Ukweli wa vurugu Zanzibar ni huu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli wa vurugu Zanzibar ni huu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bornvilla, Jun 6, 2012.

 1. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Na Jabir Idrissa

  Hali mbaya ya usalama
  iliyoanza Jumamosi usiku,
  imesadifu nilichokieleza wiki
  mbili zilizopita. Nilimsihi Rais
  Dk. Ali Mohamed Shein, kupitia
  safu hii, kuwa asikubali maneno ya fitna anayolishwa
  na wasaidizi wake. Nikasema
  akikubali fitna, atajishawishi
  kukasirika; na matokeo ya mtu
  kukasirika, ni kuchukua hatua
  yenye madhara makubwa. Ilikuwa katika makala
  iliyojadili uhuru wa watu
  kusema na kujadili mambo ya
  nchi yao – ilitoka na kichwa
  cha habari kisemacho, “Hasira
  zako Dk. Shein, ni hasara kwako.” Kweli, hasira zilizowajaa
  viongozi wa serikali na vyombo
  vyao, zimezaa hasara. Sasa
  nchi, iliyokuwa imetulia
  kabisa, watu wakienda na
  kurudi kwenye shughuli za kutafuta maisha, imerudi
  kwenye hofu kubwa. Rais hakuongoza vizuri au
  walioelekezwa kuongoza
  hawakutenda vizuri. Hapa,
  hapakutumika hekima na
  busara kwa kiwango. Hapa,
  kuna hali ya serikali kutoonyesha uvumilivu kwa
  raia. Kwa kuwa Rais Dk. Shein ndiye
  kiongozi mkuu Zanzibar,
  analazimika kubeba lawama
  kwa madhara yaliyotokea.
  Yeye atatafuta wengine wa
  kuchangia lawama hizo. Kosa kubwa lililofanywa katika
  kadhia hii, ni uongozi kuruhusu
  Jeshi la Polisi kukamata
  kiongozi wa Jumuiya ya
  Uamsho, Sheikh Mussa Juma.
  Hapana. Kumkamata mtu si kosa, ila mazingira
  yaliyotumika. Ya Sheikh Mussa
  yalikuwa ya kigaidi na
  kijambazi. Yaliwashtua
  walioshuhudia. Wakajenga
  chuki dhidi ya serikali. Hebu nitangulize hali
  ilivyokuwa Jumapili kabla ya
  kurudi kueleza kilichotokea
  Jumamosi usiku.Soko la
  Darajani (maarufu la
  Mkunazini), lilifungwa kutwa nzima. Ndio tegemeo kwa
  wakazi wote wa maeneo ya
  katikati ya mji na nje kidogo
  (ng’ambo).Stendi kuu ya
  magari (daladala)
  inayohudumia wananchi (daladala) ilifungwa. Stendi hii
  pia inahudumia wasafiri
  watokao vijiji vya mkoa wa
  Mjini Magharibi, na mkoa wa
  Kusini Unguja (Wilaya ya Kati
  na ya Kusini). Usafiri wa umma na binafsi
  ulikwama kwa kuwa eneo la
  mkabala na lilipo soko hilo
  lilizuiwa kuingia magari.Mji
  mzima na vitongoji vyake
  ulienea sauti/milio ya risasi za mipira na mabomu ya machozi
  zilizofyatuliwa na polisi. Watalii walifadhaika sana kila
  waliposikia milio ya
  risasi.Vijana wenye hasira
  walienea mitaani kuleta
  tafrani.Mali nyingi ziliharibiwa,
  yakiwemo makanisa mawili. Inafaa sasa kueleza kwanini
  hayo yalitokea. Najadili
  yaliyojiri Jumamosi. Ilianza
