Ule mtaji wa kura 11,000 za CUF uko wapi Igunga?

Jidundufila

Member
Nov 2, 2010
86
11
Nakumbuka wakati kampeni zinaaoza CUF walisema wameanza na mtaji wa kura 11 elfu je umeyeyukia wapi?
 
Kwamujibu wa matoeo ya awali jimboni Igunga, inaonekana dhahiri shahiri kua CUF sio washindani. Sasa najiuliza ule mtaji waliokua wanajivunia hadi kufikia hatua ya kuwaomba CDM wajitoe umekwenda wapi?
 
Katika historia ya dunia hii ulishasikia wapi chama cha siasa kufunga ndoa na kuolewa kama cuf, si shangai igunga kuona chausta wanawazidi.
 
tusubiri matokeo kamili ndipo tujue hizo 11000 wanaendelea kumiliki au wameongeza au wamepoteza na kama wamepoteza lazima wajiulize kwa nini zimepotea na zimekwenda wapi
 
hahaaaa cuf bwana si ndo mgombea wao kuzipiga kavu kavu na wanakijiji siku ya mwisho ya kampeni?
 
Waungwana wa hapa JF CUF walikuwa wanajitapa sana kuwa walikuwa na mtaji wa kura elfu kumi kabla ya uchaguzi na huko ndio nyumbani kwa CUF pia wakataka CDM wajitoe kwa kuwa hawakuwa na mtaji wa kura huko. Je matokeo yao vipi! mtaji umebaki au umeyeyuka kama barafu nyumbani kwa CUF ilipozaliwa
 
Wapendwa, kila uamuzi wa kushiriki uchaguzi wowote ni uamuzi bora kwa chama cha siasa makini. Kila uchaguzi una mafunzo makuu kwa wahusika. Washindi na wale walioshindwa huwa wana somo fulani huwa wanalipata. Kusema ukweli hupatikana mafunzo muhimu ambayo huwa mtaji kwa chaguzi zinazofuata.
Kwa utangulizi huu, nawapongeza wote walioshiriki katika uchaguzi wa Igunga. Naamini walioshindwa wanapata mafunzo makuu zaidi kuliko walioshindwa. Kwangu mimi nimefarijika sana kwa Wanaigunga kusema siasa za udini hazina nafasi, japo sijui kama walioanzisha dhambi hii wameadhibiwa ipasavyo! Yeyote yule, awe CCM au CUF, aliyeko nyuma ya dhambi hii alistahili adhabu kali. Najua hakuna chama chenye sera rasmi ya udini, ila baadhi ya wanachama wachovu wantafuta njia ya kutokea. Ni juu ya chama kujichunguza na kujua ni mwanachama yupi kati yao anayo mawazo hatari ya udini. Chama kikiisha baini ni nani kinatakiwa kumtenga na kutangaza hadharani. Kikishindwa kufanya hivyo, unapashwa kuwapo mfumo rasmi wa kisheria wa kukichukulia hatua kali.

Ni waulize nyote, tunao mfumo wa aina hiyo katika mfumo wetu?
 
Waungwana wa hapa JF CUF walikuwa wanajitapa sana kuwa walikuwa na mtaji wa kura elfu kumi kabla ya uchaguzi na huko ndio nyumbani kwa CUF pia wakataka CDM wajitoe kwa kuwa hawakuwa na mtaji wa kura huko. Je matokeo yao vipi! mtaji umebaki au umeyeyuka kama barafu nyumbani kwa CUF ilipozaliwa


Mkuu
kwa haraka unaweza kuona kwamba CUF wamashindwa uchaguzi lakini ukweli unaweza kuwa tofauti
kushereheke CUF kupata kura kama hizo kwenye jimbo walilozoa kura kibao miezi 12 tu iliyopita ni sawa na kujidanganya
kwa tafakari yangu sio rahisi kwa chama kama CUF kupata kura 0 (SIFURI) kwenye kituo,
wasiwasi wangu ni kwamba magamba wamechukuwa kura za KAFU kwa makubaliano ili washinde jimbo, CHADEMA wamelinda kura zao vizuri lakini kuna walakini kwamba hawa KAFU wamhujumu uchaguzi yawezekana kwa kuwambia wananchama wao kwa siri wakipigie chama cha magamba.
lakini pia BAKWATA waliwaweka wazee (babu na bibi zetu) wa IGUNGA katika wakati mgumu sana.
kwa mtanzamo wangu CHADEMA wameshinda uchaguzi kutoka kwa wananchi ila conspiracy theory imetupika magamba kutwaa jimbo
 
ccm wamewaingiza chaka nahisi waliwadanganya kwa kuwahonga chopper hahaaaaa tehe
 
Cuf huku bara hawana chao wabakie hukohuko kwao na ndoa yao na magamba,hatutaki watu wanafiki bakini zanzibar na mume wenu ccm.
 
mtaji umehamia ccm, hii inaonyesha kuwa Tanganyika tuna chama kimoja tu cha upinzani, na zanzibar hakuna chama cha upinzani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom