Ulaya, marekani waingilia kati Zanzibar

Ulaya, marekani waingilia kati Zanzibar

Shebbydo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
1,176
Reaction score
1,939
Ulaya, Marekani waingilia kati Z’bar
Mabalozi wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya (EU) wameeleza kusikitishwa na kitendo cha Tume ya

Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha
Dar es Salaam. Mabalozi wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya (EU) wameeleza kusikitishwa na kitendo cha Tume ya Uchaguzi (ZEC) wakati mazungumzo ya kutatua mgogoro yakiendelea na kumtaka Rais John Magufuli kutumia nafasi yake ya uongozi kutatua mtanziko wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Taarifa ya pamoja iliyotumwa kwa vyombo vya habari na mabalozi hao jana, pia inamtaka Rais Magufuli kuendeleza wito wake wa kuzitaka pande zote zitafute suluhu kwa amani.

Tamko hilo limetolewa siku saba baada ya mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha kutangaza kuwa uchaguzi wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani utarudiwa Jumapili ya Machi 20, lakini siku tano baadaye CUF ilitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.

Kutokana na sakata hilo, mabalozi hao wamelaani kitendo hicho wakisema kurudia uchaguzi kwa kigezo kuwa utaratibu ulikiuka, kinawatia wasiwasi kwa kuwa tume hiyo haikutoa ushahidi wa ukiukwaji huo.

Mabalozi hao wamesema katika tamko lao kuwa ZEC imerudia kauli yake ya kuwa uchaguzi ulikiuka taratibu licha ya waangalizi kutoka EU, Jumuiya za Afrika Mashariki, Sadc Marekani na Jumuiya ya Madola kufanya tathmini na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru na haki.

“Tunasikitika kuwa ZEC imetangaza tena kuwa uchaguzi utarudiwa Zanzibar, wakati mazungumzo baina ya pande mbili yanaendelea. Kwa manufaa ya Watanzania wote, tunasisitiza kuwa hali ya kisiasa ya visiwani humo ni bora ikatatuliwa kwa pande mbili kukubaliana,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyotumwa kwa ushirikiano wa mabalozi wa Uholanzi, Norway, Hispania, Italia, Ujerumani, Finland, Ufaransa, Sweden, Uswisi, Uingereza, Ireland na Marekani inasisitiza kuwa kitendo cha upande mmoja kuamua kurudia uchaguzi, kinaweza kuzidisha hofu na taharuki miongoni mwa Wazanzibari.

“Tunawaomba Wazanzibari kuwa watulivu na wavumilivu nyakati hizi na tunazitaka pande zote mbili na washirika wao kuendelea kufanya kazi pamoja ili wapate suluhisho la amani,” ilisema taarifa hiyo.

Pia inasema ili uchaguzi uwe wa kuaminika, mchakato wake hauna budi kuziwakilisha pande zote na kuwa huru na wa haki.

Hata hivyo, mabalozi hao wamesema kulingana na mazingira ya Zanzibar kwa sasa, itakuwa vigumu kwa waangalizi wa kimataifa kutegemewa kushiriki kwa namna yoyote katika uchaguzi huo.
 
Matatizo ya wa Zanzibar hao mabalozi hawayajui, tunawashauri wakae kimya wasijifanye wanajua kila kitu.
 
Nivizuri,wasiogope kusema kweli.kuna viwatu hujidai vinahatimiliki ya hii nchi. Wanataka wao ndio waseme na kuamua hata kwakupindisha haki.
Machafuko yakitokea viongozi ndo wakwanza kukimbilia visa ubalozini na kuwaacha wananchi wakiteseka.
mabalozi wakisifia hatuwaambii waache kwakuwa hawaijui hii nchi ila wakikosoa mijitu mijinga inakuja resi kuwanyamazisha.
 
Matatizo ya wa Zanzibar hao mabalozi hawayajui, tunawashauri wakae kimya wasijifanye wanajua kila kitu.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliwashauri wajumbe wa Baraza la Mapinduzi Oktoba 1987 wakati anaaga aking’atuka uenyekiti wa CCM kumpisha Mzee Mwinyi, namnukuu, “…kusema kweli Rais Abeid Amani Karume alikuwa kielelezo cha ukatili na ukandamizaji. Visiwani alitawala kwa mkono wa chuma. Nasema kilichotokea ni kile nilichobashiri kingetokea, kwamba Wazanzibari wakaanza kuuana wao kwa wao na baadhi wasio na hatia waliouawa kikatili na ambao hawakuwa wanachama wa HIZBU wala chama chochote bali ASP waliuawa mmoja baada ya mwingine, hivyo hivyo na kwa ukatili wa kutisha”

Akilituhumu Baraza la Mapinduzi kwa kuridhia ukatili huo, Mwalimu alisema: “Hamuwezi kuepuka dhambi ya umwagaji damu huu, vitisho na vurugu; wala Baraza hili haliwezi kuwatumikia vyema Wazanzibari kwa kuwa limeghubikwa na ukatili mkubwa dhidi ya baadhi ya Wazanzibari”.
Mwalimu akasema, ilikuwa ni ujinga usio kifani, kwa watu kujengeana chuki na mauaji kwa misingi ya vyama vya kisiasa vya enzi za harakati za uhuru.

Chimbuko la mgawanyiko na chuki hizi, alibaini Mwalimu, ni Mwasisi wa Taifa hilo, hayati Abeid Amani Karume ambaye, kufuatia Mapinduzi ya 1964, aliapa na kupitisha Sheria (decreed) kwamba, pasingekuwa na uchaguzi Visiwani kwa miaka 50. Ni kusema kwamba, kama Karume angekuwa hai, uchaguzi wa kwanza Visiwani ungefanyika mwaka 2014, hatua ambayo Mwalimu aliifananisha na kusimika Usultani Visiwani.
 
Hao mabalozi wanajifanya wanayajua sana hayo matatizo ya zanzibar? Bac wayatatue wao
 
Maandiko na maneno ya mzee Nyerere yalikuwa yakifalsafa, maono ya mbali na maelekezo ya kusimamia haki na kweli aliyoyasemaa kwenye nukuu yako ndio tunayoyashuhudia
 
Ningetamani kuona hili tamko lao wanalichukulia siriaz,lakini uchaguzi utafanyika na ccm itashika dola na wao watakubaliana na maamuzi hayo na siku anaapishwa Shein watahudhuria kama hawajahi kutishia kitu vile sijui sisimu huwa inawafanyaga nini hawa mabalozi.
 
Wazungu wanafki awaweze kumpa au kumkubali mpembe mwenye asili ya kiarabu kutokea omani kuchukuwa au kutawala Zanzibar na kibaya zaidi ni muislamu mwenye itikdi kali ua mmeshasau kwamba wapemba ndio wanao mahusiano na mashekhe wa uwamsho ambao sasa hivi wako ngome pale ukonga
 
Katibu Mkuu wa CUF na aliyekuwa mgombea urais Zanzibari Ndg. Seif Shariff Hamad ndiye mwarabu ambaye unaona hastahili kuongoza Zanzibari? Kwa mtazamo wako unafikiri haki ni CCM kutawala ikiwezekana milele kuliko mtu kutoka chama kingine.

Katika kuyaenzi mawazo yako leo hii mwaka 2016, Sheikh Karume aliagiza kupitia “Agano” kwa hati ya siri ambayo ndilo kibuyu cha mizimu ya kale kinachosumbua Zanzibar na Muungano hadi leo kwamba.
Wazanzibari waliowahi kuwa wanachama wa vyama vya siasa mbali na ASP Visiwani pamoja na jamaa zao, wasipewe nafasi za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na katika Serikali ya Muungano.

Siri hii ilivuja Dr. Salim Ahmed Salim, alipoteuliwa na Mwl.Julius K. Nyerere kuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Mawaziri wawili Waandamizi Wazanzibari katika Serikali ya Muungano walikwenda kwa Waziri Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine, na kudai kwamba, walitumwa na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Sheikh Aboud Jumbe na Seif Bakari, kuitaka Serikali ya Muungano (Nyerere) ifute uteuzi wa Salim kwa sababu ulikiuka matakwa ya hati hiyo ya Siri ya enzi za Karume.

chuki uangamiza taifa
 
Matatizo ya wa Zanzibar hao mabalozi hawayajui, tunawashauri wakae kimya wasijifanye wanajua kila kitu.
Ila kipindi JK anaenda nje kwenye nchi zao mlisema anaenda kuhemea kibaba
Na mkawaona wa maana, ila sasa hawana maana si ndio?
 
Wazungu wanafki awaweze kumpa au kumkubali mpembe mwenye asili ya kiarabu kutokea omani kuchukuwa au kutawala Zanzibar na kibaya zaidi ni muislamu mwenye itikdi kali ua mmeshasau kwamba wapemba ndio wanao mahusiano na mashekhe wa uwamsho ambao sasa hivi wako ngome pale ukonga
Soma vizuri historia ya Zanzibari Sheikh Karume imeshindikana kuonekana kaburi la mababu zake lakini Sultani aliyepinduliwa kaburi la baba yake lilionekana visiwani zenj.
Unaowaita wapemba wenye asili ya kiarabu hawastahili kuongoza isipokuwa waswahili. Hao waarabu mababu zao waliingia Zanzibari karne ya 11 yani mwaka 1100, unaowaita kizazi cha waarabu leo karne ya 21 imepita zaidi ya miaka 900 waende wapi?
soma vizuri historia ya visiwa, hakuna mwenyeji kumshinda mwingine wote ni wahamiaji WEUSI na WAARABU. Karume inadaiwa asili yake Nyasa
 
Mnapoenda kutembeza mabakuli kwenye Nchi zao je? Hapo ndio matatizo yenu yanakua yanawahusu?

Pesa zenyewe za kufanyia Uchaguzi mpaka wawasaidie halafu mnajifanya vichwa ngumu.
Ila kipindi JK anaenda nje kwenye nchi zao mlisema anaenda kuhemea kibaba
Na mkawaona wa maana, ila sasa hawana maana si ndio?

Kwenda kwenye nchi zao kutembeza mabakuli au kuhemea kibaba sio tatizo mbona wao wanakuja kwetu na wanachuma vingi tu!

Matatizo ya Zanzibar hayawezi kumalizwa na kelele za wazungu, haya matatizo tunaweza kuyamaliza sisi wa Tanganyika au wa Zanzibar wenyewe. Tujifunze Zanzibar hakuna mgogoro wa kisiasa, Zanzibar kuna chuki, matatizo ya Zanzibar ni matatizo ya kihistoria.
 
Soma vizuri historia ya Zanzibari Sheikh Karume imeshindikana kuonekana kaburi la mababu zake lakini Sultani aliyepinduliwa kaburi la baba yake lilionekana visiwani zenj.
Unaowaita wapemba wenye asili ya kiarabu hawastahili kuongoza isipokuwa waswahili. Hao waarabu mababu zao waliingia Zanzibari karne ya 11 yani mwaka 1100, unaowaita kizazi cha waarabu leo karne ya 21 imepita zaidi ya miaka 900 waende wapi?
soma vizuri historia ya visiwa, hakuna mwenyeji kumshinda mwingine wote ni wahamiaji WEUSI na WAARABU. Karume inadaiwa asili yake Nyasa

Makaburi ya Babu wa Mhe. A.A. Karume yapo Malawi.
Ndiyo maana wanawe walisomea shule ya Mission huko huko Malawi.
Na prefect wao aliyekabidhiwa kuwatunza bwenini wakiwa Malawi ni mzee (70+) na bado anaishi kwenye kitongoji kimoja cha Stockholm.
 
Back
Top Bottom