JFK wabongo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2015
- 3,887
- 3,195
Nasikia hata jina limebadilika! Siyo tena TLS tuliyoizoea, sasa waipachika TL Sasa! Wanaujua ukweli kuwa TLS haisimami badala ya jina la mtu. Wamefumbwa na kelele zizojulikana. Wanaujua ukweli kama Pilato naye alivyoujua na kukiri hadharani kuwa haoni kosa kwa yule mshitakiwa, bado alidriki kuuliza 'Ukweli ni kitu gani?'.
TLS wanaujua ukweli bado wanataka kutenda kinyume na ukweli huo. TLS ni chama cha kitaaluma siyo chama cha harakati. Huo ndio ukweli, kuingiza harakati ni kupingana na huo ukweli.
Mmoja wa wanufaika wa taaluma/ujuzi wa TLS ni serikali. TLS inakoelekea ni kuinyima serikali nafasi ya kunufaika na ujuzi wao. Wanataka TLS iwe mshindani wa serikali. Watu hao wanaujua ukweli ila bado wanauliza ukweli ni kitu gani? Yetu macho! Ngoja tuwaandalie mabirika ya maji ili pindi mkitoa hukumu dhidi ya ukweli tuwape mnawe mikono yenu. Japo bado siamini kama TLS watakubali kelele za harakati ziufunike ukweli.
Kwa wasiojua habari za Pilato, huyo ni liwali aliyemhukumu Yesu adhabu ya kifo japo hakuona hatia kwake.