Mtalebani
Member
- Aug 22, 2014
- 23
- 57
HUU UKWELI NI MCHUNGU KWA KWELI.
1. Kamwe usiishi na mwanaume ambae hujaolewa nae, usiishi na 'boyfriend' wako kinyumba hata kama ni mchumba wako, utaonekana uko 'cheap' na ndoa unaweza ukaisikia kwenye bomba.
Labda kama mmeamua kuishi hivyo hivyo bila Ndoa halali inayotambulika either na serikali au dini yenu.
2. Usibebe mimba ya boyfriend wako. Sio busara. Zuia kupata mimba kabla hajakuoa. Kumbuka kwamba kamwe huwezi kutumia ujauzito kama kigezo cha kumfanya akuoe. Wanaume wangapi wana watoto nje ya Ndoa?
3. Jitahidi kuzuia kutoa mimba, mmefanya, umepata mimba itunze kutoa mimba kunaweza kukakufanya uwe mgumba maisha.
4. Kamwe usiwatenge wazazi wako kwa sababu ya mwanaume, muda mwingine mapenzi hufanya watu waonekane wapumbavu. Usiruhusu mapenzi yatawale akili yako, penda kwa akili na sio kwa moyo.
5. Usifikiri kujiua kisa 'boyfriend' wako kukutosa, hana thamani hiyo, sio mwanaume mzuri pekee katika dunia.
6. Usipoteze masomo yako kwa sababu mwanaume amekutaka umtembelee kwake. Hii itakufanya uonekane uko 'cheap' pia na kumbuka kesho yako ni muhimu kuliko huyo 'boyfriend' wako mlikokutana ukubwani.
7. Usimwombe mwanaume akuoe, hustahili kufanya hivyo na wewe una thamani yako, usijiweke kuwa wa rahisi kiasi hicho.
8. Hakuna kitu mwanaume hapendi kama majibizano, kubaki kimya ni adhabu kubwa sana kwa mwanaume mkorofi. Niamini mimi katika hili.
9. Katika ndoa Usimchunguze mwanaume kama unampenda na unajua huwezi kumuacha. Mwanaume siku zote huhitaji nafasi na uhuru, hapendi kuingiliwa katika mambo yake, mnaweza mkapinga ila huo ndio ukweli toka enzi na enzi. Kama una uwezo wa kuachana nae mchunguze tu bila wasiwasi wowote.
10. 'Wavulana' hutizama mwili wa mwanamke na kumhitaji kwa ajili ya kuburudisha maungo yao, ila 'wanaume' hutizama hulka na tabia za mwanamke katika malezi, uvumilivu, usaidizi, ushauri wa maendeleo na amani ya moyo
HAPPPY NEW YEAR 2017
Follow@alexmfikwa.