Ukweli tuuweke hapa kuhusu Kassim Mganga!

komba05

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
367
291
Habari zenu wakuu!

Nimefikiria kitu kuhusu huyu jamaa, katika tasnia ya mziki hapa Tanzania! Huyu jamaa yupo vizuri, ukisikiliza nyimbo zake kuna tungo nzuri kwa lugha yetu ya kiswahili fasaha pasipo kuchanganya lugha za kigeni, pia ana mashairi yaliyotulia pasipo kuwa na matusi au misamiati ya kipuuzi!

Hakika jamaa anatisha sana kuliko hata hawa 'waramba midomo' wa sasa.

Ongeza ulichoona kutoka kwa huyu jamaa!
 
Kama anakubalika na ni mzuri mbona hafiki huko walipo akina mond,,,, by the way mm ni fan wake nambari uno
 
Katika wasanii wanaoujua mziki basi kassim ni wa kwanza,hajawahi kukosea,ni msanii ambae huchoki kumsikiliza,in short ni icon ya muziki wa bongo!!í ½í²¯í ½í²¯
Sasa kama Kassim ni Icon ya bongo je Diamond Platnumz baba tifah Dangote mtoto wa tandale young bilioner, icon ya africa mashariki na kati na mashariki ya mbali a.k.a Simba, Kifaru, atakuwa nani sasa?
 
Kama nimemuelewa ni icon kwa maana ya aina ya mziki anao imba hasa utumiaji wake maridhawa wa lugha yetu hadhim ya kiswahili, ikitokeaa unamsikiliza for the first time lazima utajua ni mswahili tena wa pwani, so kwa tafsiri hiyo ni icon.
 
Kwani Bwanako Mond kafika wapi? Maana naona unajitahidi kuliziba jua kwa ungo, kwa tunaojua muziki hasa Muziki wenye mahadhi ya pwani Kasim huwez mfananisha na Mondi hata siku 1
Aiseeeh bibie mbona umeenda mbali sana ungeniuliza kwann nimesema hivyo, na kwa kukuheshimu naomba ufute hiyo kauli sawa mama, sipo hapa kwa maneno ya kwenye kanga nipo kuyajenga, na nimesema mm ni fan no moja wa kassim kutokana na aina ya mziki wake, ila tatizo linakuwa wapi kuwepo sehemu alipo diamond ili hali yeye alimtangulia kwenye game..

Kwq kutunziana heshima na0mba uombe msamaha kwa ulichokiandika hapo.
 
Kama nimemuelewa ni icon kwa maana ya aina ya mziki anao imba hasa utumiaji wake maridhawa wa lugha yetu hadhim ya kiswahili, ikitokeaa unamsikiliza for the first time lazima utajua ni mswahili tena wa pwani, so kwa tafsiri hiyo ni icon.
Ok!!
 
Back
Top Bottom