  kwa utulivu kama kawaida,
  mpaka jioni. Nilikuwa mjini
  katika moja ya hoteli tukijadiliana masuala ya
  kitaifa na wenzangu. Tulipotoka saa 11, nilikimbilia
  waandishi wa habari kupata
  hili na lile – mambo
  yanayohusiana na habari.
  Utulivu mtupu.
  Nikasimuliwa Jumuiya ya Uamsho iliendesha mhadhara
  mpaka mchana kwenye
  uwanja wa Lumumba katika
  mfululizo wa ratiba
  inayoendelea kwa miezi sita
  sasa. Mihadhara ya asasi hii ya
  kidini, imekuwa na mvuto
  mkubwa kwa wananchi, hasa
  vijana ambao huwa wengi na
  kuifuata mpaka maeneo ya
  mikoani. Uamsho wameshaendesha zaidi ya
  mihadhara 50 Unguja na
  Pemba. Mhadhara ulihusisha
  matembezi yaliyoongozwa na
  Amir wa Uamsho, Sheikh Farid
  Hadi, msafara ukipitia Gulioni,
  Msikiti Mabuluu, Mlandege,
  Michenzani, Rahaleo, Kwa Biziredi na kurudia uwanjani
  Lumumba. Ilipofika saa 7 mchana,
  ulikuwa umekwisha; watu
  wametawanyika kwa amani na
  hakukuripotiwa tukio lolote la
  vurugu pamoja na askari polisi
  kuingilia msafara eneo la Kombawapya, wenyewe ukiwa
  umeshaingia uwanjani. Shwari
  ikaendelea mjini. Ilipokaribia saa 2 usiku,
  alitokea kijana mtanashati
  kufika msikiti wa Kwa Bizireni
  anaposali na kusomesha
  Sheikh Mussa, mmoja wa
  viongozi waliohudhuria. Hakuna aliyemfahamu kijana
  huyu. Alitoa salamu na kuitikiwa na
  wote waliokuwepo. Yule
  kijana aliyeonekana akishuka
  kwenye gari aina ya Noah,
  iliyopaki pembeni, alimvuta
  kiungwana Sheikh Mussa akimuomba wazungumze
  pembeni kidogo. Sheikh Mussa alimfuata kijana
  ambaye akiifuata gari.
  Alipofika akiwa nje ya gari,
  huku mlango wa nyuma ya
  dereva ukiwa wazi, Sheikh
  Mussa alisalimiana na mtu aliyekuwa ndani. Lakini, ghafla
  akavutwa ndani ya gari,
  mlango ukafungwa kwa nguvu,
  na dereva akaondoa gari kwa
  kasi.Ile ikashtua watu
  waliokuwa msikitini. Wakabaini Sheikh Mussa
  amechukuliwa na gari
  imeelekea Kariakoo. Walibaini baadaye iliishia
  kituo kikuu cha Polisi Mkoa
  kilichopo Mwembemadema.
  Wakapata uthibitisho kuwa
  Sheikh Mussa amekamatwa na
  kushikiliwa Madema. Waumini waliokuwa Kwa
  Biziredi walifadhaishwa.
  Hawakulala. Viongozi wa
  msikiti wakateua ujumbe
  kwenda kufuatilia Madema. Hakukuwa na kiongozi wa
  polisi kuthibitisha. Taarifa
  zilivuja kutoka ndani ya kituo
  kwamba Sheikh Mussa kweli
  anashikiliwa pale kituoni.
  Jitihada za viongozi wa msikiti kusihi Polisi wamuachie na
  kama kuna tuhuma apewe
  dhamana, hasa kwa kuwa
  familia yake haijui,
  zilishindikana. Taarifa za
  kukamatwa kwake zikaanza kuenea taratibu mjini. Haikuchukua muda, makundi
  ya watu wakakimbilia Madema
  kutaka kujua hatima ya Sheikh
  Mussa. Kwa kuwa Polisi
  hawakutaka kujadiliana,
  walijiandaa kulinda kituo chao na kulinda “mtuhumiwa” wao. Mwanzo wa matatizo ukawa
  umewadia. Polisi hawataki
  kusema wamemshika kiongozi
  wa Uamsho kwa tuhuma gani;
  wala hawapo tayari
  kujadiliana na yeyote ili kumpa dhamana. Huku watu
  waliokuwa wanajazana
  kituoni wakitaka kujua hatima
  ya kiongozi huyo. Ilipotimu saa 3 usiku, eneo la
  Michenzani, mita chache kufika
  Madema likawa limejaa watu
  wanaofuatilia hatima ya
  Sheikh Mussa. Ndipo polisi
  walipoanza kulinda hadhi yao baada ya kuamini
  wanachezewa. Risasi za mipira na mabomu ya
  kutoa machozi zikaanza
  kufyatuliwa moja baada ya
  nyingine. Kwenye saa 5 usiku,
  eneo hilo likawa limeenea
  harufu ya kemikali na moshi mzito. Sasa hata waliokuwa
  wapita njia na waliolala
  wakalewa sumu. Nilishindwa kupita kwa gari
  Kariakoo. Palikuwa na kundi
  kubwa la vijana; barabara
  imezibwa kwa mawe na
  mapande makubwa ya zege
  huku matairi yakiwaka moto. Niliposogea kwa kutembea
  nikijaribu kufika Michenzani,
  niliishia kwenye mkunazi, mita
  100 hivi kufika. Nikaona
  magari ya polisi waliosheheni
  silaha mbele ya ofisi kuu za Idara ya Majenzi. Kila baada ya muda fulani,
  nikasikia milio ya risasi na
  mabomu ya machozi
  zikielekezwa walipo vijana
  Kariakoo. Moshi na kemikali
  ziliponichosha, nikarudi eneo la Posta tulipoegesha gari. Pale Kariakoo, nikabaini vijana
  wamekata tamaa; hawakuwa
  na ujasiri wa kusonga mbele
  kwenda kufuatilia kiongozi
  wao Madema. Wafanyeje?
  Wakaanza kuondoka katika vikundi vidogovidogo
  wakielekea maeneo ya
  ng’ambo. Wakati wakitembea huku
  wengi wakiwa na mawe,
  marungu na mapande ya
  nondo, nilisikia baadhi yao
  wakisema, “Sasa kwa kuwa
  wametuzuia kumpata kiongozi wetu, tunasaka makanisa na
  baa tutayateketeza.”
  Wamekasirishwa na maudhi ya
  dola. Nikajua kazi
  itakayofanywa kutoka hapo, ni
  kazi chafu. Ndivyo ulivyokuwa usiku wa
  Jumamosi. Mpaka nilipolala,
  nikiwa hoteli ya Grand Palace,
  Malindi, nilikuwa nikisikia
  milio ya risasi ya hapa na pale.
  Hata nilipokuja juu yapata saa 9.30, nilisikia milio ya risasi,
  hali iliyoendelea hadi
  nilipoondoka mjini Zanzibar
  saa 7 mchana Jumapili. Sishangai kusikia Kamishna
  wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali
  Mussa amesema walikamata
  watu saba baada ya vurugu.
  Hakusema kamwe kama
  walimchukua kihuni kiongozi wa watu na hatimaye kuvutia
  umati kufika kituoni Madema
  kufuatilia. Taarifa yake ilikuja saa kadhaa
  baada ya uongozi wa Uamsho
  kutoa tamko wakisema
  hawahusiki na vurugu wala
  uharibifu wa mali uliofanywa.
  Uislamu unakataza vurugu, wamesema.
   
