Sikwangalasyene
Member
- Jul 3, 2018
- 76
- 130
Mungu huwapenda wasemao ukweli lakini huwavumilia wasemao uongo! Ukweli lazima ubaki kuwa ukweli na uongo vivyo hivyo.
Kama taifa, tunahitaji ukweli ushamiri ili tuweze kuyafikia na kuyatekeleza malengo yetu pendwa ya maendeleo ya nchi. Ikiwa tutaukumbatia uongo na kuufanya uwe ndio ukweli basi tutabaki maskini daima na ikibidi tutarudi nyuma kimaendeleo.
Mazingira yaliyopo kwa sasa hayana afya kustawisha taifa katika misingi ya uwazi na ukweli ili kujenga mazingira ya uwajibikaji kwa manufaa ya taifa na si watu wachache wenye nafasi za uongozi. Tukisema ukweli na wenye dhamana wakauzingatia tutasonga mbele tukiwa pamoja kama taifa kinyume chake wenye dhamana tutatumia nguvu kubwa kuwaaminisha wananchi kuwa taifa lipo vizuri na linapiga hatua ilihali hali halisi inaonyesha tunarudi nyuma.
Ukweli ni upi ambao tunapaswa kujuzana?

- Biashara za ndani na nje zimevurugwa zikavurugika
- Mapato ya ndani na ya nje yameshuka
- Uwezo wa taifa kujiendesha upo shakani
- Hali ya kisiasa haina afya kwa mustakabali wa taifa
- Sekta ya elimu inadorora
- Umaskini unakithiri
- Ari ya kufanya kazi miongoni mwa watumishi imeshuka
- Matumizi ya nguvu ya dola yameshamiri
- Ubaguzi kwa misingi ya kisiasa imeshamiri
- Umoja wa kitaifa upo rehani
- Kuaminiana hakupo tena
- Utawala ni wa mtu mmoja (Autocratic)
- Uvunjaji wa katiba umeshamiri
- Uvunjaji wa haki za binadamu imekuwa jadi
- Watawala hawapo tayari kuonywa na hata kukosolewa
- Utekelezaji wa miradi ambayo haijaidhinishwa na mhimili husika
- Ukosefu wa ajira umeongezeka
- Mapato yameongezeka
- Nidhamu ya kazi miongoni wa watumishi wa umma imeongezeka
- Mhimili wa kuidhinisha mapato na matumizi kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ya nchi upo vizuri
- Demokrasia imeshamiri
- Nchi imejaa amani na utulivu
- Umaskini unapungua kwa kasi
- Kiwango cha elimu kinapanda kwa kasi
- Utawala wa sheria unazingatiwa
- Kila mhimili unafanya kazi yake kwa uhuru pasipo kuingiliwa na mhimili mwingine
- Haki za binadamu zinazingatiwa
- Huduma za kiafya zimeimarishwa
- Kwa ujumla nchi inapiga hatua kimaendeleo