Ukweli wa mambo kadhaa kuhusu mapenzi ya karne hii!

Challya

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
462
579
1.Hakuna mwanamke ambae anaweza kukwambia ukweli kuwa ashatoka na wanaume wangapi kabla ya kuwa na wewe.

2.Unapokuwa kwenye mapenzi mapya usijisahau kwa kujionyesha,kuongea na kuringishia, siku zote penzi jipya hunoga lakini mapenzi ni kama jua huchomoza na huzama..na pia unapojua kupendwa usisahau kutendwa pia kupo!!!

3.Usijirahisishe kumpost mpenzi wako kwenye mitandao ya kijamii, mtu ambae hata inawezekana kwenu hajulikani,hata hamna dalili ya kuoana...kumpost kutafanya wale wenye mapenzi ya kweli na wewe wajiweke mbali nawe.

4. Mwanaume mwenzangu unapotafuta mwenza wa maisha basi ishi kiuhalisia,acha kuigiza maisha....mwambie ukweli huyo mwanamke, usitake uonekane wa hali ya juu wakati wewe ni wa kawaida tu....kuwa real yupo ambae atakupenda kama ulivyo.

5. Na nyie wanawake,je unajua katika maisha yako umeshafukuza wanaume wangapi wenye mapenzi ya kweli kwako kwasababu ya tabia yako chafu ya kudanga?....ebu acha hizo,tafuta kazi fanya utaenjoy maisha.

6. Mwanamke anayemuacha mwanaume wake kisa hana hela huo ni upumbavu wa kupindukia na huja kujutia kwasababu kwa mwanaume anayejielewa kufulia huwa ni kitu cha mpito tu.

7. Ewe dada na ewe kama uliopo kwenye mahusiano serious, basi unapoingia kwenye mitandao ya kijamii kuwa kama mtu ambae ni mume/mke/ mpenzi wa mtu na sio kujifanya upo single.

8. Mwanaume mpumbavu ni yule anayemuwekea bifu mwanamke kisa tu amememtongoza akakataliwa, ewe kaka tambua hilo ni ombi na sio amri na pia elewa mapenzi ni hisia,usilazimishe usipopendwa usije lia baadae!!

9. Ewe mwanamke uzuri unaweza ukakufanya uolewe haraka bali tabia zako ndio zitafanya udumu muda gani katika hiyo ndoa.

10. Hata siku moja usijutie au kulia kwa kuachana au kuachwa na mtu ambae alikuwa anaukudhara,hakupi muda wake,anakusaliti....bali unatakiwa ujutie kwa kuachana na mtu ambae alikuwa furaha kwako,muaminifu,mkweli na mkarimu kwako ila ujinga wako na upumbavu ukamuondoa kwako.

ITAENDELEA.............
9jastylezone-20191029-0003.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekupa LIKE kwa picha kali ya uzi wako.

Hiyo namba 4 imenigusa sana aisee!

Mwaka jana kuna mrembo alikuwa ananipenda ile mbaaya, na nilikuwa namficha hata shughuli ninazofanya ila akanipenda zaidi. Nikaja kumwambia mimi ninaendesha boda tena ni ya ndugu yangu tu, ila akazidi kunipenda ile mbaaya.

Mwaka huu nilisafiri hadi mjini kwao ili nikamwelezee habari njema za kutaka kumuoa; nimekuta ameshaolewa. Nilipata namba yake mpya akanambia alinipenda sana ila ndiyo hivyo ameshaolewa. Na alidhamiria kuishi nami kwa maisha yeyote yale ndiyo maana hakujali hata nilivyomwambia naendesha Pikipiki ya boss!

Ishi maisha halisi, au hata kama uko vizuri financially, jishushe kiasi ndipo utakapowaona wakupendao. Ila hawa tunaokutana nao batani ni ngumu kumuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata usimame juu ya anga uzungumze watakao kuelewa wachache sana
Ila niseme tuu, mara nyingi tuanadanganya kwa lengo la kukidhi haja na matamanio yetu. Bila uongo mambo hayaendi mkuu, ila yote na yote ahsante facts zilizoshiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekupa LIKE kwa picha kali ya uzi wako.

Hiyo namba 4 imenigusa sana aisee!

Mwaka jana kuna mrembo alikuwa ananipenda ile mbaaya, na nilikuwa namficha hata shughuli ninazofanya ila akanipenda zaidi. Nikaja kumwambia mimi ninaendesha boda tena ni ya ndugu yangu tu, ila akazidi kunipenda ile mbaaya.

Mwaka huu nilisafiri hadi mjini kwao ili nikamwelezee habari njema za kutaka kumuoa; nimekuta ameshaolewa. Nilipata namba yake mpya akanambia alinipenda sana ila ndiyo hivyo ameshaolewa. Na alidhamiria kuishi nami kwa maisha yeyote yale ndiyo maana hakujali hata nilivyomwambia naendesha Pikipiki ya boss!

Ishi maisha halisi, au hata kama uko vizuri financially, jishushe kiasi ndipo utakapowaona wakupendao. Ila hawa tunaokutana nao batani ni ngumu kumuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiongozi kwa utafiti wangu nilioufanya ni kwamba ni vigumu sana kumpata mwanamke ukimwambia ukweli !
 
Kiongozi kwa utafiti wangu nilioufanya ni kwamba ni vigumu sana kumpata mwanamke ukimwambia ukweli !
Kweli kabisa!
Ila mimi nilitumia style ya kujishusha ila akaendelea kunipenda ndiyo maana nikamuona anafaa kuwa mke mwema.

Hata mimi nilihofia kumwambia ukweli kwa kuhofia labda ange-fake tabia.
Ndiyo maana najutia kumkosa mke mwema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom