Ukweli uliofichwa makusudi

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,049
2,000
UKWELI ULIOFICHWA MAKUSUDI

Kuelimika siyo kufaulu kwa vyeti vya alama za juu, bali kuwa na uwezo wa kuhoji mambo na kuyaelezea katika upeo mwingine wa uelewa.

Wakati nasoma moja ya shida nilikuwa napata ni kutopewa nafasi ya kuekezea mambo niyoaminishwa kwa namna nilivyokuwa nikiyaona mimi maana kwa kufanya hivyo hakuna tiki ya mwalimu ingegusa karatasi yangu, kwa lugha rahisi mfumo huu wa elimu ndiyo chanzo cha watu wengi kuwa wanafiki na waongo.

Na ndiyo maana sikuwahi kutaka kuwa mwalimu wa kufundisha mwanafunzi kukariri vitu ambavyo mimi mwenyewe vinanitatiza katika kuviamini na mbaya zaidi ni pale niliposoma maandishi fulani wakati nikisoma bible knowledge, maandishi yaliyosema "ole wao waalimu maana watahukumiwa kwa matendo ya maneno yao", kwa umri ule hii sentensi ilinifikirisha tofauti sana kuhusu suala la maarifa ya malimwengu.

Moja ya vitu nilifikiri tofauti ni habari zote za historia ya dunia na hasa Afrika hususani hapa Tanzania, katika kufikiri huko kwa kina nilibaini kuwa habari nyingi zinazofundishwa shuleni zimegawanyika mara tatu, zipo ambazo siyo za kweli kabisa, zipo zinazofundishwa katika upeo wa chini wa uelewa na zipo zinazo fundishwa kinyume chake, ila leo wacha nianze na hii moja.

Kwa upeo wangu na utafiti wangu wa muda mrefu, habari ya vita ya MAJIMAJI na shujaa KINJEKITILE NGWALE ni habari iliyopotoshwa makusudi na watunzi wa habari hiyo kupitia kitu kiitwacho ACADEMIC ESPIONAGE yaani ujasusi wa kitaaluma.

Ikumbukwe kuwa history is the study of past, present and future events particularly in human affairs, yaani " Utafiti wa matukio ya zamani, yaliyopo na yajayo, haswa katika maswala ya wanadamu.

Ajabu ni kuwa wakati wa kusoma somo la historia na habari zake kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu hakuna utafiti wowote unaofanyika wala kufanya, zaidi ya waalimu kuandika notsi ubaoni na wanafunzi kunakili ili waka kariri kwa ajili ya mitihani na baadaye wajisifu kama wana historia.

Hii ilinisukuma kuwa natembelea maeneo mengi ya kihistori nchi hii ili nitafiti historia na siyo nisome historia vile nitakavyo mimi na siyo utakavyo ujasusi wa taaluma ambao siku zote malengo yake siyo kupanua watu upeo bali kuwafuga katika zizi la uvungu wa ngazi ya mamlaka saba za ulimwengu.

Ukifika eneo la Matumbi Ngarambe wilayani rufiji mkoa wa Pwani mahali alikozaliwa shujaa Kinjekitile Ngwale mwasisi wa ukombozi Tanganyika uitwao na wajerumani "the maji maji rebellion" yaani uasi wa maji maji ambao leo tunaulainisha na kuuita vita ya maji maji, ni wazi ukizungumza na maji ya mto huu yatakupatia kumbukumbu zote za kweli kuhusu kilichotokea miaka ya 1905-1907.

Unaweza ukashangaa maji yanawezaje kukupatia taarifa hizo nami sitaki kukuaminisha sana, jifunze kuwasiliana na maji kisha nenda eneo hilo, ukihoji utajifunzia wapi nenda bagamoyo au ukerewe zungumza na wazee wajuzi watakuelekeza ila ukiamini propaganda za dini kuwa maarifa ya asili ni ushirikina endelea kubaki zizini siyo mbaya.

Wajerumani mpaka leo wameaminisha dunia kuwa walishinda vita ya maji maji na walimnyonga Kinjekitile Ngwale, na waalimu wameafundisha mwanafunzi wote wa nchi hii hivyo hivyo na zaidi katika hali ya kubeza kuwa wazee walikuwa wakitamka maji kila walipopigwa risasi ili ziyeyuke kitu ambacho ni uongo mkubwa kuwahi kufundishwa na watu wakaulipia ada.

Kwa kuwa History ni kutafiti basi wacha nikupe utafiti wangu, kwanza Kinjekitile Ngwale alikuwa ni MTU aliyepevuka katika viwango vya "immortal being" yaani kumbe kisichokufa kinachoweza kuonekana na kutoweka na uwezo huu ulifahamika kama "Hongo" kwa watu wa kabila lake, uwezo ambao leo hii angesemwa kuwa ana mzimu unaoweza kumtowesha.

Hivyo basi katika uwezo huo wa Kinjekitile uliokuwa ukimuijia kwa kuongozwa na joka kubwa(ukumbuke joka kiroho lina maana zaidi ya unayoijua) lililokuwa na uwezo wa kuondoka naye kuzama ndani ya mto rufiji na siku akitoka alikuwa mkavu kabisa, swali ni je hadithi ya Musa kutawanya maji kwa fimbo huko misri na za Yesu kutembea juu ya maji mbona ni hadithi kubwa kuliko hii ya Kinjekitile kuingia ndani ya maji siku kadhaa na kutoka akiwa mkavu?

Je waalimu wa historia wamewahi kuwaambia mwanafunzi uwezo huu aliokuwanao Kinjekitile Ngwale? Na waalimu wangapi wamewahi kufika eneo hili kutafiti haya? Ninahakika majibu ni bila bila.

Kutokana na uwezo huu Kinjekitile alikuwa tajiri sana wa mifugo na watu nyumbani kwake maana watu wengi walimfuata kwa ajili ya tiba, utabiri na maarifa ya siri aliyokuwanayo kuhusu maji na siri zake kubwa.

Hata alipoamuru kuanzwa kwa vita juai 1905 alifanya hivyo kwasababu kiunajimu mwezi julai ndiyo mwanzo mpya wa muda wa malimwengu hivyo alikuwa na maarifa ya juu sana wakati ambao hakuwahi kusoma kwenye darasa la mkoloni chini ya mfumo wao wa elimu pumbazi.

Falsafa ya kupigana kwa njia ya maji ni falsafa ya kweli kabisa sawa na ile inayoelezewa kumhusu Musa na majeshi ya wamisiri kuwa yalimezwa na maji, na falsafa hiyo hiyo ndiyo ile inaelezwa katika hadithi ya nuhu na gharika, shida ya hii ya Kinjekitile na Maji maji iliandikwa na mjerumani kwa faida zake ambazo kamwe hawezi kumkweza mtu mweusi.

Ukijifunza siri za miujiza ya maji utabaini kuwa falsafa ya maji maji ilikuwa na uwezo kabisa wa kufanya kile alichokielewa Kinjekitile, tatizo lilikuwa baadhi ya wale aliowapatia falsafa ile kutokuwa katika upeo wake wa uelewa, maana kama wangemuelewa, kile kitokeacho kwenye filamu ya pradetor ya Arnold Schwarzenegger ndicho kingewatokea, yaani wapiganaji wa Tanganyika wangekuwa invisible kwa majeshi ya kikoloni.

Hivyo nathubutu kusema kuwa habari ya kwamba Kinjekitile aliwaambia watu waseme maji kila wapigwapo risasi ni kumdhalilisha shujaa wa taifa hili, ni kuyadhalilisha maji mama wa uumbaji na ni kutudhalilisha wote tuitwao kwa jina la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni wazi tunapaswa kuwataka radhi mababubu zetu hawa kwa kupokea udhalilishwaji wao.

Pili kama Kinjekitile alikuwa na uwezo wa kuondoka ndani ya mwili wake na kuzama majini siku kadhaa bila kufa, nijuavyo mimi kile wasemacho wajerumani kuwa walimnyonga Agosti 24,1905 ni uongo, maana hata yesu wanasema alisulubiwa akafa, akazikwa lakini siku ya tatu hawakumkuta kaburini

Swali ni, miujiza ya Kinjekitile na ile ya Yesu mbona inafanana kabisa, sasa kwanini tukubali kuwa Kinjekitile alinyongwa mpaka kufa ila Yesu wa kiyahudi tukubali kuwa alisulubiwa na kufufuka kwa gia kuwa alikuwa mwana wa Mungu kwani Kinjekitile yeye alikuwa mwana wa nani?

Kwa mantiki hiyo naweza sema wajerumani hawakumnyonga Kinjekitile mpaka kufa ila labda waseme walinyonga kivuli cha mwili wake baada ya kumkuta ameshaondoka na mzimu wake Hongo, kwani moja ya maarifa ya wajuzi hueleza kuwa mtu akishafikia kiwango cha immortal alichokuwanacho Kinjekitile Ngwale, huweza kuuvua mwili na kuacha kivuli watu wakakiona kama ndiye wewe halisi.

Kutokana na hayo machache, nasema kuwa maji maji haukuwa uasi bali ujuzi wa asili wa kutumia maji kujihami, ujuzi uliofunuliwa kwa wamatumbi na watanganyika wengine kwa wakati huo kujihami dhidi ya ujinga wa kijerumani wakutegemea uwezo wa mwili na silaha wakati watanganyika chini ya shujaa msomi wa siri za malimwengu Kinjekitile Ngwale wakitumia nguvu mama asili ya uumbaji.

Na bila kupepesa maneno washindi walikuwa watanganyika na siyo wajerumani maana kama wajerumani ndiyo wangekuwa wameshinda vita ile basi leo hii wao ndiyo wangekuwa wanaishi Rufiji, maana unawezaje kushinda vita halafu ukimbie eneo lako la ushindi?

Mwisho, serikali ya Tanzania kupitia wizara zake za mambo ya ndani, elimu, sanaa habari na utamaduni pamoja na usalama wa taifa inapaswa kupitia upya historia ya hadithi zote za kuandikwa na wakoloni maana zote ni uongo mtupu na udhalilishwaji mkubwa wa Taifa, na ikiwezakana wawadai fidia wahusika kwa kuichafua sura ya kweli ya historia ya taifa.

Hofu ni nani wa kumfunga paka kengele?

Anyways, umesoma nini chuo kikuu? Nimesoma European history! Wow, unaishi wapi? Chunya Mbeya Tanzania!
WAJINGA SISI.
 
Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
1,814
2,000
Ungeenda pia ukaone kazi ya bwawa la Nyerere inavyoendelea na ukweli wake. Halafu ulinganishe na hadithi za wana siasa. Utagundua vitu viwili tofauti. Bwawa la Nyerere lipo kama Km 200m toka Kibiti na kusema kweli litaibadili sana nchi yetu.

Naungana kabisa na hoja yako ya kupenda kudadisi mambo na sio kukaririr kila tunachoambiwa. Tunadanganywa mambo mengi sana. sababu ya kukosa udadisi, tunaangukia kuamini kila neno linalosemwa.

Hatuwezi kuwa watu huru kama hatutatafuta elimu na ustaarabu unaofaa kwa kutumia akili zetu. Tusipende kujiona wanyonge au sio binadamu kamili sababu ya haya mambo tuliokaririshwa
 
Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
1,814
2,000
Chapisheni vitabu, watu wasome hayo makosa ya kihistoria...
Hii ndio kazi ya wasomi wetu. Namsifu sana Prof Mwandosya. Anaandika mada mtambuka. Anapenda sana kueleza kwa ufasaha yale anayoyaona, nje ya fani yake ya uhandisi. Ndio wasomi wanavyotakiwa kuwa.

Hawa wengine ni wasomi wa aina gani? Wanatuletea matatizo kuliko suluhisho. Sasa kwanini wanajiita wasomi?
 
Bigawas

Senior Member
Feb 19, 2021
125
225
Mkuu andaa mada ya historia yake ili tujue undani wa huyu mwamba. Kwenye historia ya darasani hawakumwelezea kiundani.
 
nzaghamba

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
713
1,000
safi sana ingawa nina maswali mawili:

(1) je kiukweli yeye "Kinje" alikufa wapi na lini.

(2) historia inayofundishwa baada ya ukoloni vinatungwa au kuandaliwa na nani(Watanzania au wajeremani?)
 
Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
12,692
2,000
Hii ndio kazi ya wasomi wetu. Namsifu sana Prof Mwandosya. Anaandika mada mtambuka. Anapenda sana kueleza kwa ufasaha yale anayoyaona, nje ya fani yake ya uhandisi. Ndio wasomi wanavyotakiwa kuwa.

Hawa wengine ni wasomi wa aina gani? Wanatuletea matatizo kuliko suluhisho. Sasa kwanini wanajiita wasomi?
Tatizo Tanzania imejaa watu wanaopenda kulalamika na kukosoa tu.
 
Ushindi victory

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
375
1,000
Aya mambo ya elimu tumeyapigia sana kelele lakin waapi serkla iko kimya tuu,,kiukwel masomo yetu yanatakiwa kubadilishwa sana tena saana maana yamejawa ujinga na uongo mkubwa sana,,,historia ya tz insanzia baada ya utumwa nyuma kidg lakn aisem miaka1000 kabla tz na afrika ilikuwaje.....historia ya kwel inasema hiv afrika ni kongwee sana,tukija hapa east afrika ni kongwe pia zaid ya hizo nchi za wazungu kuwepo, east afrki apa ndioo palijulkana kama mesopotamia ya kwel na ndipo pia babilon ilkuwako, na ndiko mnala wa babel ulijengwa hapaa , mnara wenyew ulkuwa ni pyramid kama ile ya misri ,kitendo kilichomfnya mpka Mungu kuigawanya dunia na kufanya mabara yawe7,..pia east afrka ndipo ilituwa safina ya nugu, pia bustani ya eden ilikuwahuku huku, pia kiswahili ni lugha kongwe kulko lugha yoyote ya kikolon, kiswahil ni miongon mwa lugha za kibantu na za asiri ya mtu wa kale ambaye ni adamu, adamu na eva waltumia lugha za kibantu kuwasiliana baina yao maana pia waliishi afrika,,ukichunguka lugha nying za kibantu hufanana saana na ndio zilizotoka katk lugha mama ya mwanzon kabisa kabla hata ya mnara kuvunjika na kuleta izo takataka nyingne kama kiarabu na lugha ngumu z watu weupe,,,east afrika ilikuwa kongwe saana, tulikuwa na mifumo yetu ya dini,utawala na uchumi, wivu wa wazungu awa wageni ndio ulpelekea kuiarbu afrika, watu wanazan wazungu wameanza kuihujum Africa juz tu apo walipoanza kufanya utumwa kumbe tangu mwanzo mzungu alikuwa kikwazo kwa mtu mweus,mtu mweupe kaanza kitambo kuiangamiza afrika hata kabla ya kristo awa jamaa walikuwa wakituvamia polepole kutupunguza nguvu, mpka walipofanikiwa kuja kabsa kuiaribu na kutuweka utumwani kwa zaid ya miaka400,,msilolijus ni kuwa hata lile sanduku la agano la kale lipo humu humu baran afrika,,japo ayo majambaz yajiitayo wachungaji yanapotosha ukwel kwa kujua ama kutojua,,siku waafrika mkamludia Mungu wenu aliewatoa utumwan kwa wazungu ndio siku mutaungana na kuirudisha afrika ya kale kuitawala dunia,,east afrika ni pepo ya dunia, hakuna janga wala vita wala tatz lolote litakaloidhuru east afrika maana ndio sehem mahalum alioumbiwa mwanadamu pia n sehem sarama zaid dunian japo pia hawatak mujue kwel,,sku mukaachana na elimu uchwara ya kipuuz iyo na kuirudia elmu yetu tuliotenda makubwa bas atutowategemea tena wazungu,,,kuna safar ndefu sana ya kuwafanya watz wajitambue, weng akili zmekalia kushoto wameshikwa na dini &elimu uchwara, hiz ndizo siraha za adui kuipumbaza akili ya mwafrika,,mtu mweysi haitaj dini wala elimu ya mtu mgeni, maana mzungu si ndugu yako na hatowahi kuwa ndug yako, inashangaza hata awa wanaoshobokea rang nyeupe, inashangaza ata wanaosubutu kuoa watu weupe,,zaman ilkuwa ni kufuru kuchafua dam kwa kuzaa na mtu mweupe maana awo ni aliens au uzao wa maraika wahasi, viumbe waliokuja dunian kwa bahat mbaya, nandio hawa wanaoiarbu dunia kwakila kitu.......WAKE UP AFRICAN
 
kianja kyamutwara

Senior Member
Nov 4, 2020
180
250
Kuna mambo umeandika sijakuelewa vizuri ulilenga kuelezea nini, mosi, ulisema kinjekitle hakufa je yupo wapi mbona tokea waliposema wamemuua huo mzimu haukuwai kutokea tena?, pili umezungumuzia eti wajerumani kwanini hawapo rufiji mpaka sasa hujaeleza baada ya vita ya majimaji nini kiliendelea kwani mpaka tunapata uhuru tulikua na muingereza hivo kwakiasi kikubwa ninakubaliana na wewe ila baaddi ya mambo yalikua kweli, na ndomaana kuna views mbili Afrocentric views na urocentric views. Asante kwa kutugikirisha ila baadhi ya hiyo uliyoiita ya wazungu ni kweli.
 
solars

Member
Sep 1, 2020
77
150
UKWELI ULIOFICHWA MAKUSUDI

Kuelimika siyo kufaulu kwa vyeti vya alama za juu, bali kuwa na uwezo wa kuhoji mambo na kuyaelezea katika upeo mwingine wa uelewa.

Wakati nasoma moja ya shida nilikuwa napata ni kutopewa nafasi ya kuekezea mambo niyoaminishwa kwa namna nilivyokuwa nikiyaona mimi maana kwa kufanya hivyo hakuna tiki ya mwalimu ingegusa karatasi yangu, kwa lugha rahisi mfumo huu wa elimu ndiyo chanzo cha watu wengi kuwa wanafiki na waongo.

Na ndiyo maana sikuwahi kutaka kuwa mwalimu wa kufundisha mwanafunzi kukariri vitu ambavyo mimi mwenyewe vinanitatiza katika kuviamini na mbaya zaidi ni pale niliposoma maandishi fulani wakati nikisoma bible knowledge, maandishi yaliyosema "ole wao waalimu maana watahukumiwa kwa matendo ya maneno yao", kwa umri ule hii sentensi ilinifikirisha tofauti sana kuhusu suala la maarifa ya malimwengu.

Moja ya vitu nilifikiri tofauti ni habari zote za historia ya dunia na hasa Afrika hususani hapa Tanzania, katika kufikiri huko kwa kina nilibaini kuwa habari nyingi zinazofundishwa shuleni zimegawanyika mara tatu, zipo ambazo siyo za kweli kabisa, zipo zinazofundishwa katika upeo wa chini wa uelewa na zipo zinazo fundishwa kinyume chake, ila leo wacha nianze na hii moja.

Kwa upeo wangu na utafiti wangu wa muda mrefu, habari ya vita ya MAJIMAJI na shujaa KINJEKITILE NGWALE ni habari iliyopotoshwa makusudi na watunzi wa habari hiyo kupitia kitu kiitwacho ACADEMIC ESPIONAGE yaani ujasusi wa kitaaluma.

Ikumbukwe kuwa history is the study of past, present and future events particularly in human affairs, yaani " Utafiti wa matukio ya zamani, yaliyopo na yajayo, haswa katika maswala ya wanadamu.

Ajabu ni kuwa wakati wa kusoma somo la historia na habari zake kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu hakuna utafiti wowote unaofanyika wala kufanya, zaidi ya waalimu kuandika notsi ubaoni na wanafunzi kunakili ili waka kariri kwa ajili ya mitihani na baadaye wajisifu kama wana historia.

Hii ilinisukuma kuwa natembelea maeneo mengi ya kihistori nchi hii ili nitafiti historia na siyo nisome historia vile nitakavyo mimi na siyo utakavyo ujasusi wa taaluma ambao siku zote malengo yake siyo kupanua watu upeo bali kuwafuga katika zizi la uvungu wa ngazi ya mamlaka saba za ulimwengu.

Ukifika eneo la Matumbi Ngarambe wilayani rufiji mkoa wa Pwani mahali alikozaliwa shujaa Kinjekitile Ngwale mwasisi wa ukombozi Tanganyika uitwao na wajerumani "the maji maji rebellion" yaani uasi wa maji maji ambao leo tunaulainisha na kuuita vita ya maji maji, ni wazi ukizungumza na maji ya mto huu yatakupatia kumbukumbu zote za kweli kuhusu kilichotokea miaka ya 1905-1907.

Unaweza ukashangaa maji yanawezaje kukupatia taarifa hizo nami sitaki kukuaminisha sana, jifunze kuwasiliana na maji kisha nenda eneo hilo, ukihoji utajifunzia wapi nenda bagamoyo au ukerewe zungumza na wazee wajuzi watakuelekeza ila ukiamini propaganda za dini kuwa maarifa ya asili ni ushirikina endelea kubaki zizini siyo mbaya.

Wajerumani mpaka leo wameaminisha dunia kuwa walishinda vita ya maji maji na walimnyonga Kinjekitile Ngwale, na waalimu wameafundisha mwanafunzi wote wa nchi hii hivyo hivyo na zaidi katika hali ya kubeza kuwa wazee walikuwa wakitamka maji kila walipopigwa risasi ili ziyeyuke kitu ambacho ni uongo mkubwa kuwahi kufundishwa na watu wakaulipia ada.

Kwa kuwa History ni kutafiti basi wacha nikupe utafiti wangu, kwanza Kinjekitile Ngwale alikuwa ni MTU aliyepevuka katika viwango vya "immortal being" yaani kumbe kisichokufa kinachoweza kuonekana na kutoweka na uwezo huu ulifahamika kama "Hongo" kwa watu wa kabila lake, uwezo ambao leo hii angesemwa kuwa ana mzimu unaoweza kumtowesha.

Hivyo basi katika uwezo huo wa Kinjekitile uliokuwa ukimuijia kwa kuongozwa na joka kubwa(ukumbuke joka kiroho lina maana zaidi ya unayoijua) lililokuwa na uwezo wa kuondoka naye kuzama ndani ya mto rufiji na siku akitoka alikuwa mkavu kabisa, swali ni je hadithi ya Musa kutawanya maji kwa fimbo huko misri na za Yesu kutembea juu ya maji mbona ni hadithi kubwa kuliko hii ya Kinjekitile kuingia ndani ya maji siku kadhaa na kutoka akiwa mkavu?

Je waalimu wa historia wamewahi kuwaambia mwanafunzi uwezo huu aliokuwanao Kinjekitile Ngwale? Na waalimu wangapi wamewahi kufika eneo hili kutafiti haya? Ninahakika majibu ni bila bila.

Kutokana na uwezo huu Kinjekitile alikuwa tajiri sana wa mifugo na watu nyumbani kwake maana watu wengi walimfuata kwa ajili ya tiba, utabiri na maarifa ya siri aliyokuwanayo kuhusu maji na siri zake kubwa.

Hata alipoamuru kuanzwa kwa vita juai 1905 alifanya hivyo kwasababu kiunajimu mwezi julai ndiyo mwanzo mpya wa muda wa malimwengu hivyo alikuwa na maarifa ya juu sana wakati ambao hakuwahi kusoma kwenye darasa la mkoloni chini ya mfumo wao wa elimu pumbazi.

Falsafa ya kupigana kwa njia ya maji ni falsafa ya kweli kabisa sawa na ile inayoelezewa kumhusu Musa na majeshi ya wamisiri kuwa yalimezwa na maji, na falsafa hiyo hiyo ndiyo ile inaelezwa katika hadithi ya nuhu na gharika, shida ya hii ya Kinjekitile na Maji maji iliandikwa na mjerumani kwa faida zake ambazo kamwe hawezi kumkweza mtu mweusi.

Ukijifunza siri za miujiza ya maji utabaini kuwa falsafa ya maji maji ilikuwa na uwezo kabisa wa kufanya kile alichokielewa Kinjekitile, tatizo lilikuwa baadhi ya wale aliowapatia falsafa ile kutokuwa katika upeo wake wa uelewa, maana kama wangemuelewa, kile kitokeacho kwenye filamu ya pradetor ya Arnold Schwarzenegger ndicho kingewatokea, yaani wapiganaji wa Tanganyika wangekuwa invisible kwa majeshi ya kikoloni.

Hivyo nathubutu kusema kuwa habari ya kwamba Kinjekitile aliwaambia watu waseme maji kila wapigwapo risasi ni kumdhalilisha shujaa wa taifa hili, ni kuyadhalilisha maji mama wa uumbaji na ni kutudhalilisha wote tuitwao kwa jina la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni wazi tunapaswa kuwataka radhi mababubu zetu hawa kwa kupokea udhalilishwaji wao.

Pili kama Kinjekitile alikuwa na uwezo wa kuondoka ndani ya mwili wake na kuzama majini siku kadhaa bila kufa, nijuavyo mimi kile wasemacho wajerumani kuwa walimnyonga Agosti 24,1905 ni uongo, maana hata yesu wanasema alisulubiwa akafa, akazikwa lakini siku ya tatu hawakumkuta kaburini

Swali ni, miujiza ya Kinjekitile na ile ya Yesu mbona inafanana kabisa, sasa kwanini tukubali kuwa Kinjekitile alinyongwa mpaka kufa ila Yesu wa kiyahudi tukubali kuwa alisulubiwa na kufufuka kwa gia kuwa alikuwa mwana wa Mungu kwani Kinjekitile yeye alikuwa mwana wa nani?

Kwa mantiki hiyo naweza sema wajerumani hawakumnyonga Kinjekitile mpaka kufa ila labda waseme walinyonga kivuli cha mwili wake baada ya kumkuta ameshaondoka na mzimu wake Hongo, kwani moja ya maarifa ya wajuzi hueleza kuwa mtu akishafikia kiwango cha immortal alichokuwanacho Kinjekitile Ngwale, huweza kuuvua mwili na kuacha kivuli watu wakakiona kama ndiye wewe halisi.

Kutokana na hayo machache, nasema kuwa maji maji haukuwa uasi bali ujuzi wa asili wa kutumia maji kujihami, ujuzi uliofunuliwa kwa wamatumbi na watanganyika wengine kwa wakati huo kujihami dhidi ya ujinga wa kijerumani wakutegemea uwezo wa mwili na silaha wakati watanganyika chini ya shujaa msomi wa siri za malimwengu Kinjekitile Ngwale wakitumia nguvu mama asili ya uumbaji.

Na bila kupepesa maneno washindi walikuwa watanganyika na siyo wajerumani maana kama wajerumani ndiyo wangekuwa wameshinda vita ile basi leo hii wao ndiyo wangekuwa wanaishi Rufiji, maana unawezaje kushinda vita halafu ukimbie eneo lako la ushindi?

Mwisho, serikali ya Tanzania kupitia wizara zake za mambo ya ndani, elimu, sanaa habari na utamaduni pamoja na usalama wa taifa inapaswa kupitia upya historia ya hadithi zote za kuandikwa na wakoloni maana zote ni uongo mtupu na udhalilishwaji mkubwa wa Taifa, na ikiwezakana wawadai fidia wahusika kwa kuichafua sura ya kweli ya historia ya taifa.

Hofu ni nani wa kumfunga paka kengele?

Anyways, umesoma nini chuo kikuu? Nimesoma European history! Wow, unaishi wapi? Chunya Mbeya Tanzania!
WAJINGA SISI.
Asante. Hivi Kinjekitile alikuwa kabila gani? Na kama hakuuawa na Wajerumani, basi alikufa kifo gani (maradhi, uzee, au vinginevyo)? Na alikufa mwaka gani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom