Ukweli mchungu: Vyuo vya dini kama Tumaini, TEKU, SAUT, N.K ni viwango duni

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
1.Kufutiwa kudahili wanafunzi wa degree mara kwa mara, Wengi tumeshudia vyuo kibao vya watukufu0 hivi vinavyoanzia na saint xxx vikifutiwa mno udahili, Teku nahisi ni kinara

2. Huko vyuo vya uislamu nako ni vituko , hairuhusiwi kutembea au kukaa wawili mwanamke na mwanaume isipokuwa awepo mtu wa tatu, 2012 nakumbuka kuna wanafunzi walifukuzwa chuo cha morogoro kwa kujihusisha na mapenzi, Yani chuo hiki nikaona ni kama sekondari tu.

3. Mishahara kiduchu, Ukiona tu hali ya walimu ni za huruma, Kuna rafiki yangu alipata kazi hivi vyuo kufundisha degree ila akawa anapewa laki 6 kama na hapo kuna kucheleweshewa hata miezi miwili, inabidi uwe na uvumilivu, Kuna migomo ya walimu kulipwa kidogo na kucheleweshewa mishahara tumeishuhudia.
.
4.Mrundikano wa masomo, hadi kifaransa utakisoma kwa lazima na hata uwe mwislamu utajifunza ukristo, nakumbuka wanafunzi wa SAUT kuna kipindi waligoma kuhusu hii ishu, Ila hadi leo mambo yanaendelea haya.

5. Ada kubwa, unakuta chuo ada karibia 2M

6.Kwenye suala la wahitimu wa hivi vyuo kwenda kufundisha vyuo vingine vya serikali inakuwa ngumu sana, sijui kwanini wanakataliwaga, Ila mhitimu wa chuo cha serikali kwenda kufundisha huko huwa ni Neema kubwa.

6. Viongozi na Walimu kuwa na elimu ndogo, Mimi hapa chuo cha SAUT Mbeya nashangaa eti mkuu wa chuo (Principal) ni Mchungaji πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ kasomea theology wakati ukienda vyuo vingine hivi vitu inabidi uwe na PHD kabisa za mambo ya uongozi tena kuna mchujo na interviews kabisa, hupewi kuholela.

7. Walimu kuwa under qualified (chini ya kiwango) - wahitimu wa degree wanafundisha degree wenzao!!! Kweli hii ni haki!!! na wanafanya hivi nadhani ili kuepukana na gharama za kuajiri wenye masters, CPA, phd, n.k. Ushahidi nnishautoa wa huyo dogo alielipwa mshahara wa laki 6

8.Kukosekana kwa hduma za wifi, nimepiga uchunguzi vyuo vya saut mbeya na Teku hawana hivi vitu, Naonaga wanafunzi huwa wanaenda vyuo kama TIA, MUST na Mzumbe ili kupata wifi, Aibu sana hii.

9. Undugu na kujuana - ukiangalia tu uongozi wa hivi byuo ni mambo ya kujuana juana na aundugu.

Kuna vituko vingine kama mwaka flani chuo cha TEKU kilifungiwa mageti na jiji kwasababu hawakulipa tozo, ilikuwa ni aibu.

Kwa hali hii haya makanisa yaendelee kujikita na shule za sekondari ila huku vyuoni wamevamia, Na nimpongeze raisi alivyosema wanafunzi wawe wanajichagulia vyuo maana ile TCU ambayo wanafunzi walikuwa wanapangiwa vyuo ilifaidisha sana hivi vyuo, unakuta mwanafunzi anasukumiwa tu hivyo hivyo hata kama hakipendi chuo
 
...
Hii vita Ngoja nisome comments....
Utashukiwa kama mweweee....
Kama umeamua hivyo....
Ukimaliza.....
Njoo Advance Nako...

Kama mbwai mbwai tuu
 
...
Hii vita Ngoja nisome comments....
Utashukiwa kama mweweee....
Kama umeamua hivyo....
Ukimaliza.....
Njoo Advance Nako...

Kama mbwai mbwai tuu
Nimeongea facts sijasingizia kitu ndio maana nimeiita "ukweli mchungu"

Kwa advance wako poa mkuu, shule kibao kama swilla na uwata na nyingine zinafanya vizuri, kuamka ni saa kumi na nusu na kuna mboko za kutosha, ubaya ni kwamba vyuoni huwezi tumia mbinu hizi
 
Basi zungumzia Combinations nazo
 
 
Wenzako wanasoma wanaelimika wanafanya maisha wewe unakalia kufikiri Chuo gani bora. Endelea na huo Ujinga waenzako wanasonga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda kikundi cha vijana kutoka Afrika mashaiki wanakutana kwa maazimio mbalimbali , mwenyekiti anasema wenye elimu ya chuo kikuu wanyoshe mikono, Mtanzania atanyoosha kwa kutojiamini . Yote haya ni kutokana na ulichoandika .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
vijana mna mambo!

unaweza ukakaa marekani miaka 50 na usijue kingereza! we angalia ubora wa elimu wanayoitoa mambo ya malipo ya wahadhiri hayakuhusu, sometimes watu hawaweki wazi mishahara yao kwa kuwakwepa wazee, "niazime nitakurudishia wiki lijalo"then anapotelea kusikojulikana.
 
Saut main campus mbona kipo vizuri
Dadeki, kozi ambayo inabidi iwe masomo matano huko ambako unasema hamna matatizo wanasoma masomo kumi, kwa ufupi kuna matatatizo, Kaka na dada zenu walilalamikaga sana hizi ishu ila sasa hao wachungaji sijui kama wataelewa, Yani hii ni kozi ya uhasibu ila cha kushangaza uzito wa somo la basic english unafanana na uzito wa masomo ya uhasibu, Kaeni chini na hao wachungaji aisee
 

Attachments

  • 1584962055348.png
    20.1 KB · Views: 10
Wacha wasome akili ipanuke.
 
Wacha wasome akili ipanuke.
Mtu chuo kaenda kusomea taaluma ya kuwa muhasibu kuna haja ipi ya kuanza kusomea kozi za kifaransa, sijui basic english, dini, n.k hivi ni vitu vya kujifunzia sekondari ama mtu achukue kabisa kozi maalum, Haiingi akilini mkuu!!! Nimeshangazwa sana kuna kozi yao ya "Bachelor of Science in Procurement and Supply Chain Management " mtu anasomea mambo ya uhasibu badala ya kujikita na procurement πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…