Ulifanya nini au unafanya nini kupambana na kutokuwa na kazi au ajira ili maisha yaendelee?

Huu uzi wako ndio umenifanya nifungue account Jf.

Mara baada ya kumaliza kidato cha nne na changamoto kuwa nyingi sana bila kuwa na kazi yoyote nilianza rasmi vibarua vya ujenzi, kulima pamoja na kazi yoyote Ile ambayo ingepatikana mitaani, nilifanya hivyo nikiwa na lengo la kwenda kusoma ufundi wa umeme wa majumba. Nilifanya hizo kazi kwa muda wa miaka 2 mpaka nilipopata kiasi cha kwenda Kuanzia masomo ya ufundi. Nilisoma kwa miaka 3 huku nikifanya vibarua mbali mbali,baada ya kumaliza chuo na kupata cheti cha vc2 nikarudi mtaani lakini hali ilikua ngumu kazi hazipatikani kabisa basi nikatoka huko kwetu songea nikaelekea Arusha. Nikiwa Arusha nikapata kazi kiwanda cha A to Z department ya starlinger nilikomaa kwa mwaka mmoja lakini mambo yalikuwa magumu na usalama ulikua haulidhishi. Nikaacha kazi A to Z nikaingia kwenye kampuni ya ulinzi Gardaworld nimetulia kidogo hapa huku nikifanya kazi za ufundi zinapopatikana. All in all Mungu yupo
Nipo circular knitting ,ila mawe ni kidogo sana apo atoz
 
Doh! Mkuu hii simulizi yako inagusa sana.
 
Ujobless ni mbaya sana asikuambie mtu, tena ukiwa huna hata cha kufanya.

Nipo mtaani napiga kijiwe(kazi isiyo rasmi), nachuma 33% ya mshahara ambao nitapata kabla ya makato endapo nikiajiriwa na serikali kwa mwezi.

Muda wa kazi ni masaa 15 kila siku.

NB: Yatima hadeki

Prof. Janabi nilikuwa napitia kumbukumbu, watu tunatoka mbali sana.

Unayakumbuka haya mapito yako?
 
Miaka hiyo nilipanga kwenye nyumba ambayo kila mpangaji ana mishe mishe ya kufanya, kwa hiyo watu wanaamka asubuhi sana kujiandaa kutoka.

Mimi muda huo sina hata usingizi, natamani hata ningepata inshu ya kunifanya nitoke asubuhi na kurudi jioni.

Kitu kilichokuja kunipa nguvu niligundua kwa namna nilivyokuwa najiweka, japo ni jobless najitahidi kuvaa vizuri, msafi na ninanukia angalau vispray vya elfu nne, wapangaji wote au wake wa wapangaji walikuwa wananichukulia mimi kama mtu fulani wa matawi sana. Na walifika mbali wakadhani labda kuna shughuli zangu binafsi ambazo nafanya hazinibani, kumbe hamna lolote.

Kuna siku niko ndani bila ya watu kujua, nikasikia wanawake kwenye stori zao kuna mmoja anawaambia wenzie kwamba amegundua mimi ni Usalama wa Taifa na ushahidi anao, nilicheka sana.

Basi na mimi nikaona nisiwakatishe tamaa, kila ikifika asubuhi sana na mimi najiandaa natoka kama naenda kazini, kumbe naenda kuzunguka kwenye maofisi kutafuta kazi. Nikiona njaa tu imezidi nawahi kurudi nisijenikaangukia njiani, bora nikaangukie kwangu.
 
Mkuu hapa umefanya nimecheka 🤣🤣👉Nikiona njaa tu imezidi nawahi kurudi nisijenikaangukia njiani, bora nikaangukie kwangu.
 
Mkuu hapa umefanya nimecheka Nikiona njaa tu imezidi nawahi kurudi nisijenikaangukia njiani, bora nikaangukie kwangu.

Hahahahaha! Ndugu kuna stori mtu akisimulia anaweza kuonekana anaigiza. Kipindi cha nyuma ilikuwa nikisikia mtu amekufa kwa njaa namuona ni mzembe sana. Lakini kuna maisha niliyapita hapo nyuma yakaniondoa hili wenge.

Yaani mtu unapigwa na njaa mpaka unasikia kizunguzungu, halafu ukisikia na honi za magari au wapiga debe kwenye daladala unatamani uwatukane.

Haya maisha haya, basi tu.

Ndio maana japo kwa sasa siko kwenye kutafuta ajira imenibidi nisikauke kwenye haya majukwaa ya ajira kuhakikiksha tunapeana faraja kwa sababu najua kuna ambao muda huu wanapita nilikopita na wanamateso ambayo hawajui yataisha lini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom