Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,522
- 24,010
Hili ni jambo ambalo halijawahi kuacha kunizunguka kichwani nikiwaza nini hasa kilitokea kwa kijana mwenzetu Deo Filikunjombe.
Huyu kijana pasipo watu kuangalia vyama vyao walimpenda na kumwona ni kijana ambaye alikuwa ni mzuri kwenye matendo sana kuliko kwenye maneno ya kinafiki kama wanasiasa wetu wengi waliopo sasa.
Mh Deo Filikunjombe alikuwa akiifanya siasa kwa matendo chanya katika Jimbo na Hatimaye Taifa. alisimamia alichoamini kwa matendo na imani kubwa. Na katika hili hakuangalia chama. aliangalia watu wake.
Ni wazi kuwa alionekana tishio kwa wanasiasa wengi vijana waliopo ndani ya chama chake.
Je ni kweli leo hii taumkumbuki tena Deo ? ni kweli amepita kama kivuli? hatujaweza kuhoji hasa mazingira ya kifo cake na kauli zilizowah kutolewa haraka baada tu ya kifo chake?
Watanzania tunawezaje kuwazungumzia watu wa hovyo hovyo walio kwenye system hivi sasa tukasahau vijana mahiri kama Deo? hakuwa na tamaa ya haraka kama waliyo nayo vijana wengi waliopo kwenye siasa hivi sasa ambao wamekuwa wakitudhalilisha sana kwa maamuzi na kauli zao za hovyo kiasi kwamba tunajuta kuwa na viongozi wa namna hiyo wenye nembo ya ujana.
Wakati mwingne tunawavumilia na kutetea ujinga na upuuzi wao kwa kisingizio cha chama lakini kiuhalisia ni matatizo katika Taifa hili.
Ni nani alihusika na kifo cha Deo? je kilikuwa cha kawaida au watu wametaka tuamini kuwa ni cha kawaida? kuna hadhithi nyingne zimekuwa zikisemwa lakini moja wapo ni kuwa kifo chake kinahusishwa na kijana mwenzie aliye ndani ya chama hasa baada ya kuona kuwa Deo anaonekana kuwa na nguvu na kupendwa na watanzania wengi kuliko huyo kijana ambaye uwezo wake ni mdogo isipokuwa amekuwa akibebwa.
Yamesemwa mengi lakini je ndo tuseme Deo amepita kama kivuli? hizi ni mbegu ambazo zilipaswa zipaliliwe na pia ziwekewe mbole vizuri kuikuza nchi yetu na hata zinapokufa zisiwe bure bali iwe ni nafasi nzuri ya kuzaa zaidi na zaidi. wamebaki vijana mafisadi, wanafiki,wenye kujijali wao zaidi, wenye kujipenda wao zaidi kuliko Taifa, wasio na uwezo mzuri kwa kuongoza na kunena maneno ya hekima.
Mimi na wewe tunaweza kujua kama tukiamua aliyesababisha kifo cha Mh Deo filikunjombe. tusinyamaze leo yeye kesho wewe..na unaponyamaza kimya kwa mwenzio mwishoni hata wewe hutapata wa kukupazia sauti .