Ule ubinadamu wa kusaidiana umepotelea wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ule ubinadamu wa kusaidiana umepotelea wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dina, Apr 3, 2012.

 1. D

  Dina JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Jana majira ya alasiri, maeneo ya darajani (kabla ya taa za Chang'ombe), kibaka aliniibia 'side mirror' ya upande wa kulia. Wakati nahangaika na mshangao wangu, akahamia ya kushoto ili nayo aichukue. Nilijitutumua kwa kuendesha gari mbele, nyuma, kushoto kulia (maana tulikuwa kwenye foleni), ili angalau niweze kumvuruga kibaka yule asifanikiwe. Kwa bahati nilifanikiwa na hakuweza kuichukua na nikaweza kuondoka baada ya magari kuruhusiwa.

  Tatizo moja nililoliona, jamani, hata watu kunisaidia? Wenye magari yao wamejifungia na vioo, kimya! Kulikuwa na gari moja ya wazi iliyokuwa imebeba watu nyuma, na wao wananikodolea macho tu na kibaka wangu. Anyways, sing'ang'anizi kusaidiwa, ila nilibaki najiuliza ule moyo wa kusaidiana uliyeyukia wapi? Na ingekuwa mshirika ana kisu pia ningeangaliwa tu?
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Dina Pole!

  Pili You r tough and strong Woman ... Honestly I love that!! Hongera!! .... Am back soon to give my deep concerns kuhusu hili swala ...!!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  aisee pole sana
  ungejaribu kupiga kelele basi.....
  ukinyamaza kimya watu nao wanakuwa wanapigwa na butwaa

  angalau wasikie mwizi mwizi.....
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Kwa vile umefunguka acha tujifungue kikweli

  Hili ni tatizo na i need 2be sincere,jamani wanachuo ondoeni ubinafsi,unyinyi,pompous,arrogance na mambo yote yanayowafanya msitake kuwa karibu na jamii

  Nyinyi mnasoma kwa ajiri ya jamii nzima kwa maana walemavu,viwete,wafupi,weusi,wagonga zege,wasio na kazi n.k,hawa ni watu wanaowategemea popote pale na kwa kweli ilitakiwa muwe front katika kuwasiliana na watu hawa popote pale iwe hapo chuoni,mtaani ama ndani ya usafiri

  Cha ajabu mnaendekeza unyinyi na kuongea lugha za ajabu ajabu,mie na hata wengine wengi humu Jf tulisoma na tulipita hapo mlipo lakini tulijaribu kuwa social,kuongea na watu na kuintermingle na watu hakutawaondolea usomi wenu

  Huku mitaani tunawaona na usiombe ukakutana nao hawakujuhi,wanapretend sana,wanajibaraguza sana hata ukimsihi msaada mpaka aamue kukusaidia utajuta,jamani,wasomi wetu tunawasihi badilikeni
   
 5. D

  Dina JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  I tried, na asante. Ila kwa siku niliyotamani gobole, ni pamoja na jana.
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  mkuu....hii imekujaje kujaje.......?
  Dina ameongelea kuhusu wanachuo.....?
  BTW...pole sana Dina.....ungepiga kelele za mwizi nadhani ungepata msaada......
  japo inasikitisha kwa hatua Watanzania tulipofikia kwa sasa......uungwana unazidi kutoweka.......

   
 7. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kweli nashindwa kuunganisha huyu bwana anataka tupate ujumbe gani!!?
   
 8. D

  Dina JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kidogo umeniacha, naona kama sijakupata. Uanachuo wa wapi tena, manake mpaka nakaribia kusahau kama nilipita chuo!
  Au labda na wewe 'uligoma' kunisaidia kwa kunifananisha na mwanachuo mwenye 'lugha ya ajabu ajabu'?
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  Heeeee wanachuo??????????????


   
 10. D

  Dina JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu wee, nilipiga ili nahisi zilikuwa zinaishia kooni, manake sina uhakika hata kama mwenyewe nilikuwa nazisikia!
  Asante sana.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  siku hizi wizi huu umeshamiri. Hususan kuwaibia kina dada, sijui mtembee na spray za kuwasha zile?

  Kingine mtu anahofia usalama wa mali yake na usalama wake pia, na hatuaminiani siku hizi, unamsaidia mtu kumbe anakudhuru.

  Pole na hongera kwa kuwa imara.

  Nilisikia kuna vitude vipo kama spry ila vyenyewe vinatoa kitu kama shoti ukimnonyezea mtu, kama vifaa hivi vipo kweli vitawafaa wanawake, maana kudrivekwa mwanamke siku hizi ni risk....
   
Loading...