Ukweli smartphone ni tatizo kubwa kwenye familia zetu

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Habai zenu wana JF

Kama wiki moja imepita nilipata mwaliko kwa jamaa yangu fulani huko mkoani ,ni siku nyingi hatujaonana kiasi miaka kadhaa ,ukweli nilikwenda na nilianadaliwa msosi wa maana tu,
kitu kilichonisikitisha nilikuta nyumba ile smartphone zinawacontrol nyumba nzima,kuanzia jamaa yangu mke wake na wengine jamaa zake wanaoishi ile nyumba,
kawaida yangu nikiwa naongea na mtu maongzei sipendi kabisa kutumia simu sina muda wa kuchat,sasa hata nilipofika kwa jamaa yangu niliweka simu zangu mfukoni na sikuchat tena nilikaa pale kiasi cha masaa 4 hivi mpaka naondoka,
ukweli kuwa jamaa yangu akiongea neno moja anakamata simu yake anachat upande wa pili kulikuwa na wife wake na yeye ndio hivyo simu haitoki kiganjani,
ukweli sikupenda ile tabia na nikawasikitikia sana ,

kabla sijaondoka nikakwambia jamaa yangu ajitazame upya kuhusu matumizi yake ya simu yake huenda ikamuathiri zaidi,

naimani sio rafiki yangu tu hata hapa JF wenye maradhi hayo naimani wamejaa jamani simu zitazameni upya zitavunja ndoa zenu na zitavunja mahusiano yenu na watu wengine,
 
Kwetu kuna sheria kuwa kila mtu lazima aachane na simu kama kuna mko wawili au hata ukipokea simu lazima mazungumzo yawe mafupi
 
The way we are fed with information has changed. Sometimes hata ukitaka kuwasiliana na mwenzi wako vizuri zaidi, ni bora utumie simu kuliko kongea naye moja kwa moja... Siku hizi hata TV hazina mpango kama zamani...
nna zaidi ya mwezi sijaangalia tv, nikitaka mpira bar na simu yangu huku naangalia huku nachat
 
Hili nalo tatizo ila wakati mwingine namwambia ukwel coz uko na mtu mna maongezi halafu kla saa simu inakera sana
 
Hakuna mtu ananiuzi kama mtu anaruhusu simu yake iingilie mazungumzo yetu au kikao. hata boss wangu ananikera na haka kamchezo katikati ya maelekezo ya kazi anapokea simu ya kamchepuko anaongea lisaa umebaki unachoma mahindi tu
 
Back
Top Bottom