lakini wapi, wakanidaka bwana shule ikawa basi, nikatimuliwa.

About what happened next, is a story for other day.

Wewe ulifanya mkasa gani?
Kipindi kile tuna bana mitaroni kuvizia wanafunzi watoke mstarini ilitufanya KUPELEKEA mpk tukaanza kutoroka kwa kupitia dirishani mwisho wa siku mkuu wa shule alitunasa mchana tunapita dirishani kusepa manyumbani hivo ilimlazimu kwenda kugonga kengele kabla ya mda wa kwenda nyumbani😂😂😂😂😂nakumbuka nabaki kuona kama fala
 
Demu wa second master alikua ananipenda nikiwa form 4 nakarbia paper, wakati huo nilikua kiongozi wa mazingira so nilikabidhiwa ofisi ya vifaa vya usafi kukiwa na magodoro ndani yake, nikawa namnyandua yule demu kule ndani ya store wakati wa night prepo, So second master akasikia ila hakuweza kunishika ikabidi ahamishie mashambulizi angle nyingne.... Jamaa akavamia bweni letu tukiwa class akasearch akapata simu yangu..... baada ya muda nikaitwa ofisini nikaambiwa nibebe vitu vyangu, kengele ikagongwa nikaambiwa niende home
 
Hii slogan iko shule moja hivi mjini b'mlo,,"YOU CAN NOT CHANGE KAGANGO,BUT KAGANGO WILL CHANGE YOU",,.Wazee wa kuwamwagia vinyesi walimu daah
Watakua wali copy na ku paste hapo kwenye hio shule unayo izungumzia wewe.....

Shule tulikua wanafunzi kama 1500 wote boys.....

Uzur wa Kule shule usijulikane Wala kugombea uongozi wowote......

Ukiitwa na mwalimu wewe unawai kumpa mgongo na kujifunika uso Kwa tshirts, sweta au shati la shule then sepa zako nani atakujua.....

WALIMU wakorofi walikoma kuwahimiza wanafunzi kwenda prepo jichanganye taa zinazimwa na kurusha mawe juu ya bati....

Mtoto wa mama hukai pale hata Kwa wiki Moja maana chakula tulicho kula wakipewa nguruwe wanagoma kula pale ni zaidi ya JKT na tulifaulu vizuri kabisa....

Kuna room captain mmoja Sasa ivi ni MWANDAMIZI jeshini akawa na bifu na Mimi aisee yule jamaa nimoja ya viumbe wa AJABU AJABU hapa Dunia.......
 
Sikuwahi ila tu mara zote nikiadhibiwa shuleni nilikua na adhabu za peke yangu tena na Mkuu wa shule ananinyoosha uko Ofisini nikirudi class kama hakuna kilichotokea.
Sichapwi Adharani sifanyi adhabu zaidi ya Viboko na sichapwi na kila Mwalimu.
Kesi zikizidi najipa likizo nikisamehewa ndo naenda kuanza Upya Maisha.

"Nilikua nahubiriwa kimafumbo Pared kimsingi nilikua natunziwa heshima sana hata nikikosea sitajwi jina ntaitwa tu Ofisini na yataishia huko"

Ahsanteni Walimu Wangu.
Sema ukweli kuwa ulikuwa kijeba au vile vibabu vya shule

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mimi sikupigiwa kengele ila niliingia kwenye msala uliopelekea kutengwa na wanafunzi wenzangu na walimu .

Tulikuwa tunalipa ada nzuri shuleni kwenye hizi shule za KKKT ila vyakula ni vya ajabu .


Kwakuwa nilikuwa na cheo shuleni na pia ushawishi nikaongea na jamaa mmoja alikuwa kiongozi pia , siku akitoka nje atype karatasi zenye kuonesha uchungu wa ada tunayolipa na vyakula na mazingira tunayoishi kuwa haviendani ili akileta hizo karatasi tuzitapanye shule nzima usiku ili ujumbe ukifika kwa walimu na viongozi wa shule waweze kuboresha huduma ikiwemo chakula , mabweni na pia vitabu vya kutosha shuleni .

Kweli kila kitu kilienda vizuri , baada ya mimi kuzipata karatasi na kuzisambaza kila sehemu , asubuhi ikawa tafrani , walimu wakaingia kazini na maspies wa shule kumdaka mwanaharakati ila wakafeli .

Mwisho jamaa yangu akauza ramani ya vita kwa maticha sijui alipewa nini ? Tukawa tunaitwa mimi na yeye ofisi za wakubwa wa shule tunahojiwa ila nikajagundua yeye kuitwa na mimi ni bortion , targeted person ni mimi , ikaniuma sana japo bado niligoma kushiriko hiyo movement

Ndiyo hapo ofisini na kwa wanafunzi zikapigwa sumu kali , rasmi nikawa mpweke kila mtu ananiona mimi naweza kusababisha afukuzwe shule hivyo niliishi maisha ya upweke sana , nilikonda ila atleast huduma ziliboreshwa kwa kiasi chake .

Itoshe kusema nilisimama mwenyewe kuwatetea mazezeta kupata huduma bora kulingana na hela wanazolipa .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mimi sikupigiwa kengele ila niliingia kwenye msala uliopelekea kutengwa na wanafunzi wenzangu na walimu .

Tulikuwa tunalipa ada nzuri shuleni kwenye hizi shule za KKKT ila vyakula ni vya ajabu .


Kwakuwa nilikuwa na cheo shuleni na pia ushawishi nikaongea na jamaa mmoja alikuwa kiongozi pia , siku akitoka nje atype karatasi zenye kuonesha uchungu wa ada tunayolipa na vyakula na mazingira tunayoishi kuwa haviendani ili akileta hizo karatasi tuzitapanye shule nzima usiku ili ujumbe ukifika kwa walimu na viongozi wa shule waweze kuboresha huduma ikiwemo chakula , mabweni na pia vitabu vya kutosha shuleni .

Kweli kila kitu kilienda vizuri , baada ya mimi kuzipata karatasi na kuzisambaza kila sehemu , asubuhi ikawa tafrani , walimu wakaingia kazini na maspies wa shule kumdaka mwanaharakati ila wakafeli .

Mwisho jamaa yangu akauza ramani ya vita kwa maticha sijui alipewa nini ? Tukawa tunaitwa mimi na yeye ofisi za wakubwa wa shule tunahojiwa ila nikajagundua yeye kuitwa na mimi ni bortion , targeted person ni mimi , ikaniuma sana japo bado niligoma kushiriko hiyo movement

Ndiyo hapo ofisini na kwa wanafunzi zikapigwa sumu kali , rasmi nikawa mpweke kila mtu ananiona mimi naweza kusababisha afukuzwe shule hivyo niliishi maisha ya upweke sana , nilikonda ila atleast huduma ziliboreshwa kwa kiasi chake .

Itoshe kusema nilisimama mwenyewe kuwatetea mazezeta kupata huduma bora kulingana na hela wanazolipa .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
We jeshi sana Hongera Mkuu utafika mbali una Roho safi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom