Ukweli mchungu ili uweze kufanikiwa kimaisha

Wachina vipi wao hawaamini chochote vipi hakuna matajiri huko kwao??
Hao ndo balaa kabisa wana imani za ajabu ajabu na hao jamaa unakuta karibia kila mtu ana mungu wake binafsi hawana mambo ya dini kama sie ila wana imani zao pia
 
Habarin wakuu

Ngoja niende kwenye mada moja kwa moja.

Watu wengi tunatamani Sana kufanikiwa kimaisha Ila Kuna Jambo lipo nyuma ya pazia ambalo hilo ndio kikwazo cha watu wengi kuishia kulalamika maisha ni magumu.

Kwa miaka mingi tumekua tukihubiriwa kuhusu kufanya kazi kwa bidii, kutunza pesa, kuwa na mikakati mizuri nk

Ninaamin hayo yote watu huwa wanayatimiza.

Kila mtu ameshawahi kufanya kaz kwa bidii Ila matokeo yake hakuna alichopata Ila bado anaendelea kupambana tu na unawezakuta had uhai unakuishia utakua bado hujafanikiwa.

Mafanikio yamejificha kwenye IMANI
Mungu/Yesu
Mtume Mohammed/alha
Mizimu
Waganga
Uchawi

Tafuta dunia nzima hakuna mtu ambaye amefanikiwa kimaisha bila kusaidiwa na kimoja Kati ya hvyo vitu nilivyoorodhesha hapo juu

Najua ni ukweli MCHUNGU hasa kwa wale walokole lazma wataanza kukemea baada ya kuona nimeweka mizimu na waganga.

Ni kweli suala la mizimu lipo na linafanya kazi.

Kuna watu hawafanikiwi kwasababu mizimu yao haipo sawa yaan wewe upo upo tu hata hela haikai mkononi Ila bado unajipa moyo one day yes utatoboa, my friend your wrong.

Ila Kuna watu wengine mizimu yao imewakubali hata asipo fanya kitu yeye pesa anazikamata tu yaan anakua na bahati Sana huwa tunawaita Wana kismati cha hela Ila ukweli ni mizimu yao ndiyo inayowasimamia.

Kuna wengine Iman zao zipo kwenye dini, hawa mafanikio yao ni mwenyezi mungu mwenyewe ndio anatoa baraka kwao na mtu huyu huwa anafanikiwa Sana kwenye mambo yake.

Waganga,. Hapa wapo matajiri wengi sana ambao wamefanikiwa kwa kutumia njia hii, Hawa wapo ambao wameuza nafsi zao au ambao wametoa kafara ya kitu fulani ili wajipatie utajiri.

Hapa bila shaka wale ndugu zangu wa kule Njombe hawana ubishi.

Uchawi, hapa sasa ni mtu binafsi anashiriki uchawi wa kimaendeleo, kwa mfano kumroga mtu ili upandishwe cheo, kuroga wateja wawe wanakuja kwako nk.

Ndugu zangu tunajitahidi sana kupambana na maisha Ila hapa kwenye imani wengi tunachemka. Chagua kimoja ukomae nacho utatoboa. Mimi nipo kwa Yesu😁😁😁🤪 Ila msiniulize kama tayari nimefanikiwa kimaisha au la, ila nimeamua kuwafungulia code ambazo matajiri wengi hawazifungui wao wataishia kwenye:

Fanya kazi kwa bidii
Kuwa na kauli nzuri
Waheshimu watu
Jitume
Lipa kodi
Usifanye biashara haramu (japo wao wanafanya)

Mwenye akili aelewe na mwenye ubongo afunguke

BUZITATA HALICHUNWI HATA KWA LIMBWATA LA KITANGA

Hakuna mstari wa kusema hapa nimefanikiwa ,kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.

Mwenye baisjeli anamuona mwenye boda kafanikiwa ,mwenye boda anamuona mwenye bajaji kafanikiwa ,mwenye bajaji anamuona mwenye carry kafanikiwa ,mwenye carry anamuona mwenye fuso kafanikiwa ,mwenye fuso anamuona mwenye mende kafanikiwa ,mwenye mende anamuona mwenye semi kafanikia etc
 
1Timotheo 6: 9 Lakini wale ambao wameazimia kuwa matajiri huanguka kwenye majaribu, na mtego, na tamaa nyingi za kijinga zenye kudhuru ambazo hutumbukiza watu kwenye maangamizi na uharibifu. 10 Kwa maana kupenda pesa ndicho chanzo cha mambo mabaya ya kila aina, na kwa kujitahidi kufikia upendo huo, wengine wamepotoshwa kutoka kwenye imani na kujichoma kila mahali kwa maumivu mengi..
 
Hakuna mstari wa kusema hapa nimefanikiwa ,kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.

Mwenye baisjeli anamuona mwenye boda kafanikiwa ,mwenye boda anamuona mwenye bajaji kafanikiwa ,mwenye bajaji anamuona mwenye carry kafanikiwa ,mwenye carry anamuona mwenye fuso kafanikiwa ,mwenye fuso anamuona mwenye mende kafanikiwa ,mwenye mende anamuona mwenye semi kafanikia etc
Sawa mkuu siku zote swali hujibiwa kwa swali au jibu

Kama hakuna mstari wa mafanikio bas pia hakuna mstari wa umaskini.

Mtu mwenye utajiri (mafanikio) huwa na nafasi kubwa ya kutatua mambo yanayomkera kwa mfano kuwa na usafiri binafsi, kula anachojiskia, kustarehe sehem nzuri

Maskini yeye huwa na wigo mdogo sana
Ni nadra kula anachojiskia, kustarehe sehem anayoitaka pamoja na mambo mengi ambayo tunayaita anasa

Hope nimekujibu
 
Unaweza tegemea vyote ulivyovitaja hapo juu nabado ukafa fukara, tena fukara wakutupwa.
Kifupi mtoa mada wewe ndio unatakiwa kufikiria njee ya box .
 
Sawa mkuu kwa kuongeza msemo mwingine
Mafanikio ni kutumia kile ulicho nacho ili upate usichokua nacho

Haswa na ndio maana hata ukienda kwa waganga watatumia ulichonacho kukupa usicho nacho.

Hata Mungu alimwambia Musa una nini Mkononi, hiyo ndio kanuni.

Ili usifanikiwe utapaswa utumie usivyo navyo kupoteza ulivyo navyo
 
Wewe ndo unatakiwa utoke nje ya box unaongea nadharia nyingi ambazo hata kuzitetea huwezi anyway ngoja nikuache mfuasi wa mwamposa jumapili ukienda tena kamwambie akuombee upate utajiri alafu umpe sadaka apeleke kwenye miradi yake yeye ndo akawe Tajiri
Lakn haya mambo ukiangalia kwa makn unaona kabsa kuna kinachofichwa ukitaka kujua uasilia wa wa watu ukiangalia movie za kinaijeria utajua tu uasilia wao pia za kichina sidhan kama yale yte tunayoyaona et wamebuni tuu labda ni asili yao
 
Lakn haya mambo ukiangalia kwa makn unaona kabsa kuna kinachofichwa ukitaka kujua uasilia wa wa watu ukiangalia movie za kinaijeria utajua tu uasilia wao pia za kichina sidhan kama yale yte tunayoyaona et wamebuni tuu labda ni asili yao
Ni kwel mkuu Ila watu wanajifanya hawaelewi
 
Back
Top Bottom