IzukeneJr
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 758
- 753
Leo nimemkumbuka sana ndugu yangu na rafiki yangu Ndugu Othman Masoud Othman aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa Zanzibar kabla ya uteuzi wake kutenguliwa kwa kuwa tu aliipigia kura ya hapana katiba pendekezwa katika vifungu vinavyohusu muungano.
Sina hakika ni nchi gani tunaijenga na sina uhakika kama tunaweza kustawi na kuendelea ndani ya nchi ambayo watu wake hawana huru wa kufanya yale wanayoyaamini na kuyajua, badala yake kila mtu analazimika kufanya na kusema kile tu ambacho mkuu wake anataka kusikia au kuona.
Kwa mikono yetu kama taifa tunatengeneza taifa la watu waoga, wasio na uwezo wa kutoa sauti zao kueleza yale wanayoyaamini na kufikiria, badala yake sasa tunaamini kwamba ni RAIS PEKE YAKE ANAEJUA na hivyo tunafuata na kufanya lile tu analotuagiza.
Ndugu yangu Othman Masoud
Othman alisahau kwamba ukiwa Tanzania si kila jambo unapaswa kuliongea kwa namna unavyojisikia wewe. Kwa kutoa tu maoni yake ambayo yalipingana na maoni ya wakuu wake alionekana mtu asiyefaa na kuvuliwa cheo chake mara moja.
Raisi Obama ambae ni raisi wa taifa lenye nguvu zaidi duniani lakini kuna wakati na sio mara mija anakubali kwamba kuna mahali sera zake hazikuwa sahihi na anakaa na wapinzani wa sera zake wanajadiliana na mwisho wa siku kila mtu anakuwa ameridhika na nchi inastawi, tuihurumie Tanzania yetu, haya matabaka ya hawa na wale siyo mazuri na hayatatusaidia kama nchi, tuvumiane, tusikilizane tuijenge nchi yetu.
Fabian Izukene