Habari za muda huu wakuu.
Kuna taarifa za ndege kuanguka huko mkoani Pwani (Kisarawe) zinazoleta taharuki kidogo. Je, kuna watu labda wamebahatika kushuhudia au wenye ukweli wa taarifa yenyewe?
Mamlaka imesema kuwa sio ajali bali ni mazoezi ya uokoaji pindi linapotokea suala kama hili, sasa maswali yanaibuka kutokana na mwonekano wa ajali katika picha za uokoaji:
Je, mazoezi hayo huhusisha abiria wa kawaida au ni jeshi la uokoaji pekee?
Je, zoezi linahusisha abiria kujeruhiwa au kupoteza maisha katika kukamilisha zoezi hilo?
Je wananchi hupewa taarifa za mazoezi hayo ili wajiandae kiakili maana picha zinonesha watu kujeruhiwa vibaya kama sio kufa?
View attachment 2700698
Sent from my SM-G950U using
JamiiForums mobile app