Ukweli mchungu: CHADEMA iko ICU

akilinene

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
514
433
Kwa yeyote anayeifuatilia vyema CHADEMA bila unafiki na bila mhemuko atakubaliana na ukweli kuwa chama kiko ICU.

Baadhi ya makamanda wenye kuona mbali wameshaliona hili na wengi wamelieleza vyema. Kwa wale wasioona mbali na wengine wanaoongozwa tu na mihemuko bahati mbaya hawajaliona hili. Kila ukweli huu ukieleza wanatoa matusi na kudai walielezwa miaka mingi kwamba Chadema ingekufa lakini haijafa. Pengine kuna ukweli, lakini kuishi miaka mingi na kutokufa miaka ya nyuma haikuzuii kufa baadaye ama kwa uzenbe au naturally. Chama kinakufa.

Ukisikiliza maelezo ya Mnyika kwenye Press ya leo tarehe 21 October 2021 unaona kabisa kuwa chama kina umbwe ya uongozi, hakina mwelekeo na hakina washauri. Mnyika hatoshi, Lissu hatoshi na Mbowe pia hatoshi kwa siasa za sasa.

Makamanda kama mko wajanja anzisheni chama kingine na mje kwa namna nyingine inayogusa zaidi wananachi. Ajenda ya Katiba mpya haina mshiko kwa wananchi. Mtu asikudanganye,mtaji wa siasa ni watu. Hoja hata iwe nzuri namna gani bila kupata support ya watu hautoboi.

Makamanda kama kweli mnapenda upinzani anzisheni chama kingine na mje upya.
 
Naomba ni kueleze kitu kizuri tu !

Mpaka leo maadui zangu katika maisha yangu wamekonda kwa ajili yangu na kuniuliza kuwa na pumulia milija.ila nipo imara kama mbowe

Kiufupi wewe ni adui ulipo ccm ukiniuliza mimi mwanachadema kama nilivokueleza.
 
Wengi walioisingizia chadema kufa wamekufa wao , yuko mmoja hata mashada ya maua juu ya kaburi lake hayakauka bado
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Chadema kama Brand haiko ICU bwashee!
Bwashee, A brand is a voice and a product is a souvenir. Kwa chadema hiyo voice inakufa ndiyo maana hata products za voices zake hazionekani.

Angalia tu hata waandishi wa habari walioitikia wito wa press yao. Kila siku idadi yao inapungua. Mitaani ndiyo kabisa!! wanaozungumzia chadema na kesi ya Mbowe ni wachache mno na kila kukicha idadi inapungua. Ndiyo vyama vinavyokufa hivyo.
 
Chadema haiwezi kufa kwa sababu ndio chama pekee cha upinzani chenye sura ya kitaifa yaani kipo katika mikoa yote ya Tanganyika na Zanzibar!
 
Wengi walioisingizia chadema kufa wamekufa wao , yuko mmoja hata mashada ya maua juu ya kaburi lake hayakauka bado
Lakini bado haizui Chadema kufa. Katika maisha wengi wanasingiziwa mara kadhaa kufa lakini haizuii wao kuja kufa kwa ukweli baadaye. Chadema isipopata tiba ya haraka ICU ilipo, itakufa kiukweli.
 
Hoja iliyowapa umaarufu ni kupinga ufisadi,tangu Lowassa wampokee wamekuwa hawaeleweki wanasimamia Nini hasa.
Ukisema demokrasia wanapigania itakuwa utani,maana ndani ya chama Mbowe haguswi.
Walisema katiba! ya kwao ndo kichefuchefu Mwenyekiti ni Yule Yule mkwilima.
 
Chadema haiwezi kufa kwa sababu ndio chama pekee cha upinzani chenye sura ya kitaifa yaani kipo katika mikoa yote ya Tanganyika na Zanzibar!
Mkuu recall historia ya nchi yetu, vyama vya NCCR MAGEUZI enzi za Mrema leo vikoje . KANU nchini Kenya ilikuwa kila mahali, leo iko wapi. ZAPU nchini Zambia, leo iko wapi. Ni vyingi vimekufa.
 
Chadema ipo ICU kwa kesi za ugaidi

Chadema ingekuwa imekufa msingeiba uchaguzi 2020

Pumbavu zenu
 
Back
Top Bottom