Ukweli mchungu, Wafanyakazi msife moyo, Plan B ni muhimu sana

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
46,922
122,189
This is a bitter truth ! I call it a serious fact! Mfano, kama take home mtumishi unapata 800,000 kwa mwezi that makes 9.6millions per year , if take home is 1 million = 12millions per year.

Toa matumiz ya chakula , ada za watoto, umeme, maji, ving'amuzi, michango ya harusi, misiba, matibabu n.k.

Bila kutizama fursa mbali mbali zilizopo tukatumia mishahara kidogo tunayopata kama mtaji ni ngumu sana kufanikiwa. Dear members hali halisi ndo hiyo. Let us learn how to think beyond our daily blade!

Tujifunzeni ujasiliamali, nashauri tuhudhurie semina za ujasiriamali tutafakari kwa pamoja fursa zilizopo tuweze kuzitumia( tuje na ubunifu wa hali ya juu) ndiyo pona yetu kama wauguzi.

Kopa benki anzisha chochote na mdhamini wako atakuwa serikali hii unayoilaumu kutokuongezea salary.
Tutaendelea kuwa wavumilivu huku tukijipanga kustaafu mapema na kuwa entrepreneurs.

Japo kua kuongezewa mshahara ni haki yetu hata kama tunafanya plan B

C&P.
 
Walimu, madaktari na manesi wengi wakaiyafuata mawazo yako utayaona matokeo yake kwenye elimu, hospitali na vituo vya afya.
Kuna maana kubwa sana ya wengine kuwa watumishi wa umma na wengine kufanya biashara, serikali itimize wajibu wake.
 
Hata hivyo hiyo plan B inahitaji muda. Na muda wetu ndo huo ambao tunautumia zaidi tukiwa kwenye kazi zetu tunazoziita kuwa ndizo zinazotuweka mjini. Haya maisha tayari yameshaingia kirusi,poa mkuu nitaufanyia kazi ushauri wako kuwekeza kwenye ujasiriamali kupitia mshahara wangu.
 
IMG_20190501_144353.jpeg
 
Bahati nzuri wenye akili timamu tulishaanza mapema tangu awamu hii iingie madarakani. Na fundisho kubwa tulilipata pale tu makato ya bodi yalipo ongezeka mpaka kufikia 15% ya basic salary! Majibu sahihi yatapatikana miaka michache ijayo.
 
Walimu, madaktari na manesi wengi wakaiyafuata mawazo yako utayaona matokeo yake kwenye elimu, hospitali na vituo vya afya.
Kuna maana kubwa sana ya wengine kuwa watumishi wa umma na wengine kufanya biashara, serikali itimize wajibu wake.
Kama maslahi yangekuwa bora, tusingefikiria plan B maana ina athari zake pia.

Ila kwa kuwa serikali haitaki kusikia kilio cha Wafanyakazi, ni bora watu wakimbilie kwenye plan B bila kujali athari zitakazotokea kwenye utumishi wao
 
Waje wajifunze vibarua tuna ishije kwa laki 2 na 40 kwa mwezi na usipoenda kazini huna chako kikubwa kupunguza matumizi ya sifa nakutafuta plan b unaweza kujibana ukaanzisha kamradi ka kuziba mapengo..Msilie lie nasisi tunazitamani ajira zenu na mshahara huo mlio nao
 
Walimu, madaktari na manesi wengi wakaiyafuata mawazo yako utayaona matokeo yake kwenye elimu, hospitali na vituo vya afya.
Kuna maana kubwa sana ya wengine kuwa watumishi wa umma na wengine kufanya biashara, serikali itimize wajibu wake.
Hawajashauriwa waache kazi zao, Bali waangalie fursa za ziada za kuongeza vipato vyao.
 
Back
Top Bottom