 2. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Posted on June 6, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na waandishi wa habari huko kituo cha televisheni cha serikali (ZBC) Zanzibar

  Jabir Idrissa
  KUNA uhalifu umefanywa Zanzibar. Ni katika matukio mabaya yaliyoanza usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Watu wamechochewa kupambana na dola. Hili halijaelezwa na serikali. Polisi wamevamia nyumba za viongozi wa Uamsho na kuvunja milango huku wakiwatukana matusi ya nguoni viongozi na familia zao sambamba na kuwatishia maisha. Polisi hawajalieleza hili. Amir (kiongozi) wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI), Sheikh Farid Ahmed Hadi anasema usiku wa Jumamosi hiyo, akiwa kwake, alipata taarifa anafuatwa na polisi wa kuzuia fujo (FFU).[​IMG][​IMG]
  Akajiandaa. Mnamo saa 7.30 kweli wakafika. Wakataka mlango ufunguliwe. Hakuna aliyewatii. Wakarusha risasi hewani. Hakuna aliyetoka. Hakuna aliyepiga kelele kutokea ndani. Lakini, baada ya kuona vishindo vimezidi, Sheikh Farid akasema kwa sauti, "Nipo ndani na familia yangu tumepumzika. Kama mpo tayari, fanyeni chochote nje ila, ninaapa kwa jina la Allah, anayekuja ndani, tutakabiliana mimi sina bunduki."
  Polisi hawakujali. Wakafyatua mabomu. Wakavunja mlango na kuvuruga walivyovikuta nje. Wakataka kuingia ndani. Wakakatazana, "hapana. Mnajua nani wamo ndani? Tuondokeni." Wakaondoka, anasimulia Sheikh Farid. Amepata simulizi kama hizo kwa viongozi wenzake wa Uamsho. Lakini sokomoko kama lililomkuta, lilitokea nyumbani kwa naibu wake, Sheikh Azzan Khalid Hamdan, wakati mwenyewe akiwa nje ya nchi kwa matibabu.
  Sheikh Azzan aliporudi Ijumaa, akapewa taarifa na familia yake kuwa walifika polisi wa FFU na kufanya fujo. Walifyatua risasi nje, wakavunja mlango. Wakapiga mayowe ya kumtukana matusi yeye na familia. Wakaondoka. Hakutulia. Alikwenda kupiga ripoti kituo cha polisi Mfenesini, karibu na anapoishi. Wakuu wakakana kufika kwake. Wakasema askari waliomfuata walitoka Mwembemadema.
  Mwembemadema ni makao makuu ya polisi mkoa wa Mjini Magharibi.

  Hawa ndio waliotuma makachero Jumamosi ile wakamshike Ustadhi Mussa Juma Issa, mmoja wa wahadhir wakuu wa Uamsho, kipenzi cha wahudhuriaji wa mihadhara ya jumuiya hii inayohamasisha Wazanzibari kuukataa muungano.
  Wapo watu wamejitokeza kutoa ushahidi wa walivyoona polisi wanalipua nyumba na mali za vitegauchumi za raia wema, zikiwemo gari zilizoegeshwa Kisiwandui na Michenzani. Mwanamke anayefanya kazi shirika la ndege la Kenya Airways, gari yake iliteketezwa kwa bomu lililorushwa na polisi. Matukio yote hayo katika siku mbili – Jumamosi na Jumapili.
  Leo, taarifa zimepatikana za uhalifu wa Polisi uliofanywa Jumatatu, 28 Mei, muda mfupi baada ya watuhumiwa 30 wa fujo, walipoachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mwanakwerekwe, mjini Zanzibar. Kati yao wapo viongozi wawili, akiwemo Ustadhi Mussa, wa Uamsho.
  Wakati wakili wao, Abdalla Juma akiwa Mahakama ya Ardhi, Vuga, vijana wa FFU walivamia ofisi zake Amani, yapata kilomita tano kutoka Vuga. Wakapitisha mitutu ya bunduki madirishani na kufyatua risasi na mabomu ya machozi.
  Hawakujali wafanyakazi waliokuwa ndani. Ni mchana kweupe. Hapana, ni mchana wa mola muumba mbingu na ardhi siku ya kazi, Jumatatu. Ipo taarifa ya Chama cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS) kulalamikia kitendo hicho. Wamemtumia barua Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, na kumtaka asake wahusika na kuwashitaki.
  ZLS wamekiita kitendo hicho cha makusudi kilicholenga kutisha mawakili wasiwe imara katika kazi yao ya kutetea wananchi wanaposhitakiwa. Polisi wanatuhumiwa sasa kushiriki vitendo vya uhalifu katika kipindi kilekile ambacho wao wanatuhumu Uamsho kuzusha ghasia mjini Zanzibar.
  Ninayaeleza haya ili kukumbusha historia ya kisiasa Zanzibar inayochefua. Siasa za maridhiano zilizoanza kustawi tangu 2010 mwishoni, zinachafuliwa kwa nguvu. Ni kama zilivyokuwa zikipandikizwa na kustawishwa siku zile za giza, mara tu mfumo wa siasa za vyama vingi, siasa za ushindani, uliporudishwa chini ya sheria ya Tanzania.
  Sasa wapo wasiotaka amani Zanzibar idumu. Wapo. Pengine wanampenda Amani Abeid Karume, kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, ambao walizijenga, bali wanachukia matunda ya maridhiano.
  Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Hapana; si peke yao. Kwa jumla, vyombo vya dola, vya dola, vya dola. Dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola. Vyote vilitajwa kupandikiza chuki kwa wananchi, mgongo ukiwa vyama vingi na uimara wa CUF. Visima vikapakwa kinyesi, ofisi za umma zikawashwa kwa viberiti na makanisa yakachomwa kiajizi. Kanisa linawashwa, dakika mbili tu hao walinzi wamefika.
  Ushetani ule ukakoma pale wananchi wa Shengejuu, kaskazini Pemba, walipovizia usiku kutafuta nani hasa wakihusika na vitendo vile vya kiharamia. Waliokutwa mpaka leo Polisi hawajawataja.
  Ni askari polisi na mashushushu ndani ya Landrover iliyosheheni madumu ya petroli, mapipa ya kinyesi na viberiti vya kuwashia mabomu ya chupa.

  Kutaka kuzubaisha umma wa Watanzania na ulimwengu, IGP Omari Mahita akaunda kikosi kuchunguza. Akamteua Robert Manumba, kachero aliyekuwa msaidizi mkuu wa DCI Adadi Rajabu, kukiongoza.
  Alitaka wachunguze chimbuko, sababu na wahusika wa milipuko ile ya kishetani pamoja na vitendo haramu vya kupaka kinyesi madarasa na kukimwaga kwenye visima vya maji wanayotumia wananchi.
  Tangu wakati ule, karibu miaka kumi sasa, si DCI Manumba ambaye sasa ndiye DCI, si IGP Mahita wala serikali iliyotoa ripoti ya uchunguzi huo. Wananchi waseme nini hapo? Lakini kwa sababu wahusika walijulikana na kufikia kukamatwa Shengejuu, zile fitna kuwa CUF walikuwa wahusika, zilifutika.

  Tungalinao wakorofi wasiopenda maridhiano. Wahafidhina ndani ya CCM wameibuka upya wakitaka kuharibu amani na utulivu. Hawawezi kuitaja CUF moja kwa moja maana wanashirikiana nacho kuendesha serikali.
  Wametafuta pa kuingilia – Uamsho. Kwa kuwa taasisi hii imechukua jukumu la kupigania haki za wananchi wasioridhishwa na mwenendo wa muungano, wanawapakazia kuwa wanavunja amani.
  Kumbe bado kuujadili Muungano wa Tanzania ni uhaini. Pamoja na serikali kuruhusu Watanzania watoe maoni yatakayotumika kuandika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watawala hawapendi watu wafikiri tofauti na wao.

