Ulaya pamenishinda narudi bongo

Ulaya pamenishinda narudi bongo

Status
Not open for further replies.

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
1,413
Reaction score
5,150
Mim mwehu ndama kijana wa kitanzania niliwah kuandika uzi kuomba msaada kuhusu jinsi yakupata visa yakuingia nchini Sweden, na nashukuru Kwa maoni ya baadhi ya wadau nilifanikiwa kufuata ushauri nakufanikiwa kutia maguu ndani ya bara la uropa.

Lakini tangu nilipotoka bongo nakufika hapa ughaibuni huku kichwani nikiwa na lengo la kujilipua nakubaki huku moja Kwa moja maisha yamekua tofauti na nilivyo fikiria..
Ukizingatia mwenyeji wangu nayeye anaishi hapa kiujanja ujanja.

Niliomba visa ya wiki 3 na bahati nzuri baada yakufika hapa na nlipokaribia KUMALIZA muda wangu waliniongeza miezi mingine 3.

Lakini sasa sioni kinachobadilika katika maisha yangu zaidi yakupata huduma nzuri ya chakula nakuvuta hewa Safi hapa Uppsala .

Kiukweli maisha ya hapa yanazidi kuwa magumu Kwa upande wangu sababu nimejaribu kuanzisha mahusiano na mabinti, wanawake watu wazima Hadi vikongwe ili kusudi atakae jaa nioe ili niweze kupata makaratasi lakini nawao wamekuwa wagumu.

Sitaki kujivika status za kikimbizi maana nahisi ntaaribu kabisa mpangilio wote wa maisha yangu nakuitendea ubaya elimu yangu niliyoipata Kwa shida bongo land.

Nimekua mzururaji na cha ajabu hata zile KAZI za kubeba box nilizokua nazisikia zikisemwa Sana na wadau humu jf sizipati.

Kwa kifupi uchumi wangu umedidimia mara 100 zaidi ya hata nilivyokua bongo , mpaka najuta Kwa nini nilitumia pesa yangu nlioichanga Kwa shida kama nauli yakuja huku uzunguni pasipo na manufaa ya kiuchumi kwangu.

Hapa navyoongea nimeshawasilisha ombi la msaada wa nauli ya kurudi nyumbani katika kanisa naloSali hapa Uppsala.

Kwa kifupi narudi nyumbani na nikifika hapo Kwa mkuu jiwe naenda moja Kwa moja kijijini kwetu namanditi songea kulima.

Bye bye wabongo mliopo Sweden mim maisha yamenishinda narudi nyumbani.

IMG_20200316_102053.jpeg
IMG_20200316_111755.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • VID-20200312-WA0006.mp4
    3.4 MB
Europe siku hizi hakuna ishu... Wakimbizi wa kiarabu wamejaa tele.. hakuna kazi yeyote. Canada, Australia, New Zealand, USA ndio place to be at least Kuna kazi za kusafisha na kuosha na box kwa ujumla ila ulaya labda UK kwa sababu wamejitoa kwenye umoja wa ulaya hivyo wamecut influx ya unqualified people na job zimespike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mwehu ndama unawakilisha vijana wa sasa wa Tz. Miezi mitatu unataka uwe iumetimiza ndoto zako zote. Ndio nyinyi mkiajiriwa unataka miezi mitatu ununue gari,ujenge,uoe,uwe na bilioni benki matokeo yake mnakuwa wezi mnaishia jela.

Maisha sio rahisi kama unavyotaka iwe.
Mkuu hawa ndiyo wale kizazi kilichoathirika na sera za BIG RESULTS NOW... kazi kidogo matokeo makubwa ghafla...literally...

Everyday is Saturday...................... 😎
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom