Ukweli lazima usemwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli lazima usemwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by carnys, Apr 16, 2012.

 1. c

  carnys Senior Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naona bado ukweli unapotoshwa kuhusu umiliki wa eneo la Efatha, Mwenge. Soma hizi data hapa na kama kuna mtu mwenye data tofauti pia aziweke hadharani ili tuzijue na kupata ukweli:  EFATHA FOUNDATION LTD
  P.O BOX 32174, MWENGE, DAR ES SALAAM
  TELEPHONE: +255732993196, FAX:+255732993196
  WEBSITE:
  www.efathafoundation.org
  EMAIL: efathafoundationltd@yahoo.com / info@efathafoundation.org
  OUR REF: EFL/ADMN/4/2012
  DATE:
  11th April, 2012

  TAARIFA KWA UMMA

  1. UMILIKI WA KIWANJA NA. 90, ENEO LA MWENGE (NURU CENTRE)

  1.1 Utangulizi

  Tarehe 9 mwezi April 2012, Jumatatu ya Pasaka,baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza
  habari ya umiliki na matukio yaliyotokea katika eneo hilo. Habari zilizotangazwa ni za
  upande mmoja na hazina usahihi. Huduma ya Efatha inapenda kuelezea umma taarifa
  sahihi juu ya upatikanaji wa kiwanja na 90, umiliki na matukio yaliyotokea katika eneo
  hilo.

  1.2 Upatikanaji na umiliki wa eneo

  Serikali kupitia Tume ya Kurekebisha na Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC)
  ilitangaza zabuni ya uuzwaji wa eneo la Mang’ula Mechanical and Machine Tools
  Company Ltd iliyofilisika, Kiwanja namba 90, Mwenge katika magazeti ya Uhuru na Daily
  News ya tarehe 4 mwezi Mei 2005.

  Tarehe 18 Mei 2005, huduma ya Efatha kupitia kitengo chake cha uchumi, Efatha
  Foundation Ltd, ilipeleka maombi ya zabuni ya kununua eneo hilo PSRC.
  Efatha Foundation Ltd ilipokea barua kutoka PSRC yenye kumbukumbu Na.
  PSRC/1/13/93 ya tarehe 30 Mei 2005 ikiarifu kwamba zabuni yetu ya kununua eneo hilo
  imeshinda kwa kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia nne.

  Masharti ya Malipo ya zabuni yalikuwa asilimia kumi ilipwe wakati wa kupeleka maombi
  na asilimia tisini ilipwe ndani ya miezi mitatu baada ya kushinda zabuni.

  Efatha Foundation Ltd ililipa shilingi milioni arobaini yaani asilimia kumi ya bei siku ya
  kupeleka maombi ya zabuni kwa hundi Na. 000261 ya benki ya Azania na kupewa risiti
  ya PSRC Na. 6956 ya tarehe 31 Mei 2005. Na shilingi milioni mia tatu sitini ililipwa kupitia
  hundi Na. 000319 ya benki ya Azania ambayo ni asilimia tisini tarehe 10 mwezi Juni 2005
  na kupewa risiti ya PSRC Namba 6984 na hivyo malipo yote yakawa yamekamilishwa.

  Baada ya kukamilisha malipo Efatha Foundation Ltd ilikabidhiwa hati miliki Namba
  41641 ambayo ilipelekwa wizara ya Ardhi ili ibadilishwe jina kutoka mmiliki wa mwanzo
  na kuandikishwa jina la Efatha Foundation Ltd. Kwa hiyo Serikali ikahamisha umiliki
  kutoka Mang’ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika kwenda
  Efatha Foundation ltd tarehe 15 Novemba 2005 saa sita kamili mchana kwa uhamisho
  Namba 98648.

  Kabla ya Huduma ya Efatha kununua eneo hilo kulikuwa na wavamizi ambao ni
  makampuni na watu binafsi kumi na moja ambao walikuwa wamewekwa katika eneo
  hilo na Mang’ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika bila kibali cha
  mfilisi yaani PSRC. Kwa kuwa hawakuwa wapangaji halali walikuwa wavamizi
  (trespassers). Wavamizi hao wakapewa notisi ya kuondoka na PSRC lakini
  hawakuondoka. Baadae shughuli za mfilisi, PSRC, zikachukuliwa kisheria na Consolidated
  Holding Corporation (CHC). CHC nao wakawapa wale wavamizi notisi kuwa waondoke
  kwa sababu eneo hilo limeuzwa lakini hawakuondoka. Efatha Foundation Ltd ilipomiliki
  eneo hili kihalali na kisheria wakawapa wavamizi notisi ya kuondoka mwaka 2005,
  wavamizi nane wakatii amri wakaondoka na wavamizi watatu walikaidi kuondoka
  ambao ni pamoja na Afro Plus Industries Ltd.

  Baada ya hapo wavamizi watatu waliokataa kuhama wakafungua kesi mahakamani
  dhidi ya Efatha Foundation Ltd wakipinga kuhamishwa.

  Ni vyema ieleweke kuwa Efatha Foundation Ltd iliponunua eneo hili thamani yake
  ilijumuisha majengo yaliyokuwa yamejengwa humo na Mang’ula Mechanical and
  Machine Tools Company Ltd iliyofilisika. Hii ni pamoja na jengo alilokuwa anatumia Afro
  Plus Industries Ltd ambalo linalalamikiwa kubomolewa na kwamba tumeharibu mali.
  Jengo lililobomolewa ni mali ya Efatha Foundation Ltd na siyo mali ya Afro Plus
  Industries Ltd kama ilivyodaiwa.

  2. UVAMIZI WA POLISI NDANI YA KANISA LA EFATHA MWENGE

  Tarehe 9 Aprili 2012, jumatatu ya pasaka, majira ya saa kumi na mbili asubuhi waumini
  wa Efatha walikuwa katika ibada ya morning glory katika kanisa la Efatha Mwenge
  wakiongozwa katika ibada hiyo na Mchungaji David Mwakisole ndani ya kanisa. Kanisa
  limezungushiwa ukuta pande zote nne na lina mageti ya kuingilia kanisani ambayo
  yanafungwa. Polisi walipanda ukuta wakachungulia wakasikika wakisema hawa huku
  ndani. Baadae polisi wakarukia ndani kupitia ukutani. Wakati ibada inaendelea ghafla
  waumini walivamiwa kutoka nje na watu ambao baadae walitambuliwa kuwa ni polisi.
  Walipoingia kwa nguvu wakatupa mabomu ya machozi ndani ya kanisa huku wakifyatua
  risasi za moto wakati ibada ikiendelea. Kwa kitendo hicho ibada ilivurugika na kusimama
  na waumini wakaanza kukimbia ovyo ndani ya kanisa. Risasi na mabomu ya machozi
  yalitupwa kuelekea madhabahuni na kuelekea kwa waumini waliokuwa katika ibada.
  Waumini wengine waliokuwa wakija kwenye ibada walizuiliwa nje na kukamatwa.
  Kilichofuata ni vurugu huku waumini wakikimbia na polisi wakiwapiga kwa virungu,
  vitako vya bunduki na mateke. Baadhi ya waumini walijeruhiwa vibaya sehemu
  mbalimbali za mwili na ukumbi wa kanisa ulitapakaa damu. Pia polisi walivunja
  madirisha, viti, milango na spika kama ilivyoonyeshwa katika baadhi ya vyombo vya
  habari hasa ITV. Kabla hawajavamia, mmoja wa askari aliwatahadharisha wenzake kuwa
  wasipige mabomu na risasi kwa kuwa hapo ni kanisani lakini wenzake walipinga
  wakisema kuwa huyu mtu ana kiburi na watu hawa ni wakorofi. Wakati risasi na
  mabomu yakipigwa baadhi ya askari walikuwa wakiokota maganda ya risasi na mabaki
  ya mabomu ya machozi ili kuondoa ushahidi. Hata hivyo baadhi ya risasi za moto,
  maganda ya risasi za moto na mabaki ya mabomu yalibaki kanisani na yamehifadhiwa
  mahali maalum kwa hatua zaidi.

  Kanisani kulikuwa na idadi ya waumini kati ya sitini na sabini waliokuwa wanaabudu.
  Polisi waliwakamata jumla ya waumini 53 pamoja na wachungaji waliokuwa wakiongoza
  ibada wakiwapiga na kuwasweka katika magari ya polisi kuwapeleka kituoni pamoja na
  kuvuta gari zilizokuwa zimeegeshwa nje ya kanisa kwa breakdown. Tumepata habari
  kuwa walikuja na baadhi ya waandishi wa habari walioandaliwa kabla ili kurekodi tukio
  hilo na ushahidi tunao. Kwetu sisi inaonyesha kuwa tukio hilo liliandaliwa kwa makusudi
  ili likatekelezwe katika kanisa la Efatha. Tukio hili linatupa hisia kuwa kuna chuki kubwa
  kwa Huduma ya Efatha.

  Kitendo cha polisi kuvamia na kuvuruga ibada ni kinyume na sheria na katiba ya jamhuri
  ya Muungano wa Tanzania iliyoweka uhuru wa kuabudu na sheria za nchi zinazoeleza
  kwamba ibada ziheshimiwe na zisiingiliwe. Tunajiuliza kulikuwa na tatizo gani polisi
  wasisubiri nje ibada iishe na wawachukue watu wanaotaka kuwachukua. Ndani ya
  kanisa hakukuwa na vita, wala mtu mwenye silaha, wala mtu anayeuawa ambaye polisi
  walilazimika kwenda kumwokoa. Sisi tunaliona hili kuwa ni kumdharau Mungu,
  kuvuruga ibada na kuwadhalilisha waumini wa Efatha waliokuwa wakitumia uhuru wao
  wa kuabudu. Leo wamefanya hivyo kwa dharau ndani ya kanisa la Efatha, kesho
  tutegemee watakwenda kufanya nini kwa dhehebu jingine, Msikiti, Dini nyingine au
  watu waliokusanyika kihalali na kwa sababu halali?

  3. MAJUMUISHO

  Vielelezo vyote kuhusu umiliki wetu halali wa eneo hili vilishawasilishwa polisi mkoani
  na wilayani. Kutokana na maelezo haya Efatha Foundation Ltd inapenda kuuthibitishia
  umma kuwa EFATHA FOUNDATION LTD ndiyo mmiliki halali wa KIWANJA NA. 90, ENEO
  LA MWENGE (NURU CENTRE) na si vinginevyo.


  KATIBU
  EFATHA FOUNDATION LTD
   
 2. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Matapeli wa kidini hawa.
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  pelekini mahakamani sasa wanataka justify kuwa wako sawa kuvamia kiwanda na kubomoa
  yesu aliheshimu mamlaka zilizokuwapo iweje hawa wanaojichukulia sheria mkononi
  afu isitoshe mtume na nabii wao anatuma ila hashiriki
   
Loading...