Ukweli ni Kitu Gani?


Ukweli ni makubaliano yaliyopo kati ya vitu vitatu:

1. -- kitu tunachokifikiria
2. -- wazo juu ya kitu tunachokifikiria
3. -- maneno tunayotumia kuongea juu ya kitu tunachokifikiria

Hii ni pembetatu ya kisemantiki.

Kitu kinachoongelewa na kufikiriwa aghalabu kiko nje ya kichwa cha mtu anayefikiri.

Wazo liko katik kichwa cha mtu anayefikiri

Na maneno yako mdomoni mwa mtu anayeongea.

Nimejibu kulingana na nadharia ya kiepistemolojia iitwayo nadharia ya makubaliano ya kisemantiki.

Yaani 'correspondence theory of truth'

 
Uelewa wangu

-Ukweli ni dhana inayotumika kuthibitisha jambo au kitu.
-Ukweli ni dhahiri au halisi, kinaonekana na kuthibitishika.
.
 
Nafs (نَفْس) ni neno la Kiarabu linalotokea katika Quran, kihalisi linamaanisha "ubinafsi", na limetafsiriwa kama "psyche", "ego" au "roho". Neno hilo linahusiana na neno la Kiebrania.
Kwahiyo nafsi ni neno ?
 
Ukweli ni maelezo yanayoelezea tukio lililotokea au lililowahi kutokea sawasawa kabisa na namna lilivyokea. Kwa mfano, kama juzi niliwahi kupita shambani kwa Mzee Ibrahim Chande halafu nikaiba maembe shambani humo, halafu kesho yake tena nikakutana na rafiki yangu Mzee Kizito nikamweleza kuwa "Jana nilipita shambani kwa Mzee Ibrahim Chande na niliiba maembe", huo ndiyo ukweli, na maelezo mengine yoyote yale kinyume na taarifa hizi ndiyo uongo
 
Ukweli ni makubaliano yaliyopo kati ya vitu vitatu:

1. -- kitu tunachokifikiria
2. -- wazo juu ya kitu tunachokifikiria
3. -- maneno tunayotumia kuongea juu ya kitu tunachokifikiria
Nikiri, katika kufuatilia mambo kwenye hili jukwa, wewe ni mtu unaefuatilia mambo msingi.

Maandishi yako yanafundisha na kufanya ye yote anaetafuta kujifunza atazame upya katika yale anayoyaelekea.

I appreciate you!
 
Nikiri, katika kufuatilia mambo kwenye hili jukwa, wewe ni mtu unaefuatilia mambo msingi.

Maandishi yako yanafundisha na kufanya ye yote anaetafuta kujifunza atazame upya katika yale anayoyaelekea.

I appreciate you!
Naomba niongezee kwenye hizi hoja za Mama Amon kama ifuatavyo
1. -- kitu tunachokifikiria- na kukisema kwa wengine sawasawa na vile tunavyokifikira
2. -- wazo juu ya kitu tunachokifikiria
3. -- maneno tunayotumia kuongea juu ya kitu tunachokifikiria

Na kukisema (kitu), na kuyasema (mawazo/ maneno) kwa wengine sawsawa na vile tunavyokifikira kichwani mwetu
 
ni neno la Kiarabu linalotokea katika Quran, kihalisi linamaanisha "ubinafsi", na limetafsiriwa kama "psyche"
Wasiwasi wangu ni tafsiri hii "psyche".

"Nafsi" ni neno la kiarabu lilotafsiriwa kutoka neno la kilatini "persona."
 
Ukweli ni hali ya kuishi au kutenda mambo au jambo kwa uwazi, uaminifu na imani kadiri ya taratibu na sheria za utu binafsi,mazingira na/ au jamii iliyokuzunguka.
 
Ninaona katika maelezo yako "kuchanganya" mambo.

Kuna maumbile. Kwa mfano, usiku na mchana, giza na mwanga. Hii ni asili; asili imefanya hivyo.

Swali. Kwa mujibu wa maelezo yako, unaona "asili" amefanya uwongo na ukweli?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…