Ukweli mchungu ili uweze kufanikiwa kimaisha

buzitata

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
1,997
7,068
Habarin wakuu

Ngoja niende kwenye mada moja kwa moja.

Watu wengi tunatamani Sana kufanikiwa kimaisha Ila Kuna Jambo lipo nyuma ya pazia ambalo hilo ndio kikwazo cha watu wengi kuishia kulalamika maisha ni magumu.

Kwa miaka mingi tumekua tukihubiriwa kuhusu kufanya kazi kwa bidii, kutunza pesa, kuwa na mikakati mizuri nk

Ninaamin hayo yote watu huwa wanayatimiza.

Kila mtu ameshawahi kufanya kaz kwa bidii Ila matokeo yake hakuna alichopata Ila bado anaendelea kupambana tu na unawezakuta had uhai unakuishia utakua bado hujafanikiwa.

Mafanikio yamejificha kwenye IMANI
Mungu/Yesu
Mtume Mohammed/alha
Mizimu
Waganga
Uchawi

Tafuta dunia nzima hakuna mtu ambaye amefanikiwa kimaisha bila kusaidiwa na kimoja Kati ya hvyo vitu nilivyoorodhesha hapo juu

Najua ni ukweli MCHUNGU hasa kwa wale walokole lazma wataanza kukemea baada ya kuona nimeweka mizimu na waganga.

Ni kweli suala la mizimu lipo na linafanya kazi.

Kuna watu hawafanikiwi kwasababu mizimu yao haipo sawa yaan wewe upo upo tu hata hela haikai mkononi Ila bado unajipa moyo one day yes utatoboa, my friend your wrong.

Ila Kuna watu wengine mizimu yao imewakubali hata asipo fanya kitu yeye pesa anazikamata tu yaan anakua na bahati Sana huwa tunawaita Wana kismati cha hela Ila ukweli ni mizimu yao ndiyo inayowasimamia.

Kuna wengine Iman zao zipo kwenye dini, hawa mafanikio yao ni mwenyezi mungu mwenyewe ndio anatoa baraka kwao na mtu huyu huwa anafanikiwa Sana kwenye mambo yake.

Waganga,. Hapa wapo matajiri wengi sana ambao wamefanikiwa kwa kutumia njia hii, Hawa wapo ambao wameuza nafsi zao au ambao wametoa kafara ya kitu fulani ili wajipatie utajiri.

Hapa bila shaka wale ndugu zangu wa kule Njombe hawana ubishi.

Uchawi, hapa sasa ni mtu binafsi anashiriki uchawi wa kimaendeleo, kwa mfano kumroga mtu ili upandishwe cheo, kuroga wateja wawe wanakuja kwako nk.

Ndugu zangu tunajitahidi sana kupambana na maisha Ila hapa kwenye imani wengi tunachemka. Chagua kimoja ukomae nacho utatoboa. Mimi nipo kwa Yesu😁😁😁🤪 Ila msiniulize kama tayari nimefanikiwa kimaisha au la, ila nimeamua kuwafungulia code ambazo matajiri wengi hawazifungui wao wataishia kwenye:

Fanya kazi kwa bidii
Kuwa na kauli nzuri
Waheshimu watu
Jitume
Lipa kodi
Usifanye biashara haramu (japo wao wanafanya)

Mwenye akili aelewe na mwenye ubongo afunguke

BUZITATA HALICHUNWI HATA KWA LIMBWATA LA KITANGA
 
Mizimu ndio kitu gani? na inathibitishwaje kuprove kama kwei ipo?
Ndio maana ya Iman hyo mkuu
Kuamni kitu unachokiona au usichokiona,
Sasa nitaprove vipi kitu kisichooneka?
Kule njombe Kuna sehem inaitwa nyumba ng'itu Kama unahitaji kuprove nenda ukalale usiku mmoja halafu urudi uje kutengua kauli😂😂😂😂😂
 
Dogo fanya kazi achana na issue sijui mizimu,huo ni ujinga uliotukuka,weka mipango yako sawa,kua na nidhamu kwa watu na kwa fedha,maisha hayana fomula ni kujituma na kutokukata tamaa,achana na mawazo ya enzi za ujima,wenzako kwenye vita vya majimaji waliamini ukisema "Maji"eti risasi itageuka na kua maji,matokeo yake walichezea shaba kinoma!
 
Dogo fanya kazi achana na issue sijui mizimu,huo ni ujinga uliotukuka,weka mipango yako sawa,kua na nidhamu kwa watu na kwa fedha,maisha hayana fomula ni kujituma na kutokukata tamaa,achana na mawazo ya enzi za ujima,wenzako kwenye vita vya majimaji waliamini ukisema "Maji"eti risasi itageuka na kua maji,matokeo yake walichezea shaba kinoma!mafanikio ni bahati
 
Dogo fanya kazi achana na issue sijui mizimu,huo ni ujinga uliotukuka,weka mipango yako sawa,kua na nidhamu kwa watu na kwa fedha,maisha hayana fomula ni kujituma na kutokukata tamaa,achana na mawazo ya enzi za ujima,wenzako kwenye vita vya majimaji waliamini ukisema "Maji"eti risasi itageuka na kua maji,matokeo yake walichezea shaba kinoma!
Ni kweli kaka na hyo ndio maana ya code sio kila mtu lazima afungue

Ni kama tulivomshinda nduli idi amin wapo wanaoamn tulishinda ile vita kwasabab ya kuwa na jeshi imara, Ila wapo wazee walikua front watakuambia ile ngoma watz tulichakazwa vibaya mno Ila tuliokolewa na uganga wa msumbiji

Naona Kama haimake sense iv eh
 
Mafanikio ni kutimiza ndoto zako, Kama ndoto zako ni kumpata Lovenear, ukampata Sarah, na Sarah ni mzuri kuliko Lovenear, Basi hujafanikiwa.

Kama ndoto yako ni kununua BMW 3 Series, ukanunua Toyota Camry, Basi hujafanikiwa kutimiza ndoto
Sasa kunawakat unataka kutimiza hzo ndoto na unashindwa kuzitimiza

Imani sio lazima uchawi mungu pia bila Iman n kaz bure
 
Waliofanikiwa ukiwauliza wanakwambia tu, fanya kazi kwa bidii. Nafikiri kusema hivi tu haitoshi. Dunia ya sasa inataka akili nyingi kuliko nguvu.
 
Dogo fanya kazi achana na issue sijui mizimu,huo ni ujinga uliotukuka,weka mipango yako sawa,kua na nidhamu kwa watu na kwa fedha,maisha hayana fomula ni kujituma na kutokukata tamaa,achana na mawazo ya enzi za ujima,wenzako kwenye vita vya majimaji waliamini ukisema "Maji"eti risasi itageuka na kua maji,matokeo yake walichezea shaba kinoma!

You're totally, yaani 💯% WRONG
 
Hapa ni kweli kabisa maana kuna muda una work smart lakini bado unadunda tu unabaki unajiuliza hivi hapa shida nini mbna mimi tu
 
Back
Top Bottom