Ukweli mchungu: TABATA kuna miundombinu ya hovyo sana

Mrisho com

JF-Expert Member
May 2, 2015
3,901
3,937
Kuna mteja alikuja dukan kwetu majira ya jioni na kununua bidhaa,kwenye saa kumi na mbili hivi,basi ilipofika saa mbili nami nikafunga na kutafuta usafiri ili nirudi nyumbani.

Wakati nipo kituoni nikaona namba ngeni nikapokea huku akinipa maelekezo ya hapa na pale juu ya kifaa chake na kunitaka niende kwakwe nikamuunganishie maana ameshindwa.

Basi bila hiyana nikachukua pikpik akisema yeye atalipia ndipo tukaiyanza safari kwenda huko tabata buyuni.

Nilichokiona kule,barabara za tabata ni za hovyo kuliko hata za mvuha na matombo,mpaka nikawa naongea na yule dereva wa pikpik na kumuuliza hivi huku kuna viongozi wanaoishi huku??Yaan sijui nifananishe na barabara za wapi ni pa hovyo kabisa.

Ukweli useme tofauti ya Yombo na tabata labda yombo uswahilini ila kwa miundo mbinu wapo mbali sana,kwa hali hii bora ukae yombo kwa tusio na magari kuliko kuishi sehemu yenye barabara hata ukitaka ukanunue nyanya mtihani kupita.

NARUDIA TENA

""KINACHOITOFAUTISHA TABATA NA YOMBO LABDA MAJENGO&USWAHILI TOFAUTI NA HAPO BORA UISHI YOMBO KULIKO BAADHI YA MAENEO TABATA"""

babu wa maraha,kwa sasa nipo mvuha navuna ndizi
 
Mkuu achana na Tabata,Ile ni Republic.๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ๐Ÿƒ Nifah
Huyu itakuwa alipita barabara za Kifuru kule ndanindani za kutokea Bima au Baracuda ๐Ÿ˜„
 
Zamani tulikuwa tukisikia tabata jibu la kwanza ni eneo la dampo lakini siku hizi watu wazito tu wapo huko,muda unaenda mbio sana.
 
Huko nimepapita sana nikiwa nimechelewa ndio boda walikuwa wanasema ni shortcut, yani nikifika ninakoenda tumbo lote linauma! Kuna mashimo sio poa.
Nenda yombo uone mitaa inavyowaka,barabara hugusi tope
 
Kama haujawahi kuishi daslm ukiwasikia wahuni wanavyoisikia na maeneo wanayotoka ni tofauti kabisa...daslm ina maeneo mengi wanaishi binadamu ila ni ya hovyo na machafu sana aisee..
 
yombo pako poa sana tatizo ina sehemu kubwa ambayo ni uswahilini. ila ni pazuri sana kwa factor nyingi

1. bara bara za yombo ni nzuri sana

2. yombo ni karibu sana na mjini yaani posta na kariakoo

3. yombo kuna njia nyingi za lami za kukufikisha mjini. kama una usafiri wako foleni unaikwepa kwa urahisi sana, maana unachagua upite barabara gani zote ni nzuri zina lami

4. hospitali za serikali kubwa kabisa za kisasa zimejengwa yombo zaidi ya moja. mfano yombo vituka hospitali ya ghorofa ina huduma zote, na yombo buza tena hospitali ya ghorofa na ina kila huduma

TATIZO LA YOMBO ni mitaa ya kishua yenye ustaarabu ipo michache sana, sehemu kubwa wamejaa waswahili
 
Back
Top Bottom