  Tunaona kila viongozi wa polisi wanavyojitahidi kupotosha ukweli wa kilichotendeka mjini Zanzibar, ile dhamira yao ya kupotosha inawarudia. Wanatajwa baada ya kuonekana wazi wakivamia na kuharibu mali ikiwemo ofisi za wanasheria.
  Mpanga ubaya mwisho humrudia. Hawajajisafisha, wamejiumbua. Na ndiyo matokeo ya polisi nchini kushabikia siasa. Wanasubiriwa watamshika nani mchoma makanisa. Bado watafute ushahidi kuthibitisha kesi ya watu 30, pamoja na wafadhili wa Uamsho.

 3. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na waandishi wa habari huko kituo cha televisheni cha serikali (ZBC) Zanzibar

 4. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,027
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  NA JABIR IDRISSA

  Hali mbaya ya usalama iliyoanza Jumamosi usiku,imesadifu nilichokieleza wiki mbili zilizopita. Nilimsihi Rais Dk. Ali Mohamed Shein, kupitia safu hii, kuwa asikubali maneno ya fitna anayolishwa na wasaidizi wake. Nikasema akikubali fitna,atajishawishi kukasirika; na matokeo ya mtu kukasirika, ni kuchukua hatua yenye madhara makubwa. Ilikuwa katika makala iliyojadili uhuru wa watu kusema na kujadili mambo ya nchi yao – ilitoka na kichwa cha habari kisemacho, "Hasira
  zako Dk. Shein, ni hasara kwako." Kweli, hasira zilizowajaa viongozi wa serikali na vyombo vyao, zimezaa hasara. Sasa nchi, iliyokuwa imetulia kabisa, watu wakienda na kurudi kwenye shughuli za kutafuta maisha, imerudi
  kwenye hofu kubwa. Rais hakuongoza vizuri au walioelekezwa kuongoza hawakutenda vizuri. Hapa,hapakutumika hekima na busara kwa kiwango. Hapa,kuna hali ya serikali kutoonyesha uvumilivu kwa raia. Kwa kuwa Rais Dk. Shein ndiye
  kiongozi mkuu Zanzibar, analazimika kubeba lawama kwa madhara yaliyotokea.Yeye atatafuta wengine wa kuchangia lawama hizo. Kosa kubwa lililofanywa katika kadhia hii, ni uongozi kuruhusu Jeshi la Polisi kukamata kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mussa Juma.Hapana. Kumkamata mtu si kosa, ila mazingira yaliyotumika. Ya Sheikh Mussa
  yalikuwa ya kigaidi na kijambazi. Yaliwashtua walioshuhudia. Wakajenga chuki dhidi ya serikali. Hebu nitangulize hali
  ilivyokuwa Jumapili kabla ya kurudi kueleza kilichotokea Jumamosi usiku.Soko la Darajani (maarufu la Mkunazini), lilifungwa kutwa nzima. Ndio tegemeo kwa wakazi wote wa maeneo ya katikati ya mji na nje kidogo (ng'ambo).Stendi kuu ya magari (daladala) inayohudumia wananchi (daladala) ilifungwa. Stendi hii pia inahudumia wasafiri watokao vijiji vya mkoa wa Mjini Magharibi, na mkoa wa Kusini Unguja (Wilaya ya Kati na ya Kusini). Usafiri wa umma na binafsi ulikwama kwa kuwa eneo la mkabala na lilipo soko hilo lilizuiwa kuingia magari.Mji mzima na vitongoji vyake ulienea sauti/milio ya risasi za mipira na mabomu ya machozi zilizofyatuliwa na polisi. Watalii walifadhaika sana kila waliposikia milio ya
  risasi.Vijana wenye hasira walienea mitaani kuleta tafrani.Mali nyingi ziliharibiwa,yakiwemo makanisa mawili. Inafaa sasa kueleza kwanini hayo yalitokea. Najadili yaliyojiri Jumamosi. Ilianza kwa utulivu kama kawaida,mpaka jioni. Nilikuwa mjini
  katika moja ya hoteli tukijadiliana masuala ya kitaifa na wenzangu. Tulipotoka saa 11, nilikimbilia waandishi wa habari kupata hili na lile – mambo yanayohusiana na habari.Utulivu mtupu.Nikasimuliwa Jumuiya ya Uamsho iliendesha mhadhara
  mpaka mchana kwenye uwanja wa Lumumba katika mfululizo wa ratiba inayoendelea kwa miezi sita sasa. Mihadhara ya asasi hii ya kidini, imekuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi, hasa
  vijana ambao huwa wengi na kuifuata mpaka maeneo ya mikoani. Uamsho wameshaendesha zaidi ya mihadhara 50 Unguja na Pemba. Mhadhara ulihusisha matembezi yaliyoongozwa na Amir wa Uamsho, Sheikh Farid Hadi, msafara ukipitia Gulioni, Msikiti Mabuluu, Mlandege,Michenzani, Rahaleo, Kwa Biziredi na kurudia uwanjani Lumumba. Ilipofika saa mchana,
  ulikuwa umekwisha; watu wametawanyika kwa amani na hakukuripotiwa tukio lolote la vurugu pamoja na askari polisi
  kuingilia msafara eneo la Kombawapya, wenyewe ukiwa umeshaingia uwanjani. Shwari ikaendelea mjini. Ilipokaribia saa 2 usiku,alitokea kijana mtanashati kufika msikiti wa Kwa Bizireni anaposali na kusomesha Sheikh Mussa, mmoja wa viongozi waliohudhuria. Hakuna aliyemfahamu kijana huyu. Alitoa salamu na kuitikiwa na wote waliokuwepo. Yule kijana aliyeonekana akishuka kwenye gari aina ya Noah,iliyopaki pembeni, alimvuta kiungwana Sheikh Mussa akimuomba wazungumze pembeni kidogo. Sheikh Mussa alimfuata kijana ambaye akiifuata gari.Alipofika akiwa nje ya gari,huku mlango wa nyuma ya dereva ukiwa wazi, Sheikh Mussa alisalimiana na mtu aliyekuwa ndani. Lakini, ghafla
  akavutwa ndani ya gari,mlango ukafungwa kwa nguvu,na dereva akaondoa gari kwa kasi.Ile ikashtua watu waliokuwa msikitini. Wakabaini Sheikh Mussa amechukuliwa na gari imeelekea Kariakoo. Walibaini baadaye iliishia
  kituo kikuu cha Polisi Mkoa kilichopo Mwembemadema.Wakapata uthibitisho kuwa Sheikh Mussa amekamatwa na
  kushikiliwa Madema. Waumini waliokuwa Kwa Biziredi walifadhaishwa.Hawakulala. Viongozi wa msikiti wakateua ujumbe
  kwenda kufuatilia Madema. Hakukuwa na kiongozi wa
  polisi kuthibitisha. Taarifa zilivuja kutoka ndani ya kituo kwamba Sheikh Mussa kweli anashikiliwa pale kituoni.

  Jitihada za viongozi wa msikiti kusihi Polisi wamuachie na kama kuna tuhuma apewe dhamana, hasa kwa kuwa familia yake haijui,zilishindikana. Taarifa zakukamatwa kwake zikaanza kuenea taratibu mjini. Haikuchukua muda, makundi
  ya watu wakakimbilia Madema kutaka kujua hatima ya Sheikh Mussa. Kwa kuwa Polisi hawakutaka kujadiliana,walijiandaa kulinda kituo chao na kulinda "mtuhumiwa" wao. Mwanzo wa matatizo ukawa umewadia. Polisi hawataki
  kusema wamemshika kiongozi wa Uamsho kwa tuhuma gani;wala hawapo tayari
  kujadiliana na yeyote ili kumpa dhamana. Huku watu waliokuwa wanajazana
  kituoni wakitaka kujua hatima ya kiongozi huyo. Ilipotimu saa 3 usiku, eneo la Michenzani, mita chache kufika Madema likawa limejaa watu wanaofuatilia hatima ya Sheikh Mussa. Ndipo polisi walipoanza kulinda hadhi yao baada ya kuamini
  wanachezewa. Risasi za mipira na mabomu ya kutoa machozi zikaanza kufyatuliwa moja baada ya nyingine. Kwenye saa 5 usiku, eneo hilo likawa limeenea harufu ya kemikali na moshi mzito. Sasa hata waliokuwa wapita njia na waliolala
  wakalewa sumu. Nilishindwa kupita kwa gari Kariakoo. Palikuwa na kundi kubwa la vijana; barabar imezibwa kwa mawe na
  mapande makubwa ya zege huku matairi yakiwaka moto. Niliposogea kwa kutembea nikijaribu kufika Michenzani,niliishia kwenye mkunazi, mita 100 hivi kufika. Nikaona magari ya polisi waliosheheni silaha mbele ya ofisi kuu za Idara ya Majenzi. Kila baada ya muda fulani,nikasikia milio ya risasi na mabomu ya machozi
  zikielekezwa walipo vijana Kariakoo. Moshi na kemikali ziliponichosha, nikarudi eneo la Posta tulipoegesha gari. Pale Kariakoo, nikabaini vijana wamekata tamaa; hawakuwa na ujasiri wa kusonga mbele kwenda kufuatilia kiongozi
  wao Madema. Wafanyeje? Wakaanza kuondoka katika vikundi vidogovidogo wakielekea maeneo ya ng'ambo. Wakati wakitembea huku wengi wakiwa na mawe,marungu na mapande ya nondo, nilisikia baadhi yao wakisema, "Sasa kwa kuwa
  wametuzuia kumpata kiongozi wetu, tunasaka makanisa na baa tutayateketeza."Wamekasirishwa na maudhi ya dola. Nikajua kazi itakayofanywa kutoka hapo, ni kazi chafu. Ndivyo ulivyokuwa usiku wa Jumamosi. Mpaka nilipolala,
  nikiwa hoteli ya Grand Palace,Malindi, nilikuwa nikisikia milio ya risasi ya hapa na pale.Hata nilipokuja juu yapata saa 9.30, nilisikia milio ya risasi,hali iliyoendelea hadi nilipoondoka mjini Zanzibar saa 7 mchana Jumapili. Sishangai kusikia Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema walikamata watu saba baada ya vurugu.Hakusema kamwe kama
  walimchukua kihuni kiongozi wa watu na hatimaye kuvutia umati kufika kituoni Madema kufuatilia. Taarifa yake ilikuja saa kadhaa baada ya uongozi wa Uamsho kutoa tamko wakisema hawahusiki na vurugu wala uharibifu wa mali uliofanywa.
  Uislamu unakataza vurugu, wamesema.
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,794
  Trophy Points: 280
  Haya matango pori kuleni wenyewe,
  Kwa mfano: huyo sheihk farid alipoambiwa na askari kuwa wanamuhitaji kwa nini hakutii amri iyo???

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 6. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,315
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160

  ANAYEHITAJIWA HUFANYIWA HAYA KWANZA

  [video]http://www.mzalendo.net/habari/video-baadhi-ya-ukweli-kati-ya-ukweli-uliyojificha-machafuko-zanzibar[/video]
   
 7. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Unaumwa wewe.
   
 8. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wakati ule watu walipouwawa na polisi kwenye maandamano ya chadema kule Arusha , mashehe walikuwa wanasema chadema wanatakiwa watii mamlaka zilizopo hapa duniani kwa sababu hata maandiko matakatifu Biblia/Qoran yanatutaka tufanye hivyo...Nashindwa kuelewa ni kwanini vijana wa Uamsho walishindwa kutii amri ya polisi ya kutawanyika mpaka walipotawanyishwa kwa mabomu...kutokutii amri za mamlaka ndiyo chanzo cha vurugu hizo ...teh teh teh
   
Loading...