Ukweli ni Kwamba sisi Wazazi wa Kiume tuna uchungu sana na Watoto kuliko Mzazi aliyeingia Labor. Njoo unipinge kwa hoja

Ukweli ni Kwamba sisi Wazazi wa Kiume tuna uchungu sana na Watoto kuliko Mzazi aliyeingia Labor. Njoo unipinge kwa hoja

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
36,228
Reaction score
60,546
Ukweli ni kuwa sisi Wababa ambao ndio Baba wa Familia hizi zote Ulimwenguni tuna uchungu sana wa Uzazi.

Uchungu wetu una maumivu makali kwenye scale ya 10/10 wakati wanawake wanakuwa na 7/10.

Unapoambiwa Mke wako yuko Labor ward( wodi ya uzazi) hali unayobaki nayo huku nje haielezeki. Maana hujui nini kinaenda kutokea. Unakuwa kwenye sintofahamu ya hali ya juu.

Maumivu yetu sio ya Mwili wa Nyama, zaidi yako ktk mtindo wa kihisia na saikolojia. Na hii ndio inauma zaidi.

Huwa hatuoneshi uchungu wa maumivu kwa show off za machozi bali kwa response/ mwitikio wa aina yake kabisa.

Ndio maana mtoto wako ukisikia anavuta bangi, ni changudoa, mla pombe kupita kiasi na kukosa heshima kwenye jamii huwa tunakufa kwa presha na msongo wa mawazo. Roho na nafsi zinauma sana.

Mwanangu wa kike amefika form 2 wewe umempa mimba wakati nina mipango naye ya kufika mbali kwa kweli sisi Wabab mnatuumiza sana nyoyo.

Kibaya zaidi kama ukiwa Mwanaume unachezea watoto wa watu na kujidai we ni kidume My friends labda ufe mapema, malipo lazima yatajibu tu.

Kama kuna mtu anadhani ana maumivu makali ya Kuzaa na kulea kama sisi Wababa basi anipinge kwa hoja. Ndio maana ugomvi mwingi kwa familia huja pale Baba anapotaka Watoto wakae kwenye mstari wakati huo huo Mama watoto anashindwa kutoa ushirikiano au hata kuonekana kipingamizi. Matokeo yake Baba anaona bora akuachie we mwenyewe upambane na hali yako.

Basi ni hayo tu ndugu zangu

No reform no elections.

Oktoba ni Matikiti
 
Pia unaweza kupima athari za maumivu baadae.....mtoto asipokaaa kwenye mstari Mama anasamehe tu hata kama mtoyo anaharibika.

Kutokana na uchungu wa Baba huwa hawezi kuchukulia jambo kirahisi rahisi.
Mama gani ana samehe usizungumzie malezi ulio lelewa wewe ukajumlisha kwa wote mkuu.Pia kusamehe sio kwamba mzazi haumii ila anakuwa hana jinsi.
 
Baba ni unsung hero.
Ila asilimia kubwa ya wamama ni wabinafsi haswa kwa watoto dhidi ya baba zao ndio maana mama anasemwa sana katika jamii. Baba anaweza kuwa anamenyeka sana ila upendo anaugawa kwa mke, watoto na wazazi wake,, jambo ambalo wanawake wengi hawaliwezi
 
Back
Top Bottom