Ukweli kuhusu wimbo wa Malaika

Kwa kufuatilia mabishano kama haya utajua kuwa waafrika na watu weusi kwa ujumla tuna tatizo moja kubwa sana ambalo mababu zetu walilifanya na litatugharimu mpaka kesho. Tatizo hilo ni lack of documentation. Kila kitu kilikuwa ni kuhadithiana kwa mdomo tuu bila maandishi au vitu kuwa rasmi. Hakuna aliyehangaika kuweka vitu kimaandishi kabisa. Tatizo kama hili limepelekea mpaka leo wamarekani weusi hawajui exactly asili yao kwa Afrika ni sehemu gani hasa. Wengine watakuambia Ethiopia, Senegal, Nigeria n.k yaani kila mtu anavyojisikia. Ukiangalia vizazi ambavyo vimepita tangu wapelekwe utumwa ni vichache sana kupoteza kumbukumbu kubwa kama ya wametokea wapi Afrika! Tatizo hili pia lipo upande wa Afrika hakuna kumbukumbu au hesabu ya waliochukuliwa utumwa upande huu na walipelekwa wapi na akina nani?
 

Ni kweli ila kumbuka kuwa yapo matukio muhimu mengi sana yaliyotukia Afrika na pia hata Ulaya na still they are controversal na sababu ni kwamba there are no vivid and clear evidences to support their existances na hii inatokana na
-Kutokuwa na knowledge n skills ya kudocument kwa wahusika wa hizo events.

-Kutokuwa na vifaa muhimu vya kuhifadhia hizo kumbukumbu kwa miaka hiyo. Mfano ni huu wimbo maarufu wa Mtz mwenzetu wa mwaka 1946-47,hata hao wamarekani weusi wa miaka hiyo tatizo lao ni hilo hilo.
 
Naomba mnisaidie kujua jina la wimbo wa aei afrika u naopigwa radio DW wanapokuwa wanasoma Habari za Africa...naupenda sana ila sijui muimbaji...

Mtunzi na muimbaji na Franklin Boukaka, ni muimbaji na alikua ni mwanaharakati wa kupigiwa mfano ambae aliuawa wakati wa jaribio liloshindwa huko Congo ya Brazzavile
Aliuawa mwaka 1972 Akiwa na umri wa miaka32.
 
Mtunzi na muimbaji na Franklin Boukaka, ni muimbaji na alikua ni mwanaharakati wa kupigiwa mfano ambae aliuawa wakati wa jaribio liloshindwa huko Congo ya Brazzavile
Aliuawa mwaka 1972 Akiwa na umri wa miaka32.

Ingia youtube andika LE BOUCHERON.ukipata tafsiri ya wimbo huo ndio utajua ni kwa nini aliuawa.
 
natamani sana kuijua historia halisi ya huu wimbo. comments za humu zimenichanganya tu
 
Nakubaliana kabisa na "Black Sniper" kwamba wimbo wa "malaika" uliimbwa na Adam Salim. Baba yangu (marehemu) alikuwa na gramophone (ambacho ni chombo kilichokuwa kinatumika kucheza muziki uliokuwa umerekodiwa kwenye sahani ya santuri). Baba alikuwa amenunua sahani ya santuri yenye wimbo wa "malaika" zaidi ya miaka kumi kabla ya uhuru. Uhuru ukipatikana nilikuwa shule ya msingi lakini karibu miaka kumi kabla nilishasikia huo wimbo wa "malaika" kwenye santuri ya baba. SIO Fadhili Wiliam aliyeutunga bali yeye aliupiga kwenye gita la umeme , akaurekodi kwenye studio ambayo iliandikisha hatimiliki ya wimbo huo. Huo wimbo wa malaika ulikuwa unaimbwa kabla ya uhuru pamoja na nyimbo nyingine maarufu kama 'Embe Dodo' na "Dereva Kombo'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtumzi ni Adam Salim alikuwa ni Mtanzania aileishi Nairobi, na alikuwa ni mechanics wa magari alimuimbia Halima mnamo mwaka 1945-46
Kweli mtunzi original ni Mzee ADAM Salim Mallya mkibosho, alimtungia Halima Maruwa msichana aliyempenda ila wazazi wa msichana wakamwozesha tajiri chitora baada ya kuona Adam hakuwa njema saaana, ndipo Adam katika udhuni na kunung'unika yake akatoka na wimbo "wimbo wa malaika' kibaya zaidi akusajili/ hakuomba hati miliki. Hii ilifanya fadhili William mkenya Kwa namna yake Kwa vile alikuwa tajiri na mmiliki studio akajimilikisha na kuwa na hati miliki yeye, na amefaidika kweli kweli huyu fadhili Kwa kulipwa na waliorudia rudia wimbo hapa Dunia huku Mzee ADAM Salim akiachwa bila kitu. Watu au makundi maarufu waliorudia wimbo malaika' kama BONEY M amemwa acknowledge MZEE ADAM SALIM KAMA MTUNZI WA KWANZA.
Mzee ADAM ni marehemu alifariki mwaka 90 au 80 mwishoni.
 
Wakenya kwa haya ni kawaida
Kweli kabisa na wakenya kwa kuiba na kusema ni vyao kawaida sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…