Ukweli : Wabunge na madiwani waliojiuza wanaona aibu kujitokeza hadharani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,111
Huu ndio ukweli niliouona waziwazi , wamepoteza kabisa ule ujasiri waliokuwa nao , wako kama mtu aliyejisaidia hadharani kwa bahati mbaya baada ya kukumbwa na tumbo la kuhara

Ukiacha Waitara ambaye labda amepata ahueni baada ya kuokota unaibu waziri , wengine wote wanaona aibu hata kujitokeza hadharani tu ! hii ina maana kubwa sana ndugu zangu , ama kweli Usaliti ni laana mbaya mno !

Nachukua nafasi hii kuwapa pole sana familia za Wasaliti hao kwa aibu wanayopitia kwenye kipindi hiki , maana kama baba wa familia ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya familia anaweza kununuliwa hii inaleta picha mbaya sana na inaweka rehani familia nzima , familia haitajiamini tena na mwishowe inakata tamaa.
 
Dhambi ya usaliti inatawanyika kama moto wa nyika. Na bado 2020 ndipo watajifunza maana ya kusimama kama wewe na akili za kupachikwa uongeze na za kwako. Hakutakuwa na msaada wala kupita bila kura ya naoni. Haiwezekani sisi tufie chama tangu 1977 halafu utoke ulikokuwepo kuja kukaribia mezani tena bila kunawa.
 
Hiyo ni kawaida kwa watu waliobadilisha upepo,wanachukua muda kidogo kufit in kwenye mazingira mapya,wasiwasi wangu ni kuwa lowassa mwaka wa 3 sasa lakini ameshindwa kuendana na kasi ya Chadema kuandika habari za uongo mitandaoni
 
Jifunzeni demokrasia enyi bandugu. Mnasahu kuwa hata upande wa upinzani kuna waliohama kutoka upande wa chama tawala.
Haya mambo ya kuitana wasaliti ni sawa na gubu la mke mwenza tu.
 
Huwajui wanasiasa wewe...Au unasema tu kujiliwaza, mtu kama mwita waitara anaona aibu? au Mollel wa Hai? wakati ndio wamekuwa vocal zaidi? Labda ungesema Mtatiro
Sifa kubwa ya mwanasiasa ni uwezo wa kujivua akili na kutetea kitu ambacho hukiamini kabisa kwa nguvu zote, na hawa jamaa wanaweza hiyo kazi
 
Nilikua na jamaa yangu hata kwenye jumuia za kikristo hashiriki nasi tena anamtuma mkewe na watoto! Kila nikiwauliza watoto Baba yenu yuko wapi wanadai Baba hajisikii vizuri nahisi ni tumbo la kuhara kama mleta mada ulivyosema hapo
 
Back
Top Bottom